SIKU
chache baada ya tuhuma za ubakaji na mzozo wa familia ya mwimba Injili
mahiri nchini, Flora Mbasha na mumewe, Emanuel Mbasha, mambo mengine
yameibuka.
Yaliyoibuka
safari hii ni taarifa kwamba, juzikati, Flora alivamiwa na watu
wasiojulikana nyumbani kwake, Tabata Kimanga jijiini Dar dakika chache
baada ya yeye kuingia na gari akitokea mafichoni anakoishi kwa sasa.
Kwa
mujibu wa chanzo, siku ya tukio ilikuwa saa 9.15 alasiri ambapo Flora
aliingia nyumbani kwake na kufunguliwa geti kubwa kisha kuingiza gari
ndani na geti kufungwa tena.
“Flora aliingia na gari akitokea hotelini anakoishi kwa sasa. Alikuwa ameshaingia na geti likafungwa. Ghafla, watu wakafika na kugonga geti hilo kwa nguvu huku wakisema watalibomoa geti kama wenyeji hao hawatafungua,” kilisema chanzo.
Mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha akiwa na mumewe, Emanuel Mbasha,
“Flora aliingia na gari akitokea hotelini anakoishi kwa sasa. Alikuwa ameshaingia na geti likafungwa. Ghafla, watu wakafika na kugonga geti hilo kwa nguvu huku wakisema watalibomoa geti kama wenyeji hao hawatafungua,” kilisema chanzo.
Chanzo kikazidi kudai kwamba, ilibidi Flora apige simu polisi ili wafike kumuokoa yeye na familia yake.
“Polisi wawili walifika haraka sana wakiwa na bunduki na kukuta wale watu wamekimbia maana walimsikia Flora akiongea na polisi kuomba msaada.
“Polisi wawili walifika haraka sana wakiwa na bunduki na kukuta wale watu wamekimbia maana walimsikia Flora akiongea na polisi kuomba msaada.
“Lakini
polisi wenyewe ilibidi watumie nguvu kubwa kugonga geti na
kujitambulisha ndipo akatokea Flora na kuchungulia nje kupitia dirisha
dogo. Alipowaona polisi akafungua mlango,” kilisema chanzo hicho.
Akihojiwa na polisi hao, Flora alisema watu hao walikimbia na hakuwajua kwa sura wala hawakujitambulisha ni akina nani.
Akihojiwa na polisi hao, Flora alisema watu hao walikimbia na hakuwajua kwa sura wala hawakujitambulisha ni akina nani.
Alizungumza
na gazeti hili baada ya tukio, Flora alisema: “Unajua kwa sasa nina
hofu sana na nilihisi wale watu walikuwa wakinifuatilia kwa karibu kila
sehemu, sasa naogopa kuendelea kuishi hapa, wanaweza kurudi na sijui
lengo lao.”
Hata
hivyo, baada ya askari hao kuondoka katika eneo hilo, Flora naye
aliingia kwenye gari lake akiwa na mdogo wake na kuondoka.
Mume
wa Flora, Mbasha naye yupo mafichoni baada ya kudaiwa kumbaka binti wa
miaka 17 ndani ya nyumba yao huku utata ukitawala kuhusu ukweli wa tukio
hilo ambalo limeigawa jamii.
0 comments:
Post a Comment