IMEBAINIKA kuwa
miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai kufanyishwa ngono na waganga wa
kienyeji ‘sangoma’ ili kupata ujauzito baada ya kukaa muda mrefu
bila watoto, wamo wake wa vigogo Bongo, Uwazi limechimba.
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu
kwa baadhi ya wanawake hao umebaini kuwa, waume wao wanafanya kazi
katika nyadhifa za juu serikalini, wengine ni wastaafu na kwamba waume
hao hawajui kinachoendelea.
Kwa mujibu wa mwanamke mmoja(jina lipo),
katika sakata hilo kuna wake wa maprofesa, kanali mstaafu wa JWTZ na
mmoja ambaye mume wake aliwahi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa (RPC)
ambaye kwa sasa naye ni mstaafu.
...Kamanda Kiondo akizidi kuonyesha vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na waganga hao wa kienyeji.
Mwanamke huyo alizidi kudai kuwa, ndoa
moja katika hizo ilivunjika baada ya mume kubaini kuwa, mkewe alikuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa sangoma hao.
‘KUFULI’ ZILISHATUMIKA
Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo za ndani ‘kufuli’ za wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa na polisi kwa sangoma hao maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam zilikuwa zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa wakati wa tukio linalodaiwa lilikuwa na kutengezea dawa.

Baadhi ya watuhumiwa wa sakata hilo.
KWA NINI WALITOA TAARIFA POLISI?
“Sisi tuliamua kutoa taarifa polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono na wale waganga kwa muda mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi tulishatumia mamilioni ya pesa baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo nyumba,” alisema mwanamke huyo nje ya kituo cha polisi.

Wanawake hao ambao hawakupenda majina
yao yatajwe kwa kuhofia waume zao kujua, walisema ni kweli baadhi yao
wamekaa katika ndoa kati ya miaka nane hadi 10 bila kupata watoto wala
mimba zilizoharibika.
Kamanda
Kiondo akionesha baadhi ya nguo za ndani, 'kufuli' zilizokutwa kama
ushahidi kwa baadhi ya wanawake waliofanyishwa ngono na sangoma hao.
Hata hivyo, baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga hao.
KAULI YA RPC
Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu.
Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu.
Kamanda Kiondo akikusanya tunguli zilizotumiwa na waganga hao wahalifu tayari kwa kuzichoma moto mbele ya wahandishi wa habari.
Vitu hivyo viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya waandishi wa habari.
“Ninaamini kuwa kwa vitendo hivyo vya kujamiiana ni hatari na huu ni ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi mbalimbali ikiwemo Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema Kamanda Kiondo.

...Tunguli zikiteketezwa kwa moto.
Waliokamatwa katika zoezi hilo ni Juma Mohamed (32) na Abdallah Musa (25) ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo.
0 comments:
Post a Comment