Tuesday, 10 June 2014

MBUNGE MCHUNGAJI MSIGWA:' KWA NILIYOYAFANYA SIHITAJI KAMPENI\

...

IRINGA ni miongoni mwa mikoa ambayo siku za nyuma ilikuwa ni tegemeo la chakula kwa taifa letu, ikiwa ni mojawapo ya iliyounda kitu kilichoitwa Big Four, kwa uzalishaji wa chakula, mingine ikiwa ni Mbeya, Ruvuma na Rukwa.
Lakini katika miaka ya hivi karibuni, uzalishaji huo umekuwa ukishuka, jambo linalosababishwa pamoja na mambo mengine, mabadiliko ya hali ya hewa na usimamizi mbaya wa viongozi wa vijiji katika kuhimiza ukulima wa kisasa, matumizi ya mbolea na kadhalika.

Mji wa Iringa nao, kama ilivyo miji mingi nchini, wananchi wanadai umekuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi zinazotokana na miundombinu mibaya, msongamano wa watu, huduma duni za afya, kushuka kwa elimu na kuzagaa kwa Wamachinga.
Kwa sasa Jimbo la Iringa mjini lipo chini ya Mbunge Mchungaji Peter Msigwa kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye alipata ushindi wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 kwa kumshinda mpinzani wake mkuu, Monica Mbega wa CCM.
Shughuli kubwa za wakazi wa mji wa Iringa katika kukuza uchumi ni biashara za daraja la kati na zile ndogondogo (Wamachinga). Katika makala haya, Mbunge Msigwa anazungumzia jinsi anavyokabiliana na changamoto mbalimbali jimboni kwake, ikiwa ni pamoja na maoni yake kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Elimu
Katika sekta ya elimu, Msigwa anasema hali ya ufaulu imepanda na kulifanya jimbo lake kuongoza miongoni mwa majimbo yote mkoani Iringa, kwani zaidi ya asilimia 90 ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wanafaulu kwenda sekondari na wanaomaliza kidato cha nne na kuendelea cha tano, ni zaidi ya asilimia 85.
“Niwatoe hofu wapiga kura wangu kuwa kwa kipindi chote ambacho nitakuwa madarakani, kiwango cha ufaulu kitaendelea kupanda na kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule, atapata haki yake ya msingi ambayo ni elimu kwa ajili ya manufaa yake na taifa kwa jumla,” alisema na kuongeza;
“Kazi ya mbunge ni kusimamia maendeleo, wapo baadhi ya watu hawajui tafsiri hii, jimbo hili sikulikuta hivi, lakini kwa kipindi chote ambacho nimekuwa hapa, nimewajibika kikamilifu na kazi hiyo itafanyika kwa muda wote nitakaokuwa imamia maendeleo hivi sasa barabara nyingi za jimbo lake zinapitika na ujenmwakilishi wa Iringa mjini bungeni.”
Barabara
Kuhusu barabara, Msigwa anasema wakati alipoingia madarakani hali haikuwa nzuri, lakini kwa muda ambao amesimamia maendeleo hivi sasa barabara nyingi za jimbo lake zinapitika na ujenzi wa nyumba za kuishi na ofisi nazo zimekuwa zikiongezeka.
Alisema maendeleo ya kweli yatapatikana endapo barabara zitakuwa nzuri, kitu ambacho anakipigania kwa nguvu kubwa ili aweze kufikia malengo yake.
Maji
Wakati baadhi ya majimbo yaliyo mijini yakihangaika na ukosefu wa maji salama kwa wananchi wake, mjini Iringa hali ni tofauti. Maji safi na salama yanapatikana katika maeneo yote, hali anayosema imetokana na msukumo wake kwa idara na taasisi mbalimbali zinazohusika na bidhaa hiyo muhimu kwa maisha ya binadamu.
Kutokana na upatikanaji huo wa maji kwa asilimia mia moja, ikiwemo pia katika shule zote za sekondari jimboni, hofu ya magonjwa ya mlipuko imetoweka.
“Kunapokuwa na ukosefu wa maji, madhara makubwa yanaweza kutokea kwa sababu ni vigumu sana kuhimili afya ya mtu pasipo uwepo wa maji. Baadhi ya miradi ya maji ilitokana na misaada kutoka Benki ya Dunia.”
Afya
Kuhusu afya, mbunge huyo alisema wakati alipochukua nafasi hiyo, hali ilikuwa ni tofauti na sasa kwani imeboreshwa, hasa katika hospitali kuu ya mkoa ambapo yeye binafsi hufanya ziara za mara kwa mara ili kubaini matatizo. Aliisifu serikali ya mkoa na hospitali hiyo kwa kumpa ushirikiano wa kutosha, kitu kinachochochea kuwepo kwa huduma bora kwa wapiga kura wake.
Mchungaji Msigwa alisema huduma bora za afya zinazopatikana jimboni kwake zinachangiwa pia na hali ya usafi iliyopo, kwani mji huo ni miongoni mwa miji safi ambayo ni michache nchini kwani ukitembea katika mitaa mbalimbali ya mji huo, hali ya usafi ni ya hali ya juu. Takataka hazitupwi hovyo na kila baada ya umbali fulani, kuna pipa la kuhifadhia uchafu.
Ulinzi na Usalama
Akizungumzia kuhusu ulinzi na usalama, Mbunge Msigwa alisema hapo awali, hali ya uhalifu ilikuwa ni ya kiwango kikubwa, lakini tokea alipoingia madarakani, kwa kushirikiana na wadau wengine, kamati mbalimbali ziliundwa ili kudhibiti matendo ya kihalifu, jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya, mbunge huyo alisema mwenendo wa sasa wa Bunge la Katiba hautoi matumaini ya upatikanaji wa katiba mpya ya nchi, kwani tayari kuna mizengwe mingi inayoweza kusababisha lengo kutotimia.
Alishauri kusitishwa kwa mchakato huo hadi hapo baadaye.
Juu ya mtazamo wake kuelekea uchaguzi mkuu ujao, alisema hana hofu ya kurejea mjengoni kwani kazi nyingi alizosimamia zinampa jeuri ya kusema kuwa hahitaji hata kufanya kampeni mwakani, kwani alichokifanya kinajionyesha na wananchi wanakiona.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger