Mojawapo
ya eneo linalolalamikiwa na wanafunzi wa vyuo na taasisi za elimu ya
juu kuhusu Bodi ya Mikopo ( HESLB), ni eneo la madaraja wanayopangiwa na
bodi hiyo kwa ajili ya kupata mkopo wa masomo ya kozi wanazochukua.
Kuna
malalamiko kwamba, bodi ya mikopo imekuwa ikipanga madaraja kwa
upendeleo kwa kuwa ile dhana ya kumkopesha mwanafunzi anayetoka katika
familia maskini kwa kiwango cha asilimia 100,haionekani kufanya kazi kwa
wanafunzi walio wengi.
Kwa
muda mrefu kumekuwa na malalamiko kwamba,katika upangaji wa madaraja
unaofanywa na bodi,wanafunzi wanaotoka katika familia zenye uwezo mkubwa
au wa kati, ndio wamekuwa wakipata asilimia 100 na wale wanaotoka
katika familia maskini wakiishia kuambulia asilimia 60 mpaka 40.
April mwaka huu, bodi ya mikopo nchini ilianzisha utaratibu mpya wa
kuomba mikopo kwa wanafunzi wapya na wale wanaoendelea kwa njia ya
mtandao.
Mfumo
huu unatarajiwa kuchukua nafasi ya ule wa zamani, ambapo mhusika
alikuwa anatakiwa kujaza fomu kisha kuziwasilisha HESLB.
Fomu
hizo zilijazwa taarifa mbalimbali za muombaji zilizokuwa zinahitajika
na bodi ili ziisaidie kumpangia muombaji daraja la fedha alizostahili
kupewa kama mkopo kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali anazopaswa
atika chuo au taasisi aliyokuwa anachukua kozi yake.
Wanafunzi wote wakidato cha sita mnatakiwa kuomba mkopo kwa kutumia utaratibu wa kulipia MPESA kabla ya kwenda jeshi kuepuka usumbufu.
KWA MAELEZO ZAIDI TEMBELEA :www.heslb.go.tz au olas.heslb.go.tz
0 comments:
Post a Comment