1. Kubadili mtindo wa kujikwatua.
Mwanamke anaweza kuwa amezoea kujikwatua
kwa namna fulani lakini baada ya muda akaamua kubadili muonekanao wake
kwa kubadilisha aina mpya ya kujikwatua kwa kuongeza vikorombwezo fulani
fulani akitegemea mwenzi wake ata notes lakini asijue kwamba wanaume
kwenye jambo hilo wala haliwagusi kabisa mpaka wafanye kushtuliwa.
Kwa hiyo nawashauri tu msije mkaumia bure pale mnapoona wenzi wenu hawa notice mabadiliko mliyoyafanya ndivyo tulivyo....
2. Kubadili mtindo wa nywele.
Kwa kawaida wanawake hutumia muda wao
mwingi kutengeneza nywele zao ili kujipa mwonekano mpya na pia
wakitarajia kwamba wenzi wao watapenda, lakini cha kushangaza wenzi wao
wala haiwagusi na wala hawa notice mabadiliko hayo ya nywele mpaka
wafanye kushtuliwa na wenzi wao. jambo hilo huwa linawakwaza sana
wanawake, lakini labda tu niwape ushauri wa bure, msiweke matarajio
makubwa ya kudhani kwamba mabadiliko ya nywele mnayoyafanya yatawavutia
wenzi wenu, si kweli utafadhaika bure bora tu mfanye kwa utashi wenu
3. Kubadili rangi za kucha
Wanaume wengi hawajui tofauti ya rangi,
kwa hiyo hata mwanamke abadili rangi yake ya kucha kwa ajili ya ku match
na mavazi fulani aliyonunuliwa na mwenzi wake au hata aliyonunua
mwenyewe anaweza kushangaa mwenzi wake asishtukie jambo hilo. Ajabu eh!
4. Mkoba mpya.
Unaweza kukuta mwanamke kajinasibu na
kununua mkoba mpya wa gharama baada ya kujinyima sana akitegemea mwenzi
wake atauona na kumsifia lakini atashangaa mwenzi wake wala haulizi
anaona tu kama ni mkoba wa kawaida. Lakini pia hata kama mkoba wenyewe
ume match na mavazi bado ni ngumu kwa mwanaume ku notice na ndiyo maana
inawauma sana wanawake wengi. Mtuhurumie tu, ndivyo tulivyo....
5. Kiatu kipya
Viatu navyo ni eneo lingine ambalo
wanaume hawa notice kabisa, mwanamke anaweza kununua kiatu kipya
akitarajia mwenzi wake atakiona na kumsifia lakini wala, labda tu kama
mwanaume huyo anapenda aina hiyo ya kiatu na aliwahi kukisifia baada ya
kumuona mwanamke mwingine amekivaa na kikampendeza, lakini kama si
mpenzi wa viatu wala mwanamke asitarajie kusifiwa, ni mpaka pale
atakapomshtua mwenzi wake kwa kumuuliza kama kiatu alichovaa
kimempendeza au la na sije akashangaa akijibiwa kwa kifupi tu, "ndiyo"
bila comments.
Kwa kawaida wanawake wanapenda ukiwasifia kuhusu jambo fulani utoe na comments japo kidogo tena kwa undani kabisa....
6. Lebasi za ulimbwende na makochokocho mengine
Hereni, bangili na kishaufu au kipini
cha puani kinaweza kumpa mwanamke muonekano mpya, lakini muonekano huo
hauwezi kumshangaza mwanaume kama mwanamke anavyotarajia, jambo hilo
huwa linawakera sana wanawake lakini ukweli ndiyo huo wanaume
hawasumbuliwi na vitu vidogo vidogo.
7. Pambo jipya chumbani au kitandani
Mwanamke anaweza kubadili mwonekano wa
nyumba au wa chumba cha kulala akidhani kwamba jambo hilo litamvutia
mwenzi wake. si kweli wanaume hawako hivyo anaweza akafika nyumbani na
kuona kama vile hakuna kilichofanyika mpaka afanye kushtuliwa na mwenzi
wake kwa kuulizwa kama ameionaje nyumba au chumba chao cha kulala.
haishangazi mwanaume akiuliza kwani kuna nini....!
Kwa mwanamke jibu hili anaweza hata
kutamani kumtwanga mwanaume na flower verse kwa hasira, lakini mianaume
ndivyo tulivyo, mtuhurumie tu.
0 comments:
Post a Comment