Thursday, 15 May 2014

NJEMBA LANUSURIKA KUFA KWA UBAKAJI WA KITOTO

...
NJEMBA aliyejulikana kwa jina la Mfaume Kassim amesurika kuuwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuwalawiti watoto watatu wa kiume na kumbaka binti mmoja (majina yao yanahifadhiwa) kwa nyakati tofauti. 

Binti aliyefanyiwa kitendo hicho kiovu cha ubakaji.
Tukio hilo lilitokea Chanika, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo wananchi hao walifikia hatua ya kumwangushia kipigo kwa madai kuwa, kila akikamatwa kwa vitendo hivyo, huachiwa baada ya muda mfupi na kuendelea kudunda mitaani.
Akizungumza kwa uchungu baba wa mmoja wa watoto waliofanyiwa kitendo hicho, Abdillah Mpacha (pichani), alisema tukio lilitokea Kigezi, Chanika ambapo mtoto wake alikuwa akitokea Madrasa.
Alisema, alipokuwa njiani kuelekea nyumbani alikutana na mbakaji huyo na kumlaghai kwa pipi na kashata kisha kumpeleka nyumbani kwake na kumfanyia kitendo hicho.

Hapa anafafanua zaidi: “Tulishangaa kuona mtoto hana furaha kama kawaida, huku akiwa na wasiwasi mwingi, baadaye akalalamikia maumivu ya tumbo.
“Tulipompeleka hospitalini, baada ya uchunguzi na vipimo alionekana kuwa ameharibiwa vibaya sehemu za siri, hapo ndipo akasema ukweli na kumtaja mbakaji akasema alificha kwa sababu alimwambia kama angesema angemchinja.”
Alisema, kutokana na kuharibiwa sehemu za siri ilibidi awekewe mpira kwa ajili ya kujisaidia haja kubwa.
Awali tukio hilo liliripotiwa kwenye Kituo cha Polisi Chanika na kufungiliwa jalada namba CHK/RB/718/2014 kabla ya kuhamishiwa Kituo cha Polisi Stakishari na kufunguliwa jalada namba STK/RB/3609/2014 KUBAKA.

Nyaraka zinaonyesha uhalifu uliofanywa na Mfaume Kassim.
Hata hivyo, wananchi wa eneo hilo wanasema kuwa, baada ya siku tatu, Mfaume alionekana  nyumbani kwake akiwa hana wasiwasi jambo lililowatia hasira na kuamua kumshushia kipondo.
Mjumbe wa Mtaa wa Kigezi, Mzee Shabani alisema Mfaume aliokolewa na polisi waliofika eneo hilo lakini wanakijiji wamefikia uamuzi wa  kumfukuza kabisa kijijini hapo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger