Waamuzi 25 wa FIFA watachezesha mechi za Kombe la Dunia. Waamuzi hao wanatoka katika mabara yote sita, na wote watachezesha angalau mechi isiyopungua moja. Waamuzi hao na wasaidizi wao watakuwa wakifuatiliwa kwa karibu na kupewa kila msaada wanaohitaji na FIFA ili waweze kuchezesha kwa haki.
Afrika kupitia CAF inawakilishwa na Noumandiez Doué (Ivory Coast), Bakary Gassama (Gambia) na Djamel Haimoudi (Algeria). Mwamuzi aliyechezesha fainali ya mwaka 2010 Howard Webb kutoka England ni miongoni mwa waamuzi walioteuliwa kutoka UEFA
0 comments:
Post a Comment