Asili
Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, Jimbo la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Lugha ya mama ilikuwa Kikwere.Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga. Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, Babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.
Masomo
1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Middle School Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga. Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza digrii yake mwaka 1978. Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.
Kupanda ngazi katika siasa
1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mw. 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha.1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa uraisi upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwl. Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia Benjamin Mkapa nafasi aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri ya Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.
Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya raisi na akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.
0 comments:
Post a Comment