Tuesday, 17 June 2014

NIGERIA NA IRAN SARE TASA,UJERUMANI 4 URENO 0,USA YAIBANIA GHANA 2-1

...


Nigeria yaridhika na sare tasa dhidi ya Iran
Timu ya Iran na Nigeria zilitoka sare ya suluhu bin suluhu , katika mechi yao ya kundi F huko Curitiba, kwenye fainali ya kombe la dunia siku ya Jumatatu.
Timu hiyo ya Carlos Queiroz ilionekana kuwa ngumu kushindwa tangu mwanzoni.

Super Eagles ya Nigeria,ambao walikua na rekodi nzuri katika michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia walishindwa kupenya safu ya ulinzi ya Iran.
Hii ilikua sare ya kwanza tasa katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2014.
Timu zote mbili zilijaribu kupata nafasi ya kufunga bao lakini hakuna iliyofaulu.
Iran ilipoteza nafasi ya kufunga bao pale ambapo kipa wa Nigeria, Vincent Enyeama alipouzuia mkwaju wake Reza Ghoochannejad.
Mabingwa hao wa bara Afrika mwaka 2013, walitarajiwa kushinda mchuano huo lakini timu ya Iran iliwapatia changamoto si haba.
Matokeo haya yanaipa timu ya Argentina uongozi wa kundi hilo baada ya kuishinda timu ya Bosnia-Herzegovina, 2-1, siku ya Jumapili.
Timu ya Iran itakutana na Argentina siku ya Jumamosi, huko Belo Horizonte, nayo Nigeria kuiandaa kukabiliana dhidi ya Bosnia kule Cuiaba.
Nigeria ilimiliki mchuano huo katika muda wote wa dakika 90, lakini hawakufaulu kuwashinda wa Irani.
Mkwaju wake Ghoochannejad na ule wa Ahmed Musa ndizo zilizokua nafasi nzuri za kufunga bao katika kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili, Shola Ameobi alizuiwa mara mbili na mlinzi wa Iran, Mehrdad Poolani.
Nigeria yaridhika na sare tasa dhidi ya Iran
Victor Moses ndiye aliyepata nafasi ya kwanza ya Nigeria kupata uongozi lakini mkwaju wake hafifu ulikamatwa na kipa wa Iran Reza Haghighi.
Kipa wa Iran Haghighi, asiye na uzoefu mkubwa katika mechi za kimataifa alionekana kutishika kila wakati washambulizi wa Super Eagles waliposhambulia lango lake na aliponea katika dakika ya saba kutokana na mkwaju wa kona.
Kenneth Omeruo alitia mpira wavuni lakini refa tayari alikua ameshapuliza kipenga kuonyesha kuwa kipa, Haghighi alikua amechezewa visivyo na John Obi Mikel.
Emmanuel Emenike alijaribu katika upande wa kushoto, lakini Pejman Montazeri alikua kizuizi katika upande huo pia.
Katika kipindi cha pili, Iran ilianza kuonyesha kujiamini na kuanzisha mashambulizi dhidi ya lango la Nigeria.
Mchuano huu ulielekea kuonekana kuwa hafifu na hakuna timu iliyoonyesha ukakamavu wa kuchuana na Argentina ama Bosnia.
Shola Ameobi aliingia katika nafasi yake Victor Moses katika dakika ya 52 na akaja karibu kuipatia Nigeria bao la kwanza baada ya kupewa pasi na Ramon Azeez.
Nigeria tena walikaribia kupata bao katika dakika za mwisho kupitia kwake Ogenyi Onazi.
Hata hivo mchuano huo ulitimia kuisha kwa sare tasa .


Ujerumani 4-0 Ureno

Thomas Mueller ndiye mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mechi moja Brazil
Thomas Muller alifunga mabao matatu na kuisaidia Ujerumani kuishinda Ureno mabao manne kwa nunge.
Mlinzi wa Ureno, Pepe alionyeshwa kadi nyekundu na kuondolewa katika mchuano huo.
Ujerumani, mabingwa mara tatu wa kombe la dunia, walionyesha mchezo wa kiwango cha juu. Ujerumani ilichukua uongozi pale ambapo Thomas Muller alipopiga mkwaju wa penalti, baada ya Joao Pereira kuchezea vibaya Mario Goetze.
Mart Hummels alifunga bao la pili kupitia kichwa.
Pepe alionyeshwa kadi nyekundu muda mfupi baadaye kwa kosa la kumgonga Muller kwa kichwa.
Pepe alionesha kadi nyekundu baada ya kumgonga kichwa Mueller
Muller alifunga bao la tatu, ambalo lilikua lake la pili katika mchuano huo, kwa mkwaju wa kutoka karibu na lango.
Katika dakika ya 77, Thomas Muller aliongeza bao la nne la Ujerumani na kufanya idadi ya mabao yake katika mchuano huo kuwa matatu.
Muller anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mechi moja, kwenye kombe hili la dunia, mwaka 2014.
Kufuatia ushindi huu, Ujerumani inaongoza kundi hili kwa alama tatu.
 

