

Akisimulia kuhusu mauaji hayo, ndugu wa marehemu aitwaye William Lomayany alisema usiku wa tukio, saa 4, mtuhumiwa alirejea nyumbani kwake na kutomkuta mkewe, akamsubiri hadi saa 6 usiku, mke akarejea.

William alizidi kusema kuwa, wawili hao walianza kugombana kwa maneno lakini baada ya muda hali ya utulivu ilirejea, ndipo asubuhi ilipopatikana taarifa za kuuawa kwa Agnes jambo lililotafsiriwa kuwa huenda utulivu huo tayari Agnes alishauawa.

Ilidaiwa kuwa, baada ya taarifa hiyo, majirani waliingia ndani ya chumba hicho na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umelala kwenye dimbwi la damu huku akiwa mtupu.

“Nilikwenda kufunga mlango, baba aliondoka bila kusema chochote. Lakini jana usiku (Julai 6) baba alimpiga sana mama na alinipiga na mimi wakati namwambia amsamehe,” alisema Jessica.
Majirani wa wanandoa hao, wamelaani mauaji hayo na kusema Lucas hakupaswa kumuua mkewe badala yake angewashirikisha watu wengine wakiwemo wazazi wamkanye kama alikuwa akimsaliti.
“Kwa jinsi Lucas alivyokuwa mpole sikutegemea kama angemuua mkewe kikatili, kama alikuwa akimsaliti angewaeleza wazazi wake ili wamkanye,” alisema jirani yao ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, uchunguzi unaendelea na jeshi lake linamsaka mtuhumiwa huyo.
0 comments:
Post a Comment