Friday, 16 May 2014

Huyu Ndio Kinara wa Uwizi wa Mabank Tanzania..Anatafutwa kwa Udi na Uvumba

...

Jeshi la Polisi Kanda Maalum D’Salaam limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa mhimu ambaye ni kinara wa mtandao wa wizi katika mabenki ambaye anajulikana kwa jina la RONALD S/O MOLLEL umri miaka 37, mfanyabishara na mkazi wa Kimara Bonyokwa Jijini D’salaam.
         
           Mtuhumiwa huyu amekimbilia mafichoni mara baada ya tukio la ujambazi katika Tawi la Benki ya Barclays  Kinondoni lililotokea tarehe 

15/4/2014 ambapo majambazi walifanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha T.Shs.390,220,000/= , USD 55,000/= na EURO 2150/=.  Aidha sasa imefahamika kwamba mtuhumiwa huyu ni mume wa mtuhumiwa wa kwanza katika tukio la 
Barclays Benki aitwaye ALUNE D/O KASILILIKA @ ALUNE D/O MOLLEL , 

miaka 28,  Mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa Benki Tawi la Barclays Kinondoni.  Mtuhumiwa Mollel anatafutwa kwa kila hali kwa vile yeye ndiye alikuwa kinara wa kupanga tukio hilo la Barclays na mara baada ya tukio ametoroka na kiasi kikubwa cha fedha hizo zilizoibiwa.

Zipo taarifa za kuaminika kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akipanga na kushiriki kikamilifu katika matukio mbali mbali ya uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuongoza vikundi vya majambazi vilivyowahi kupora katika mabenki mbali mbali katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.  Mtuhumiwa huyo ni hatari kwani ana mtandao na watumishi muhimu katika matawi mbali mbali ya mabenki kwa lengo la kufanikisha uhalifu katika mabenki hayo.
Jeshi la Polisi limelazimika kutoa picha yake hadharani kwa kutumia dhana ya ulinzi shirikishi ili mtuhumiwa huyu akionekana akamatwe na taarifa zitolewe katika kituo chochote cha Polisi ikiwa ni lengo la polisi kupambana na uhalifu katika dhamira ya kuzuia uhalifu, kulinda maisha na mali za wananchi.  

    Zawadi nono ya fedha taslim itatolewa kwa siri kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu.  Pamoja na maelezo hayo mtuhumiwa mwenyewe sasa anapewa fulsa ya kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kabla ya kukamatwa kwa njia nyingine
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger