Wednesday, 4 June 2014

DENTI ALIYESUBIRI KIFO, AFARIKI

...
NASWAYETU BLOG


MIBURO Anne, msichana mwenye umri wa miaka 17 aliripotiwa katika gazeti hili Mei 27, mwaka huu ikiwa na kichwa cha habari ‘NINASUBIRI  MUNGU AICHUKUE ROHO YANGU’, amefariki dunia wiki iliyopita akiwa njiani kurejea nyumbani kwao, nchini Burundi.
Add caption
Marehemu Anne aliyefariki akiwa na umri wa miaka 17 enzi za uhai wake.
Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akisumbuliwa na uvimbe mwilini, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako ugonjwa wake ulishindwa kutibika.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, mwanafunzi huyo alianza kuumwa tokea akiwa kidato cha pili, hali iliyomlazimu kuacha kwenda shule ili kufuatilia matibabu, ambayo yalimfikisha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Marehemu Anne akiwa na uvimbe uliosababisha kifo chake.
Kaka wa marehemu aliyetambuliwa kwa jina moja la Albert alisema mdogo wake alipoteza maisha wakiwa mpakani mwa nchi hizi mbili na kwamba alimhangaikia sana ili aweze kupona licha ya uwezo wake mdogo kifedha.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger