Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatangaza nafazi za Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Cheti kwa Mwaka wa Masomo 2014/2015.
Kuzidownload bofya link hizo hapo chini, ya kwanza ngazi ya cheti (Certificate Grade A) na ya pili ni stashahada (Diploma).
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015 UTANGULIZI
Moja
ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa
walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa, wanafunzi wanaochaguliwa
kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti ni wale wenye ufaulu mzuri
katika mtihani ya kidato cha NNE. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la
Kwanza hadi la Tatu kwa ajili ya Cheti na wenye ufaulu wa alama 26 au
27 (mwaka 2004 hadi 2012) na alama 32 hadi 34 (mwaka 2013) watadahiliwa
katika programu ya mafunzo kabilishi ya mwaka mmoja.
Aidha,
kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya
Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili. Watakaojiunga na mafunzo ya
ualimu na kufaulu mafunzo yao watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana
na taratibu za Serikali.
VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/2015.
1: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’: MUDA MIAKA 2
- Cheti Ualimu wa kawaida katika vyuo vya Ilonga, Kabanga, Kitangali, Mandaka , Murutunguru , Ndala , na Tarime
- Cheti Ualimu Elimu ya Awali katika vyuo vya Kabanga, Kinampanda, Mhonda, Mtwara (U), Singachini, Tandala, Tarime
- Cheti Ualimu Elimu kwa michezo katika vyuo vya Ilonga, Tarime, Ndala na Mtwara (U)
Mwombaji awe:
Mhitimu
wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 mwenye ufaulu wa kiwango
kisichopungua Daraja la III katika Mtihani uliofanyika katika kikao
kimoja.
2: MAFUNZO KABILISHI NGAZI YA CHETI (BRIDGING COURSE) KWA AJILI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI:- MUDA MWAKA 1
Mafunzo
katika vyuo vya ualimu Bustani, Kinampanda, Mhonda, Mpuguso, Mtwara
(U), Nachingwea, Singachini, Tandala, Katoke na Sumbawanga
Mwombaji awe:
- Amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 hadi 2012 na awe amefaulu kwa kiwango kisichopungua Daraja la IV kwa alama 26 au 27 (kwa mtihani wa mwaka 2004 hadi 2012) na alama 32 hadi 34 (mtihani wa mwaka 2013) kwa mitihani iliyofanyika katika kikao kimoja; na
- Mwenye ufaulu wa angalau kiwango cha D katika masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili katika Mtihani wa Kidato cha IV.
3: ELIMU MAALUM: MIAKA 2 katika chuo cha ualimu Patandi:-
Mwombaji awe:
- Mwalimu wa Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
- Mwenye ufaulu angalau somo moja la Sayansi katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi:Walimu wanaofundisha Elimu Maalum hata kama hawana mafunzo maalumu ni sifa ya nyongeza (uthibitisho uambatishwe).
MAELEZO MUHIMU
- Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
- Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
- Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2013 waliojaza nafasi ya mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti Daraja ‘A’ kwenye ‘Selforms’ wakati wanamaliza Elimu ya Sekondari wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo;
- Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
- Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz);
- Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
- Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu.
VIAMBATISHO
Waombaji
wa mafunzo ya ualimu watume maombi yao kwa njia ya Barua ikionyesha
anuani kamili ya mwombaji pamoja na viambatisho vifuatavyo:
- Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV;
- Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti (kwa waombaji walioajiriwa); na
- Barua zilizopitishwa na waajiri (kwa waombaji walioajiriwa).
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 30 MEI 2014.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
UTANGULIZI
Moja
ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa
walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa, wanafunzi wanaochaguliwa
kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ni wale wenye ufaulu
mzuri katika mitihani ya kidato cha NNE na SITA. Ili kufanikisha azma
hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, itadahili wanafunzi wenye
ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi Daraja la Tatu tu.
Aidha,
kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa Sayansi na Hisabati wa
takribani walimu 26,000, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa
waombaji waliofaulu masomo ya Sayansi na Hisabati ili kuziba pengo hili.
Nia ya Serikali ni kuwavutia wanafunzi wengi wa masomo ya Sayansi na
Hisabati. Kuanzia mwaka huu wa masomo 2014/2015, wanafunzi watakaojiunga
na fani ya Ualimu kwa masomo ya Sayansi na Hisabati watagharimiwa na
Serikali kupitia mfumo wa ruzuku na mkopo. Wanafunzi watakaokuwa na
ufaulu wa Daraja la Kwanza watapatiwa Ruzuku na wale wenye Daraja la
Pili na la Tatu watapewa mkopo ili kuwasaidia katika masomo yao.
