Tuesday, 10 June 2014

SUA:UCHAGUZI MKUU CHUO KIKUU CHA SOKOINE(SUA) MOROGORO,VIJANA WAJITOKEZA KWA WINGI KUCHUKUA FOMU.

...
                                      
Zikiwa zimebakia siku 9 kuelekea uchaguzi wa serikali ya wanafunzi sua,baadhi ya vijana wameonekana wakichukua fomu za uongozi wa nafasi mabalimbali;zikiwemo nafasi za ubunge na urais wa chuo.

Uchaguzi huo utahusisha kampasi mbili MAZIMBU na  MAIN CAMPUS.


Hata hivyo uchaguzi huo utakuwa wa aina yake kutokana na kuhusisha vijana wakakamavu na waliokomaa kisiasa,tukiongea na mmoja wa wagombea na machachari waliotangaza nia ya kugombea ubunge NEW HOSTEL BLOCK B amesema kuwa hadi sasa anauhakika kuwa atashinda 99% na kutangazwa mbunge wa hostel hiyo.
Baadhi ya vijana walitangaza nia ni pamoja SHABAN SHABAN(AGRI GENERAL), JEREMIAH(INJINIA),VALENCE(FOODIST) .

Wakati huohuo Mwandishi wa MASWAYETU BLOG alishuhudia watu wakiwa kwenye pirika mbalimbali za group discussion,assignment na kujiandaa kwa test mbalimbalimbali zinazoendelea chuoni hapo.

Hata hivyo nilibahatika kukutana mojakwa moja na mgombea Urais ambae ansoma mwaka wa pili na alikuwa waziri katika serikali iliyopita amesema kuwa hana shida wala wasiwasi na ana uhakika kuwa lazima aibuke mshindi wa uchaguzi huo,ikizingatiwa kuwa hoja anazo na uwezo wa kuwatumikia wanafunzi hao watakaomchagua.


Uchaguzi huo unatarajiwa kuendeshwa siku ya tar.20 mwezi huu ambayo itakuwa ndio  siku rasmi ya study break wakijiandaa na UNIVERSITY EXAMINATION(U.E) wakati huo huo baadhi ya wanafunzi watakaokuwa wameteuliwa kwa ajili ya mkutano mkubwa september ujulikanao kama "SEPTEMBER CONFERENCE" UTAKAYOFANYIKA katika campus ya MAZIMBU FREEDOM SQUARE kwa mda wa  wiki mbili.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger