Wednesday, 4 June 2014

PICHA:MAMA ZITO AKIWA NA MWANAE ENZI ZA UHAI WAKE KABLA YA MAUTI

...

Bi. Shida Salum Mohamed enzi ya uhai wake.


Mwenyekiti  wa Taifa wa Chama cha Walemavu Tanzania (Chawata), Shida Salum Mohamed, aliyefariki dunia juzi (Jumapili) wakati akiendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Ami, Masaki, Dar es Salaam, aliteseka kwa miezi tisa kabla ya kifo chake.
Mwili wa marehemu Shida Salum ukiandaliwa kwa ajili ya kuombewa siku ya jana kabla ya mazishi yalifanyika siku ya jana mkoani Kigoma.
Shida ambaye ni mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, alianza kusumbuliwa na maradhi ya saratani ya shingo ya kizazi Agosti, mwaka jana, ingawa hali yake ilimpa afadhali nyakati kadhaa.
Viongozi mbalimbali wakishiriki kuombea mwili wa marehemu.
Hata hivyo, Uwazi limebaini kuwa hata kabla ya Agosti mwaka jana, Shida aliwahi kuzidiwa na maradhi ambapo Zitto alimpeleka India kwa matibabu, ingawa haijafahamika wakati huo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani.
Watu waliojitokeza katika mazishi ya mama yake Zitto yaliyofanyika siku ya jana mkoani Kigoma.
Kwa mujibu wa Zitto, baada ya Shida kuugua Agosti mwaka jana, alipatiwa matibabu kisha hali yake iliimarika na kuanza kufanya shughuli zake za kawaida.
“Tulikuwa na matumaini makubwa sana kwa wakati huo kwa jinsi maendeleo yake yalivyokuwa lakini Februari mwaka huu ghafla mambo yalibadilika,” alisema Zitto.
MASKINI HAKUWEZA KUAPISHWA KUWA MBUNGE WA KATIBA
Mapema mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, alimteua Shida kuwa mmoja kati ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba katika kundi la 201 kutokana na nafasi yake ya uenyekiti wa Chawata.
Shida ambaye ni mwanachama wa Chadema, vilevile mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, alikwenda Dodoma Februari mwaka huu kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba lakini wakati anasubiri kuapishwa hali yake ilibadilika.
Mwili wa marehemu Shida Salum ukiombewa kabla ya mazishi huko mkoani Kigoma.
Zitto aliliambia gazeti hili kuwa baada ya hali ya mama yake kubadilika, alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alianzishiwa matibabu kabla ya kusafirishwa kwenda India kwa matibabu zaidi.
 Alisema, baada ya kutoka India aliendelea kutibiwa nyumbani katika kipindi ambacho hali yake ilikuwa na nafuu lakini ilipobadilika tena, alipelekwa Ami ambako alitibiwa mpaka mauti yalipomkuta.
MAZISHI KIGOMA
Mwili wa Shida, ulisafirishwa kwa ndege juzi alasiri na mazishi yalifanyika siku ya jana mkoani Kigoma.
Viongozi mbalimbali kutoka vyama tofauti vya siasa, walikuwa bega kwa bega na Zitto kuanzia Hospitali ya Ami na baadhi walisafiri kwenda kushiriki mazishi ya Shida.
Zitto akiwa na mama yake enzi za uhai wake.
Baadhi ya viongozi waliokuwa bega kwa bega na Zitto ni wabunge, Catherine Magige, Grace Kiwelu, Edward Lowassa, Nimroad Mkono, Halima Mdee, Deo Filikunjombe, Murtaza Mangungu, Ester Bulaya, Hamisi Kessy na wengine wengi, huku maveterani wa siasa na taaluma nchini, Dk. Salim Ahmed Salim,  Profesa Philemon Sarungi na Profesa Issa Shivji wakishiriki kikamilifu.
Sisi Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Sote Tutarejea.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger