Monday, 9 December 2019

MWANAMKE AFUFUKA.... MAPIGO YAKE YA MOYO YALIZIMA SAA SITA...MADAKTARI WASIMULIA

Audrey alikosa fahamu kwa saa sita baada ya mapigo yake ya moyo kusimama

Mwanamke wa Uingereza ambaye alipata mshtuko wa moyo baada ya mapigo yake ya moyo kuacha kufanya kazi kwa saa sita amefufuka tena katika kile ambacho madaktari wamesema ni jambo ambalo halijawahi kutokea hapo kabla.

Audrey Schoeman alipata mshtuko wa moyo alipopigwa na dhoruba ya theluji wakati anapanda mlima Pyrenees akiwa na mumewe mnamo mwezi Novemba.

Madaktari wanasema huo ndiyo muda mrefu zaidi kwa mtu kuwahi kupata mshtuko wa moyo nchini Uhispania.

Audrey, ambaye kwa sasa anakaribia kurejea katika hali yake ya kawaida, amesema anatarajia kupanda tena mlima huo msimu wa masika.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34 anayeishi Barcelona, alianza kupata matatizo ya kuzungumza hali ya hewa ilipobadilika alipokuwa akipanda mlima na baadaye akapoteza fahamu.

Hali yake ilizorota zaidi wakati akisubiri kupata huduma za dharura na mume wake Rohan akaamini kwamba mkewe anakufa.

Akizungumza na vyombo vya habari Alhamisi iliyopita, Mumewe Rohan alikiambia kituo cha televisheni cha TV3: "Nilikuwa najaribu kumgusa, mapigo yake ya moyo hayakuwa yanapiga kabisa... Sikuweza kuhisi akipumua."Mume wa Audrey Schoeman, Rohan, ambaye alidhani mkewe amekufa

Timu ya uokoaji ilipofika saa mbili baadaye, joto la mwili la Audrey lilikuwa limeshuka hadi nyuzijoto 18.

Alipowasili katika hospitali ya Vall d'Hebron huko Barcelona, hakuwa na dalili zozote za kurejesha uhai.

Hata hivyo kiwango cha chini cha joto ambacho kilisababisha Audrey augue, pia kilimsaidia kunusuru maisha yake, amesema daktari wake Eduard Argudo.

"Alionekana kana kwamba amekufa,"amesema hivyo katika taarifa aliyotoa.

"Lakini tulichokifahamu hasa katika mshtuko wa moyo, tulijua kwamba kulikuwa na uwezekano wa Audrey kufufuka."

Joto la mwili lililinda mwili na ubongo wake usizorote zaidi wakati akiwa amepoteza fahamu, daktari Argudo amesema, licha ya kwamba alikuwa anaelekea kufa.

Aliongeza: "Kama angekuwa katika mshtuka wa moyo kwa kipindi hicho kirefu, joto la mwili wake likiwa kawaida, angekuwa amekufa."

Wakiwa katika hali ya kukimbizana na muda, madaktari wa Audrey waligeukia mashine maalum inayoweza kuondoa damu na badala yake wakamuingiza hewa ya oksijeni.

Joto la mwili wake lililofikia nyuzijoto 30, walitumia kifaa cha kufanya moyo uanze kupiga tena, saa sita baada ya kupata huduma ya kwanza.Audrey na Rohan Schoeman na walioshughulika kumpa huduma ya kwanza

Audrey alitolewa hospitali siku 12 baadaye, akiwa tu na matatizo ya hisia kwa sababu ya kiwango cha joto alichokuwa nacho wakati amepoteza fahamu.

"Tulikuwa na wasiwasi kuhusu madhara atakayopata katika mfumo wake wa neva," amesema daktari Argudo.

"Hasa ukizingatia kwamba hakuna mtu ambaye moyo wake ulisita kupiga kwa muda kama huo kisha ukuanza tena kufanya kazi."

Akizungumza baada ya kurejea katika hali yake ya kawaida, Audrey anasema hafahamu chochote kuhusu kilichotokea.

"Kwa siku ya kwanza na pili, sikujua kile kinachoendelea, eti nipo katika chumba cha wagonjwa mahututi," amesema.

