Naibu katibu mkuu wa CCM bara Mwigulu Nchemba akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini.
Wananchi wa jimbo la Iringa mjini wakimsikiliza Nchemba katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa.
Na Francis Godwin Blog
NAIBU katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Bara Mwigulu Nchemba awahakikishia wananchi wa jimbo la Iringa mjini kuwa muda wa mbunge wa jimbo hilo kuongoza umefika kikomo na kuwa ataongoza mapambano ya kumng’oa mwakani katika uchaguzi mkuu.
NAIBU katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Bara Mwigulu Nchemba awahakikishia wananchi wa jimbo la Iringa mjini kuwa muda wa mbunge wa jimbo hilo kuongoza umefika kikomo na kuwa ataongoza mapambano ya kumng’oa mwakani katika uchaguzi mkuu.
Akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini leo katika uwanja wa
Mwembetogwa Nchemba ambae ni naibu waziri wa fedha alisema kuwa mbali
ya mbunge huyo kupewa nafasi hiyo ya bure mwaka 2010 ila bado
ameshindwa kuwa na huruma na wananchi wa jimbo hilo na kuendelea
kujinufaisha yeye badala ya kuwekeza kwa wananchi hasa vijana na ndio
sababu ya kushindwa kufanya vikao na wanachama wake na kuendelea
kuitisha maandamano badala ya kufanya kazi.
“Tutajipanga vema kila kona ya jimbo la Iringa mjini ili kulirudisha
jimbo mikononi mwa CCM kwa kumpata mbunge ambae atawatumikia wananchi
na sio wa kujitumikia yeye na kuwa mbunge wa maandamano kwa kipindi
chake chote”
Nchemba
alisema kuwa kutokana na kazi kubwa iliyopfanywa na vijana wa jimbo
la Iringa kwa kumpigania mbunge Msigwa alipaswa kuwa na roho ya huruma
kwa vijana hao ikiwa ni pamoja na kuwageuza daraja na kuwafanyisha
maandamano yasiyo kwisha badala ya kuwaanzishia miradi ya kiuchumi.
“Hivi
tazameni leo maeneo yote ya makanda wa Chadema majimboni mwao ni
maandamano kila siku kila wakati utasikia hakuna kulala makamanda huku
mbunge anashindwa kuwasaidia …..na siku hizi wanakuja na hoja ya
makamanda pambaneni tutachukua nchi huku hata kata kwao ni ndoto sasa
niwaambie leo hata nusu ya nchi hii kamwe hawatapata”
Asema
mmoja kati ya mke wa kiongozi mojawapo wa Chadema alimuuliza hivi kwa
nini mume wake anapenda sana maandamano alimjibu kuwa mume wake huyo
akichukia huwa anafanya maandamano ndani ya chumba cha kulala.
Nchemba
pia ameponmgeza utendaji kazi wa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa
Ritta Kabati na kuwa siku zote amekuwa akiwapigania wananchi wa
jimbo la Iringa mjini bungeni tofauti na mbunge wa jimbo mchungaji
Msigwa ambae amekuwa akiongoza kwa kufanya maandamano.
Katika
hatua nyingine Nchemba alisema amesema kuwa muda wa matajiri
kuendelea kujinufaisha na misamaha ya kodi umekwisha na kuwa
anajipanga kupeleka sheria bungeni itakayowabana wafanyabiashara
wakubwa kulipa kodi kama wanavyolipa wafanyabiashara wadogo.
Alisema
kuwa watu wanapata misamaha hadi inakatisha tamaa kwani ni pesa
nyingi za kimaendeleo zinapotea kutokana na utitiri wa misamaha
inayoendelea kutolewa .
“Napeleka sheria katika bunge hili la bajeti itakayofuta misamaha ya
kodi kwa viwanda na wafanyabiashara wakubwa…inakuweje wananchi
masikiti hata wanapotaka kuanzisha saluni wanalipizwa kodi ila
wafanyabiashara wakubwa na baadhi ya watu pia nitapeleka sheria ya
kubana matumizi ya fedha za umma”
Alisema
kuwa inashangaza kuona mashirika ya umma yanavuna na kutumia huku
wanyonge wakiendelea kuteseka na walimu na askari wakiendelea kukosa
kulipwa madai yao.
“hatuwezi kusema leo walimu ama askari ni wengi wakati watu
wanakwepa kulipa kodi huku wanafunzi wakikosa mikopo ya elimu ya juu
eti kutokana na kukosa fedha wakati watu wengine wanakwepa kodi….hili
ni jambo la aibu sana najua wapo wabunge watakaopinga ila wananchi
mtaona ni nani ni mbunge wa wananchi …kwani najua wapo wabunge ambao
hawalipendi hili watapinga ila lazima nilifikishe hata kama chungu ila
lazima suala hili likomeshwe”
0 comments:
Post a Comment