Monday, 16 June 2014

KAHABA AKAMATWA AKIJUZA NJE YA OFISI ZA SERIKALI

...
Njaa mbaya! Kama ulikuwa unadhani ile Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers imenywea, basi umenoa! Safari hii imenasa tukio la mrembo akijihusisha na biashara haramu ya ngono nje ya ofisi za serikali, Ijumaa Wikienda lina kitu laivu.
Mrembo aliyekuwa akijihusisha na biashara haramu ya ngono nje ya ofisi za serikaliakikurupuka mara baada ya kunaswa mtegoni.
Tukio hilo lisilo la kimaadili lilijiri usiku wa manane wikiendi iliyopita kwenye ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama, Dar.
Baada ya kupokea kero kwa wakazi wazalendo wa eneo hilo kuwa ofisi yao inanajisiwa, OFM ilifanya uchunguzi wake wa kina na ilipojiridhisha ndipo ikaweka mtego.
Kabla ya tukio ilisemekana kuwa pamoja na ngono kufanyika waziwazi na machangudoa waliopo maeneo mbalimbali ya Sinza na Kijitonyama, Dar, siku hizi wadada hao wafikia hatua mbaya zaidi kwa kufanyia maeneo yenye hadhi na sifa maalum kama viwanja vya shule za msingi, nje ya ofisi za watu, karibu na misikiti na makanisani.
Timu ya OFM kazini ikimdhibiti mrembo huyo aliyekuwa akifanya biashara haramu.
“Yaani siku hizi hawa wasichana hawani soni hata tone, wamefikia hatua ya kufanyia ngono sehemu rasmi tena bila kificho, kwa mfano pale maeneo ya Sinza-Mapambano si wanafanyia ngono kwenye uzio wa shule!
Ukifika pale asubuhi utakuta kondomu kibao. Hata pale kwenye ofisi za mtendaji utawaona wanafanyia ngono kule nyuma kwenye miti bila hata ya hofu,” alisema mmoja wa wakazi wa Kijitonyama.
Tukirudi kwenye tukio, OFM ikiwa doria chimbo, mishale ya saa nane na nusu usiku, hakukuwa na purukushani yoyote iliyoonesha viashirio vya ngono nje ya ofisi hiyo
Mrembo huyo akiwa chini ya ulinzi wa kachero mara baada ya kunaswa.
Ghafla nusu saa baadaye makamanda wa OFM waliokuwa katika kufunga vifaa vyao vya kazi, walishuhudia Bajaj ikisimama mbele na kumshusha mrembo mmoja maarufu kwa jina la Shishi akiwa na ‘mteja’ kisha wakajibanza kwenye miti nje ya ofisi hiyo.
Makamanda wa OFM walikuwa makini kufuatilia mchezo mzima ambapo waliwashuhudia wawili hao wakitandika khanga tayari kwa ajili ya ‘mambo yao’.
Baada ya kila kitu kuwa sawa ndipo makamanda walipiga simu kwa askari wa doria waliokuwa maeneo hayo na kuwavamia kisha kuwatia nguvuni ambapo katika kujitetea mrembo huyo alisema kuwa, mteja wake alimlazimisha kufanyia ngono katika eneo hilo kwa sababu alimaliza fedha zote kwa kumnunua yeye pombe.
Askari akimuingiza mrembo huyo kwenye gari kumpeleka kituoni.
“Najua eneo hili ni la serikali lakini huyu jamaa alikuwa na fedha kidogo na nyingine ya gesti nikaamua bora yote anipe mimi kisha nikamleta hapa. Nisameheni sitarudia,” alisema mrembo huyo huku mteja wake aliyeonekana kukolea kinywaji akiomba aachiwe kwa kuwa hakujua alilokuwa akilifanya.
Hadi OFM inaondoka eneo la tukio wawili hao walikuwa wametaitiwa mikononi mwa polisi ambapo kwa kawaida kisheria watashitaki kwa kosa la uzembe na uzururaji.
Alipotafutwa Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama ili kuzungumzia ishu hiyo hakupatikana hewani na hata alipofuatwa ofisini kwake kulikuwa na kufuli kubwa.
Imeandaliwa na Chande Abdallah, Richard Bukos, Deogratius Mongela na Issa Mnally.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger