Tuesday, 10 June 2014

UTARATIBU WA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA'JKT'

...

TANGAZO

JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINAUTANGAZIA UMMA KUEPUKANA NA MATAPELI WANAOCHUKUA FEDHA KWA LENGO LA KUWAPATIA VIJANA NAFASI ZA KUJIUNGA NA JKT. NAFASI ZA KUJIUNGA NA JKT HAZIUZWI POPOTE.

JESHI LINAOMBA UMMA UTAMBUE KUWA LINAENDESHA MAFUNZO YA AINA MBILI. AINA YA KWANZA NI YA KUJITOLEA NA AINA YA PILI NI YA MUJIBU WA SHERIA.
NAFASI ZA VIJANA WA KUJITOLEA ZINATOLEWA NA MKUU WA JKT KUPITIA WAKUU WA MIKOA TANZANIA BARA NA VISIWANI. AIDHA WAKUU WA MIKOA HUZIGAWA NAFASI KWA WAKUU WA WILAYA, NAO WAKUU WA WILAYA HUGAWA KATIKA TARAFA, KATA NA VIJIJI VYAO.
AINA YA PILI NI YA MUJIBU WA SHERIA KWA VIJANA WANAOHITIMU KIDATO CHA SITA KATIKA MWAKA HUSIKA NA MAJINA YAO YANATOLEWA NA WIZARA YA ELIMU NA UTAMADUNI KUPITIA BARAZA LA MITIHANI TANZANIA.
JAMII INATAHADHARISHWA KUACHA KUTOA FEDHA KWA MATAPELI KWA NIA YA KUPATA NAFASI ZA KUJIUNGA NA JKT. KUTOA AU KUPOKEA RUSHWA NI KINYUME CHA SHERIA. HIVYO MTOAJI NA MPOKEAJI WAKIGUNDULIKA WATASHUGHULIKIWA KISHERIA.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA  NA MKUU WA JKT
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger