Umati wa watu ukiwa unashangaa kitendo cha mwanadada (kushoto mwenye kitambaa cha zambarau kichwani) aliyemkwapulia 20,000 mwenzake.
MWANADADA mmoja ambaye jina lake
halikufahamika amejikuta akinusurika kupigwa na wananchi wenye hasira
kali baada ya kumuibia mama aliyekuwa na mtoto.
Ishu nzima imetokea maeneo ya jirani na
hospitali ya Amana, Ilala, jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya mama
mmoja aliyekuwa na mtoto kumkabidhi mwanadada (mwizi) mtoto na mkoba
wake, ndipo mdada huyo alipochomoa shilingi 20,000/= kwenye mkoba wa
mama huyo.
Aliporudi mama wa mtoto alimkabidhi
mtoto na mkoba wake kisha kuondoka kwa haraka na wasiwasi mwingi, kitu
kilichomshitua yule mama na kujisachi ndipo alipobaini kuibiwa na kuanza
kupiga kelele za mwizi.
Vijana walionyesha uwezo wao kwa
kumkimbiza na kumkamata ambapo alinyang’anywa pesa na zogo likaibuka
wakati wengine wakitaka kumpiga huku baadhi ya vijana wakionekana
kumkingia kifua kwa kuwa ni mwanamke.
0 comments:
Post a Comment