Cha kushangaza watu hao walimvamia
askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH NGONYANI na
kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha aina ya SMG ikiwa
na risasi 30.
Ndipo walipoanza kushambulia kwa
risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30.
Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka
kusikojulikana.
Askari Ngonyani alifariki dunia
alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga.
Askari mwingine aitwaye VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo
bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia.
Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni.
Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa
Hospitali hiyo aitwaye VERONICA MUSIME, anathibitisha askari huyo
kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine
wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina.
Kazi ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe
makini sana na staili hii ya ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na
majeruhi hawa ni kuwapata watuhumiwa wote na silaha walizoiba
bila kuchelewa. Bila kujali mkoa ulipo, taarifa za haraka tunatarajia
kupata toka kwako kuhusiana na wahusika wa tukio hili. AMEN
0 comments:
Post a Comment