"Lakini tangu wakati huo, nimekuwa nikijitahidi kusoma zaidi hasa kuhusu joto la mwili na kwa kweli na hisi furaha sana kuona nilinusurika kifo."

Audrey anasema anahisi yeye ni mwenye bahati na pia amewashukuru wafanyakazi wa hospitali hiyo.

"Ni kama miujiza na pia madaktari walichangia pakubwa, Audrey amesema.

Ameongeza kwamba kuna uwezekano mkubwa hatarejea tena kupanda mlima katika kipindi hiki.

"Kwa muda huu haitowezekana lakini nina imani kwamba msimu wa masika nitaweza kuupanda tena. Sitaki tukio hili liwe sababu ya kuachana na kile ambacho nimekuwa nikikipenda," amesema.
CHANZO - BBC
Share:

URUSI YAFUNGIWA MIAKA MINNE KUTOJIHUSISHA NA MCHEZO WOWOTE DUNIANI


Timu ya taifa ya soka ya Urusi

Urusi imefungiwa miaka 4 kutojihusisha na mchezo wowote duniani, baada ya kupatikana na hatia ya kufanya udanganyifu kuhusu vipimo na maabara juu ya utengenezwaji na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni.

Taarifa ya Shirika la kupinga dawa za kuongeza nguvu michezoni 'World Anti-Doping Agency' (WADA) leo Desemba 9, 2019, imeeleza kuwa Urusi inatakiwa kusimamishwa na mashirikisho yote yanayosimamia michezo duniani ikiwemo FIFA kwa upande wa soka pamoja na Kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC).

Kufungiwa huko ni wazi kuwa Urusi itakosa michuano mbalimbali mikubwa ndani ya miaka hiyo ikiwemo Olimpiki 2020, itakayofanyika jijini Tokyo Japan, pamoja na FIFA World Cup 2022 nchini Qatar.

Uamuzi huu umekuja ikiwa ni miaka minne imepita tangu uchunguzi mkali uanze kufanyika, ambapo tayari viongozi mbalimbali wa michezo nchini humo, wameshafungiwa kwa hatia hizo hizo za kuhusika kuruhusu wanamichezo kutumia dawa za kuongeza nguvu.

WADA wameweka wazi kuwa Urusi kupitia maabara zao za Moscow, waligoma kuchunguzwa na baadaye walipokubali walitoa taarifa feki na kisha kufuta baadhi ya taarifa ambazo zingeeleza ukweli juu ya suala hilo.

Kwa upande wa klabu ya Saint Petersburg ambayo inajiandaa na mchezo wake dhidi ya Man City kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, wao wataendelea pamoja na timu ya taifa itacheza EURO 2020 kutokana na michuano yote hiyo kuandaliwa na UEFA na sio FIFA.

Hata hivyo wamepewa siku 21 kuweza kukata rufaa katika mahakama ya kimataifa ya michezo 'Court of Arbitration for Sport' (CAS).
Share:

LOWASSA : KAMA RAIS MAGUFULI AKIACHIWA AKAPIGA MIAKA YAKE KUMI NCHI HII ITABADILIKA


Waziri mkuu za zamani, Edward Lowassa amesema Rais Magufuli akiongoza nchi kwa miaka 10 itapiga hatua kubwa katika maendeleo.


Lowassa  ametoa kauli hiyo katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika mjini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba.

"Amani ndio msingi anaoutumia mheshimiwa Magufuli leo kuongoza nchi yetu, kuleta mshikamano na umoja, nampongeza amefanya kazi nzuri sana…kama akiachiwa akapiga miaka yake kumi…kumi mheshimiwa nchi hii itabadilika,” – Amesema Lowassa

Lowassa alikihama Chama Cha Mapinduzi (CCM)  mwaka 2015 na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambako alipitishwa kugombea urais mwaka 2015 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu, lakini baadaye Machi Mosi, 2019, alirejea CCM.


Share:

SERIKALI YAITAKA TAASISI YA UHASIBU TANZANIA (TIA) KUBORESHA ZAIDI MITAALA YAKE

Mgeni Rasmi Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi ( kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango) akimkabidhi mmoja wa Wahitimu Shahada yake. 