Watakaofaulu mafunzo ya ualimu katika masomo ya Sayansi na Hisabati
watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za serikali.
VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/2015.
1: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA: MASOMO YA SAYANSI, HISABATI NA UFUNDI: MUDA MIAKA 2
- Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpwapwa, Tukuyu, Songea, Butimba, Klerruu na MonduliMwombaji awe amehitimu: Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa ‘Principal Pass’ mbili katika Masomo ya Sayansi na Hisabati.
- Ualimu wa ufundi katika chuo cha ualimu Klerruu. Mwombaji awe amehitimu:
a.Mafunzo ya FTC kati ya mwaka 2004 na 2010 kutoka Vyuo vya Ufundi, Au
b.
Mafunzo ya ufundi katika ngazi ya NTA Level 6 au sifa linganishi
(equivalent qualification) kati ya mwaka 2007 na 2013 kutoka chuo
chochote cha Ufundi kinachotambulika na Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE).
(iii) Ualimu wa Kilimo katika chuo cha ualimu Monduli
Mwombaji awe amehitimu:
Kidato
cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu ‘Principal Pass’
mbili katika somo la ‘Agricultural Science’ na ‘Biology’, ‘Chemistry’ au
‘Food and Nutrition’.
2: MAFUNZO MAALUM YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA KWA KIDATO CHA NNE MASOMO YA SAYANSI/HISABATI NA ENGLISH: MUDA MIAKA 3
Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati na English katika vyuo vya Butimba, Morogoro, Korogwe, Songea na Mpwapwa
Mwombaji awe amehitimu:
Kidato
cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa Daraja la Kwanza
hadi la Tatu, na Credit mbili (yaani A, B+, B au C) katika masomo ya
Sayansi, Hisabati na English.
3: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA: MUDA MIAKA 2
- Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango cha ‘Principal Pass’ mbili katika Masomo ya Sayansi Jamii.
- Biashara katika vyuo vya Shinyanga na Kasulu. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Biashara.
- Sanaa za Ufundi, Sanaa za Maonyesho, Muziki na Michezo katika chuo cha Butimba. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja
Tanbihi: Masomo
ya ‘Economics’, Basic Applied Mathematics’, ‘General Studies’,
‘Divinity’ na ‘Islamic Knowledge’ hayatatumika kama kigezo cha kumchagua
au kumdahili mwombaji.
4: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI STASHAHADA ELIMU YA MSINGI: MUDA MIAKA 3
Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
Mwombaji awe:
Amehitimu
Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 wenye ufaulu wa Daraja la
Kwanza hadi Daraja la Tatu katika Mtihani uliofanyika katika kikao
kimoja.
Tanbihi:
Kipaumbele kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya ‘Mathematics’,
‘Biology’, ‘Physics’, ‘Chemistry’, ‘Agriculture’, ‘Food and Nutrition’,
‘English’ na Kiswahili na wahitimu wenye mahitaji maalumu.
5. MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA (SEKONDARI): MUDA MIAKA 2
- Ualimu wa masomo ya Sayansi katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpwapwa, Tukuyu, Songea, Butimba, Klerruu na Monduli.Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Sayansi na Hisabati; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
- Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa, Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu. Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Sayansi Jamii; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
- Ualimu wa masomo ya Biashara katika vyuo vya Shinyanga, Kasulu. Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass” moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Biashara; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
- Ualimu wa masomo ya Elimu Maalumu katika chuo cha Patandi. Mwombaji awe: Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi; Au Sayansi ya Jamii na uzoefu wa kazi ya ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili, Au Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
Tanbihi: Walimu
wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalum kama wasioona, viziwi, wenye
ulemavu wa akili, n.k. ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).
6: MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA ELIMU YA MSINGI: MUDA MIAKA 2:
Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
Mwombaji awe:
Mwalimu wa Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
MAELEZO MUHIMU
- Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
- Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
- Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
- Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz)
- Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
- Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu;
VIAMBATISHO
Waombaji
wa mafunzo ya ualimu watume maombi yao kwa njia ya Barua ikionyesha
anuani kamili ya mwombaji pamoja na viambatisho vifuatavyo:
- Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV, VI na Ufundi;
- Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada (kwa waombaji walioajiriwa); na
- Barua zilizopitishwa na waajiri (kwa waombaji walioajiriwa).
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 30 MEI 2014.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)
0 comments:
Post a Comment