WACHEZAJI Neymar na Oscar wamepeleka vilio Croatia baada ya kuipa
ushindi wa mabao matatu timu yao ya Brazil kwenye mechi ya ufunguzi wa
Fainali za Kombe la Dunia 2014 zinazofanyika nchini Brazil.
Croatia walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 11 ambalo ni la kujifunga likiwekwa kimiani na beki Marcelo wa Brazil.
Baadaye wenyeji Brazil walikuja juu na kusawazisha bao hilo kupitia kwa
mchezaji wao mahiri anayefananishwa na Pele, Neymar kwa shuti la mbali
lililomuacha mlinda mlango wa Croatia, Stipe Pletikosa katika dakika ya
29 ya kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Neymar aliipatia Brazil bao la pili kwa mkwaju wa
penalti ambao kipa Pletikosa alijaribu kuupangua lakini ukajaa wavuni na
kuwapa wenyeji ushindi wa 2-1 dakika ya 71.
Mchezaji wa Chelsea, Oscar alihitimisha furaha ya waandaaji fainali hizo kwa bao lake la tatu dakika ya 90 ya mchezo.
Mpaka mwisho, Brazil 3, Croatia 1.
Leo michuano hiyo itaendelea ambapo Cameroon watavaana na Mexico, Uholanziwakikwaana na Hispania huku Chile wakipepetana na Australia.
VIKOSI NA ALAMA ZAO
Brazil: Julio Cesar 6; Dani Alves 5.5, Thiago Silva 6, Luiz 6, Marcelo 5.5, Paulinho 6 (Hernanes 63, 6), Gustavo 7, Hulk 6 (Bernard 68, 6), Oscar 7, Neymar 8 (Ramires 88), Fred 6.5.
VIKOSI NA ALAMA ZAO
Brazil: Julio Cesar 6; Dani Alves 5.5, Thiago Silva 6, Luiz 6, Marcelo 5.5, Paulinho 6 (Hernanes 63, 6), Gustavo 7, Hulk 6 (Bernard 68, 6), Oscar 7, Neymar 8 (Ramires 88), Fred 6.5.
Benchi: Jefferson, Fernandinho, Dante, Maxwell, Henrique, Willian, Jo, Maicon, Victor.
Mabao: Neymar 29,71 penalti, Oscar 90.
Kadi za njano: Neymar, Gustavo
Croatia: Pletikosa
6, Srna 6.5, Corluka 7, Lovren 6.5, Vrsaljko 6; Modric 7, Rakitic 7,
Perisic 6.5, Kovacic 6 (Brozovic 62, 5), Olic 6, Jelavic 6.
Benchi: Zelenika, Pranjic, Vukojevic, Schildenfeld, Rebic, Sammir, Vida, Eduardo, Subasic.
Mabao: Marcelo 11 (kujifunga)
Kadi za njano: Corluka, Lovren.
Mchezaji Bora wa mechi: Neymar.
Refa: Yuichi Nishimura (Japan) 5.
Mashabiki: 61,000
0 comments:
Post a Comment