Unaweza
kuona ni kiasi gani maisha ya kupanda na kushuka kwa kila mtu kwani kwa
upande wa O-ten mambo hayamuendei vizuri kabisa kwa kifupi anahitaji
maombi ya mama Rakwatare kwani hali yake sio na ulevi aka gambe
limepitiliza.
O-ten aliye-hit na ngoma yake kali ya nicheki na baadae kuwa muhimili mzuri wa East Coast team iliyokuwa chini ya Crazy Gk na member kama Mwanafa na Ay, mkali huyo kwa sasa yuko Moro town ambako ndio home kwao, baada ya nicheki tunakaamua kumcheki tulimpomkuta kidogo ikawa shida kwani alikuwa gambe mbaya na huku uso wote ukiwa na manundu tena akilia kama aliyefiwa.
Baada
ya kutaka kujua undani ya yaliyomkuta ndio akafunguka kwamba amepigwa
sana na vijana bila ya sababu yeyote lakini tulipofuatilia tukaona ni
suala la ulevi wa kupindukia.
0 comments:
Post a Comment