STAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa tangu aanze kujihusisha na masuala ya mapenzi hajawahi kulia.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper
Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper
ambaye ana muonekano wa ‘kigumu’, alisema siku zote anaamini katika
kupambana hivyo hawezi kumlilia mwanaume hata iweje.
“Sijawahi kulia pale nilipoachwa wala
kuachana na mwanaume, akili yangu yote inaamini katika kutafuta maisha
hivyo siwezi kujirahisisha nikamwaga machozi kwa ishu za mapenzi,”
alisema Wolper.
0 comments:
Post a Comment