“Sijawahi
kuona mwanamke mzuri na mwenye imani kama mama Komba ( Salome )
jamani, unajua kulea watoto ambao mama zao wapo duniani ni
kazi sana,”alisema Komba katika kipindi cha mkasi kinachorushwa na East African Television
Mheshimiwa Komba alisema ana watoto
tisa wakiwemo wa ndani ya ndoa na nje ya ndoa na wote
wamelelewa na mke wake Salome na ndio maana anampenda na
kumjali kila siku za maisha yake kwani anastahili kuitwa
mwanamke haswa…..
John Komba aliyasema hayo siku
chache baada ya kuonekana picha zake mbaya za kimahaba
alizopiga akiwa na msichana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake…..
Katika mahojiano na kipindi cha
Mkasi, John Komba aliongelea mambo mengi na kusema kuwa ukiwa
kiongozi na mtu mkubwa nchini ni lazima uzushiwe mambo
yakiwamo maradhi makubwa na kashfa mbalimbali…..
“Sioni
ajabu kuzushiwa mambo ambayo sijayafanya kwani wanamuziki,
wanasiasa na hata viongozi mbalimbali wanakutana na mambo ya
kuzushiwa kwa kuwa wanajua wakifanya hivyo watawaangusha
kutokana na vyeo vyao lakini bado tupo bana,” alisema Komba huku akicheka.
Komba aliendelea kuzungumza kuwa mwaka 2015 utakuwa mwisho wake kuimba na anakusudia kuwarithisha vijana wapya….
Mheshimiwa Komba alihitimisha kwa
kusema kuwa katika maisha yake hafikirii suala la kufa kwani
kifo kipo tu hata ukifikiria na kukaa kuwaza jambo hilo ni
kujitafutia mkosi tu katika maisha yako.
0 comments:
Post a Comment