MSANII Vanitha
Omary aliyeolewa hivi karibuni, amesema vifo vya mfululizo vya wasanii
wenzake vimemlazimu kuondoka katika fungate ili ashirikiane na wenzake
katika shughuli za misiba.
Vanitha
aliyefunga ndoa siku moja kabla ya kifo cha msanii Recho Haule, alisema
marehemu huyo alikuwa ni mtu wake wa karibu hivyo akalazimika kufuta
mapumziko hayo ya baada ya ndoa.
“Tangu
niolewe balaa juu ya balaa, hata sijafaidi ndoa yangu katika fungate,
maana ilipita siku moja tu nikapata msiba wa Recho, tukamaliza ili
tupumue, ukaja wa George Tyson ambaye naye alikuwa ananihusu sana,
nikalazimika kuonyesha ushirikiano,” alisema.
0 comments:
Post a Comment