MVUTANO mkubwa
umeibuka juu ya wapi azikwe marehemu Nasra Mvungi, mtoto aliyeishi
ndani ya boksi kwa miaka minne baada ya kufariki dunia hivi karibuni
katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mwili wa mtoto Nasra Mvungi ukishushwa kwenye gari ndani ya Uwanja wa Jamhuri Morogoro kuagwa.XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Habari zilizopatikana mjini hapa, zinasema kuwa mzozo umeibuka kwa ndugu
wa marehemu Nasra ambapo baba yake mzazi, Rashid Mvungi na bibi wa
marehemu, Asha Abdallah (mama mzazi wa mama wa marehemu ambaye pia ni
marehemu) kila mmoja akitaka kuuchukua mwili wa Nasra na kuuzika.
“Mjukuu wangu nina uchungu naye sana, nakumbuka mengi sana kuhusu yeye.
Nataka kumzika mwenyewe. Hapa nilipo nimeshaagiza maturubai kwa ajili ya
kuweka msiba nyumbani kwangu,” alisema Bi. Asha kwa masikitiko.
Risasi Mchanganyiko liliwasiliana na Ofisa Ustawi wa Jamii, Mkoa wa
Morogoro, Osward Ngungamtitu na kumsimulia kuhusu mvutano huo wa
kifamilia, ambapo alisema wao kama chombo cha serikali ndiyo wanaohusika
na msiba huo.
“Sasa hivi (juzi Jumatatu saa 7 mchana) tunapita Chalinze, tunakuja na
maiti huko Morogoro. Sisi kama serikali kwa kuwa ndiyo tuliosimamia
matibabu ya Nasra, sisi ndiyo tutasimamia pia maziko yake.
Wanatofautiana bure tu.
“Tutafikisha maiti mochwari hapo Hospitali ya Mkoa halafu ataagwa katika
Uwanja wa Jamhuri kabla ya mazishi siku hiyohiyo (jana).”
0 comments:
Post a Comment