Wabunge
wanawake wenye muda mrefu bungeni pamoja na mke wa waziri mkuu, Mama
Tunu Pinda juzi walimuandalia sherehe ya kumfariji mbunge wa viti maalum
(CCM), Vicky Kamata baada ya harusi aliyotarajia kufunga wiki
iliyopita, kukwama.
Sherehe hiyo ya faraja, ilifanyika Hoteli ya Dodoma kati ya saa 1.00 jioni na saa 6.45 usiku juzi mjini hapa.
“Unajua
hata yeye mwenyewe tulim-surprise (tulimshtukiza). Alijua kuwa ni
chakula cha jioni, lakini alipofika alikutana na muziki, kwaya na
wabunge wengine waliompokea kwa vifijo na nderemo,” alisema mmoja wa
wabunge waliohudhuria hafla hiyo. Sherehe hizo zilitumbuizwa na kwaya ya
kikiristo ya Mvuke ya kanisa la Anglican mjini Dodoma.
Alisema
Vicky alijua kuwa amealikwa na mbunge wa viti maalum (CCM), Magreth
Sitta kwa ajili ya chakula cha jioni lakini alipofika aka kutana na
sherehe.
“Tuliona
ni vyema kumuandalia sherehe kidogo ili kumpa moyo kwamba hayo
yametokea kwa sababu Mungu alitaka kumuepushia na mambo makubwa siku za
usoni,” alidokeza mmoja wa waliohudhuria sherehe hiyo.
Baadhi
ya wabunge waliohudhuria ni wabunge wa viti maalum kutoka CCM ambao ni
Magreth Sitta, Anna Abdallah, Felister Bura, Hilda Ngoye, Agness
Hokororo na Anastazia Wambura.
Wengine
waliohudhuria ni Asumpta Mshama (Nkenge-CCM), Anne Kilango (Same
Mashariki-CCM) na Waride Bakari Jadu (Kiembe Samaki-CCM). Chanzo hicho
kilisema wabunge Anne Kilango, Magreth Sitta na Anna abdallah,
walielezea jinsi baadhi ya wanawake viongozi walivyokumbwa na mikasa
kama ya Vicky na wengine hata kuacha wakiwa makanisani.
“Wengine
walieleza jinsi walivyoteswa na wenza wao na kwamba amshukuru Mungu
pengine amemuepushia mambo makubwa ambayo yangeweza kutokea kama ndoa
ingefungwa,”alisema shuhuda huyo.
Alisema
sherehe hiyo ilikuwa kama ibada maana muda mwingi ulitumika katika
kumuhubiria Vicky na kumsihi asikatishwe tamaa na badala yake asonge
mbele.
Alipoulizwa kuhusu sherehe hiyo, Vicky alikiri kufanyika lakini akakataa kuielezea kwa kina.
“Mimi
niliitwa kwenye chakula cha jioni lakini nilipofika pale nistaajabu
kukutana na sherehe,”alisema Vicky ambaye alikataa kuelezea kwa kina
kuhusu sherehe hizo.
0 comments:
Post a Comment