Staa
katika tasnia ya filamu Alice Bagenzi "Rayuu" amefunguka na kusema
amechoka maisha ya kuishi kiupweke hivyo anatafuta mwanaume wa kumuoa
ili naye awe katika ndoa na aachane na maisha ya ukapera maana kwa sasa
yanamuelemea na kila aonapo watu walio olewa jinsi wanavyoishi na
wanaume zao basi na yeye anatamani sana maisha hayo.
Akifunguka Rayuu alisema "natafuta
mwanaume wa kuniweka ndani ambaye atakuwa mkweli atanipenda kwani
nimechoka maisha ya kisela nataka niwe mke halali wa mtu tena mwanaume
atakayekuja kwangu nitampenda sana"
Pia aliongezea kwa kusema "mimi ni binti mzuri tena bado mdogo hivyo maisha ya kurukaruka nimechoka"
0 comments:
Post a Comment