WAKATI vifo mfululizo vikitokea Mei mwaka huu miongoni mwa wasanii maarufu nchini, nyota wa filamu Bongo, Devotha Mbaga ameibuka na kusema endapo ataaga dunia, hahitaji kufanyiwa mbwembwe wakati wa msiba na mazishi yake kama wasanii wengine walivyofanyiwa.
Akistorisha na gazeti hili, Devotha alisema hatahitaji kununuliwa jeneza la kifahari, bali lichongwe kwa mbao za kawaida na lisiwekwe mapambo yoyote, watu wasilie msibani kwake na kwamba endapo vitu hivyo vitakiukwa, basi mwili wake utagoma kubebeka.
“Unajua duniani nimekuja uchi, sasa siku nikifa sitaki mbwembwe za kununuliwa jeneza la mamilioni wakati nimeacha watoto, ni bora hizo fedha wapewe wanangu ziwasaidie, vivyo hivyo pia sitaki watu walie kwa kuomboleza kwenye msiba wangu kwa sababu watakuwa wananiumiza tu, hata watoto na ndugu zangu nilishawaambia,” alisema Devotha.
Katika misiba ya hivi karibuni ya wasanii nyota, imeshuhudiwa kamati mbalimbali zikiundwa na kuchangisha fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitumika kununulia majeneza ya bei mbaya, vyakula vya gharama na shughuli zingine ikiwemo ukodishaji wa magari ya kusindikiza msafara wakati wa mazishi.
0 comments:
Post a Comment