Sunday, 15 June 2014

MAKAHABA WAONGEZEKA BRAZIL,HUKU WACHEZAJI WA UIENGEREZA WAJIPAPATIKIWA

...

BIASHARA ya ukahaba imeanza kunoga Brazil kutokana na kufanyika kwa fainali za Kombe la Dunia ambazo zilianza jana usiku nchini humo ambapo wenyeji Brazil walifungua na Croatia.

Kwa Mujibu wa BBC, wanawake nchini Brazil wanaanza kujihusisha na biashara ya ukahaba huku wakiwalenga zaidi wachezaji wa England.

Wasichana wanaofanya kazi katika danguro la Vilka Mimosa iliyoko Rio wanatoa huduma kwa gharama ya chini, 'maalumu' kwa mashabiki wa Uingereza kwa sababu wamesafiri kutoka mbali.

Makahaba wanaofanya kazi katika danguro kubwa zaidi nchini Brazil watatoa huduma maalumu kwa mashabiki wa Uingereza, muda mfupi tu kabla ya kung'oa nanga kwa michezo hiyo mikubwa zaidi ya soka ulimwenguni.

Wakati michezo hiyo ikianza katika taifa ambalo kandanda inaenziwa mno, takriban wasichana 4,000 wa Vilka Mimosa iliyoko Rio wako tayari kuwapokea wageni wengi kutoka kwenye mataifa 32 yanayoshiriki Kombe la Dunia.

Wengi wanawaona mashabiki wa Uingereza kama njia ya kupata kipato zaidi, huku wengine wakianza kuifanya biashara hiyo kwa sababu tu ya mashindano hayo.

Wasichana hao watalipisha euro 16 ili kufanya mapenzi kwa muda wa nusu saa, huku wengi wakiamini wanaweza kutafuta hati za kusafiria ili kwenda kuishi na Waingereza.

Wengi wa makahaba walijifunza kiingereza, kabla ya michuano hiyo ili kuweza kuwasiliana.

Huku akiwa amevalia sketi ya rangi ya bluu, Mel mama mwenye watoto wawili alisema; "Natamani kukutana na mwanaume kutoka taifa la Uingereza, natamani kupanua mtazamo wangu. Nilikuwa kahaba kuanzia majuma matatu yaliyopita. Najua kutakuwa na desturi zingine nyingi wakati wa Kombe la Dunia.

"Natumai kupata fedha hizo ili kuisaidia familia yangu, kulipa kodi na bili. Tunawasubiri Waingereza, siwezi kuzungumza lugha yao, lakini tutawasiliana kwa njia ninayoijua."

Vila Mimosa iko karibu na machinjio na soko la nyama, na nyuma ya barabara hiyo kuu ni maskani yenye mitaa mingi ambapo wasichana hao hufanyia biashara yao. Baa zote 100 katika eneo hilo zina namba, huku Mel akifanya kazi katika baa namba 62 kuanzia saa 2 usiku hadi saa 2 asubuhi.

Katika barabara iliyoko nje ya baa hiyo, wafanyabiashara wanapika maharage pamoja na supu ya nyama huku wageni pia wakipata fursa ya kunywa 'Mocoto', kinywaji kinachotengenezwa kwa kuchemsha miguu ya ngĂ­ombe.

Huku mapato ya jumla kwa mwananchi wa kawaida yakiwa chini ya euro 200 kwa mwezi, makahaba hao huweza kupata hadi kufikia mara nne ya mapato hayo. Katikati mwa eneo hilo lenye madanguro, wanawake walio nusu uchi hucheza au kusimama kwa foleni ndefu, ili kuonekana na wageni wanaopita.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger