Akiwa mjini Iringa kwenye viwanja vya
Mwembetogwa, Mh Mwigulu Nchemba ......alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara,
alisema kuwa Watanzania wana uhuru mkubwa sana wa kuongea mpaka
wanakosa adabu hata kwa wazee wao "..najua mnaona natumia lugha kali,
lakini ndio kawaida yangu kusema ukweli, ...natamani niwe Rais wa nchi
hii ili niwafundishe adabu Watanzania, ndio!" Labda inawezekana
alimaanisha kuwafundisha adabu Watanzania fulani,
lakini kwakuwa alikuwa akiongea kwa jazba aliteleza ulimi, au
alimaanisha hivyo. Watu waliohudhuria mkutano huo walipigwa na butwaa,
aliliona hilo na kubadilisha mada haraka. Aliwafurahisha watu pale
aliposema"..kule kwetu Singida, ng'ombe mpole ndie anaekamuliws sana
maziwa, lakini yule mkorofi anaachwa, kadhalika (serikali) inawatoza
kodi wajasiriamali wadogo bila msamaha lakini wawekezaji wakubwa
wanasamehewa mabilioni ya fedha!) suala hilo ameahidi kupambana nalo.
0 comments:
Post a Comment