Marekani yaiibana Ghana 2-1


Marekani yalipiza kisasi cha kushindwa na Ghana 2-1katika kombe la dunia
Bao la kichwa la John Brooks, katika dakika za mwisho za mechi ziliisaidia Marekani kuilaza Ghana kwa mabao mawili kwa moja, katika mchuano wao wa kwanza wa kundi G, huko Natal.
Clint Dempsey alikua ameipa Marekani bao la kwanza chini ya dakika moja mchuano ulipoanza; Baada ya sekunde 31 pekee.
Hili ndilo lililokuwa bao la kasi kabisa katika historia ya taifa hilo katika kombe la dunia.
Marekani imelipiza kisasi kushindwa na Ghana katika mkondo wa mchujo kwenye kombe la dunia la mwaka 2010, Afrika Kusini.
Jozy Altidore angeongezea uongozi wa Marekani katika dakika ya kumi na tisa ila mkwaju wake ulizuiwa na kipa wa Ghana.
Altidore aliondolewa baadaye katika mechi hiyo baada ya kujeruhiwa.
Yawezekana kuwa hataweza kuichezea Marekani tena katika michuano iliyosalia ya kombe la dunia mwaka huu.
Kikosi hicho kitasalia na wachezaji 22 kwa michuano yao inayokuja kwani sheria za Fifa zinazuia wachezaji wengine kuongezwa katika kikosi baada ya kuanza kwa mashindano.
Ghana ingesawazisha kabla ya mapumziko wakati Christian Atsu alipompatia Jordan Ayew pasi nzuri.
Hata hivyo Ayew, anayeichezea timu ya Marseille huko Ufaransa, alitoa mwaju hafifu.
Katika kipindi cha pili, Ghana ilianza kutafuta bao la kusawazisha.
Asamoah Gyan alipewa nafasi nzuri ya kufanya hivyo lakini alipogeuka ili kuuondoa mpira, Geoff Cameron, wa Marekani alikua tayari keshafika na kulizuia jaribio hilo lake Gyan.
Marekani ilizidisha shinikizo lao la kutafuta bao la pili, hata hivyo Ghana ikatangulia kwa kusawazisha mnamo dakika ya 82, pale ambapo pasi yake Gyan, ilimfikia Andre Ayew naye bila kusita akautia mpira wavuni.
Marekani yalipiza kisasi cha kushindwa na Ghana 2-1katika kombe la dunia
Wachezaji wake mkufunzi, Jurgen Klinsmann, waligeuka na kuanza kutafuta bao la ushindi kwa dhati.
Graham Zusi alimpa pasi mchezaji wa akiba Brooks, kutoka kwenye kona.
Brooks aliugonga kwa kichwa mpira nao ukaingia wavuni katika dakika ya 86 na kuipa Marekani uongozi tena. Marekani ilidhibiti lango lao kwa dakika tano za ziada na kupata ushindi dhidi ya Ghana.
Mpira wa kichwa kutoka kwa John Brooks, katika dakika za mwisho za mechi ziliisaidia Marekani kuilaza Ghana kwa mabao mawili kwa moja, katika mchuano wao wa kundi G, huko Natal.
Awali, Clint Dempsey alikua ameipa Marekani bao la kwanza chini ya dakika moja mchuano ulipoanza; Baada ya sekunde 31.
Hili ndilo lililokuwa bao la kasi kabisa katika historia ya taifa hilo katika kombe la dunia.
Marekani imekipiza kisasi kushindwa na Ghana katika mkondo wa mchujo kwenye kombe la dunia la mwaka 2010, afrika Kusini.
Jozy Altidore angeongezea uongozi wa Marekani katika dakika ya kumi na tisa ila mkwaju wake ulizuiwa na kipa wa Ghana.
Altidore aliondolewa katika mechi hiyo baada ya kupata jeraha.
Yawezekana kuwa hataweza kuichezea Marekani tena katika michuano yao iliyosalia ya kombe la dunia mwaka huu.
Kikosi hicho kitasalia na wachezaji 22 kwa michuano yao inayokuja kwani sheria za Fifa zinazuia wachezaji wengine kuongezwa katika kikosi wakati huu.
Ghana ingesawazisha kabla ya mapumziko wakati Christian Atsu alipompatia Jordan Ayew pasi nzuri
Hata hivyo Ayew, anayeichezea timu ya Marseille huko Ufaransa, alitoa mwaju hafifu.
Mashabiki walioshuhudia Marekani ikiibana Ghana 2-1
Katika kipindi cha pili, Ghana ilianza kutafuta bao la kusawazisha.
Asamoah Gyan alipewa nafasi nzuri ya kufunga bao lakini alipogeuka ili kufyatua kombora , Geoff Cameron, wa Marekani alikua tayari keshafika na kuzima azimio lake .
Marekani ilizidisha shinikizo lao la kutafuta bao la pili, hata hivyo Ghana ikatangulia kwa kusawazisha katika dakika ya 82, pale ambapo pasi yake Gyan, ilimfikia Andre Ayew naye bila kusita akautia mpira wavuni.
Wachezaji wake mkufunzi, Jurgen Klinsmann, waligeuka na kuanza kutafuta bao la ushindi kwa dhati.
Graham Zusi alimpa pasi mchezaji wa akiba Brooks, kutoka kwenye kona.
Brooks aliugonga kwa kichwa mpira nao ukaingia wavuni katika dakika ya 86 na kuipa Marekani uongozi tena.
Marekani ilidhibiti lango lao kwa dakika tano za ziada na kulipiza kisasi kushindwa na black stars katika mashindano mawili ya kombe la dunia.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger