Mlinzi wa Brazil Thiago Silva (Kushoto) na Mshambuliaji Neymar(kulia)
Mlinzi wa Brazil Thiago Silva hatocheza katika mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani Jumanne .
Hii ni baada ya juhudi za shirika la soka la Brazil kukata rufaa kwa shirikisho la soka duniani FIFA kutaka kadi ya pili ya njano iliyompelekea kutocheza mechi hiyo muhimu kutofanikiwa.
Fifa imetupilia mbali ombi la BFA la kuitaka ibatilishe kadi ya njano ambayo imemlazimu kocha Luiz Felipe Scolari kutafuta mlinzi mbadala kuziba pengo la nahodha huyo.
Thiago alioneshwa kadi yake ya pili timu hiyo ilipoilaza Colombia Ijumaa iliyopita.
Kauli hiyo ni pigo kwa wenyeji hao ambao tayari wamempoteza Mshambuli muhimu Neymar ambaye alijeruhiwa uti wa mgongo.
Kocha wa Brazil Scolari anapanga kumtumia Willian kuziba pengo la Neymar.
Scolari amesema kuwa Brazil itajitahidi dhidi ya Ujerumani licha ya kumkosa Neymar ambaye alikuwa ameifungia mabao manne.
Kwa upande wake kocha wa Ujerumani Joachim Low amesema kuwa Wabrazil ni wakakamavu na mara nyingi wanacheza kwa nguvu.
Timu hizo zitakutana kesho zitakapocheza mechi ya kwanza ya nusu fainali huko Belo Horizonte.
Matumaini ya wenyeji kutwaa ubingwa wa dunia yameimarika baada ya timu hiyo kufuzu kwa nusu fainali.
0 comments:
Post a Comment