Na Abby Nkungu, Singida

SERIKALI imeitaka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kuboresha zaidi mitaala yake ili iweze kuzalisha wataalamu mahiri wenye ujuzi na weledi kwa ajili ya kujibu changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa Sera ya uchumi wa Viwanda  hivyo kuwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kipato cha kati kabla ya mwaka 2025.


Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi  kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango mjini Singida wakati wa Mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Wahitimu 1,688 wa kozi za Cheti cha Awali, Astashahada, Stashahada na Shahada kutoka Kampasi za Mwanza, Kigoma na Singida.

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi, Waziri Mpango alisema fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa biashara na Uongozi wa raslimali watu ambako Kampasi za Kigoma, Mwanza na Singida  zimejikita, ni muhimu katika kuendesha uchumi wa Taifa; hususan katika kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma. 

Alisisitiza kuwa Sera ya nchi kwa sasa ni Uchumi wa Viwanda, hivyo umahiri wa Wataalamu wanaozalishwa na Taasisi hiyo lazima uonekane dhahiri ili kufanikisha azma ya Serikali ya Tanzania ya Viwanda. 

"Ili kukabiliana na changamoto za Usimamizi wa mapato na matumizi ya fedha za umma, mahitaji ya soko, ushindani na utandawazi mnapaswa kuboresha mitaala yenu kukidhi viwango vya Kimataifa katika umahiri badala ya maarifa tu ili kukabiliana na changamoto za utekelezaji wa Sera ya viwanda. Tunahitaji wataalamu wenye weledi, maarifa na umahiri wa kutatua changamoto na si kuongeza changamoto", alifafanua.

Aidha, aliwasihi wahitimu hao kuweka mbele suala la uaminifu na uadilifu kwa kuwa hiyo ndiyo silaha na dira sahihi ya maisha yao ya kila siku. “Uhasibu ni taaluma iliyotukuka; hivyo ni vyema ninyi mliosomea mkazingatia kwa kiwango cha juu miiko, kanuni na taratibu zinazotawala fani hiyo”.

Alieleza  kuwa kashfa mbalimbali zinazosikika nchini na kwingineko duniani ni matokeo ya  watu kukosa uaminifu na uadilifu.  “Mtakapotoka hapa baada ya kuhitimu masomo yenu, mtakutana na changamoto mbalimbali, ila mkumbuke ni uadilifu na uaminfu pekee ndio utakaowaongoza katika maisha yenu yote” ,aliwaasa.


Dk Mpango aliwataka wahitimu hao kutumia vyema elimu waliyoipata katika kubuni, kuanzisha na kusimamia shughuli mbali mbali za kibiashara zitakazowasaidia wao na jamii yote ya Watanzania katika kujiletea maendeleo.


“Hatua mliyofikia iwe chachu ya kujiimarisha zaidi kitaaluma ili kuweza kushindana katika soko la ajira na kujiajiri. Msipojiimarisha, mtajikuta kazi zenu zinachukuliwa na watu wa nje" alisema na kutoa angalizo; 

"Soko letu la ajira rasmi ni dogo na kwa kweli halikidhi mahitaji ya wahitimu wote nchini. Ili kukabiliana na changamoto ya soko la ajira, ni vyema mkaelekeza mawazo yenu kwenye kujiajiri badala ya kuajiriwa".

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Bi Luciana Hembe alitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo kuwa ni pamoja na gharama kubwa za pango katika Kampasi za Kigoma na Mwanza kutokana na kukosa majengo yao wenyewe na uhaba wa miundombinu ya majengo Kampasi ya Singida kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi. 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TIA, Saidi Chiguma aliwataka wahitimu hao kuzingatia uadilifu, nidhamu na uzalendo wakati wote ili kujipambanua na wahitimu wa vyuo vingine. 
Share:

Rais Magufuli Asamehe Wafungwa 5,533 Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, ametangaza kuwaachia wafungwa 5533 ambao walikuwa wamefungwa katika Magereza mbalimbali nchini.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho wa miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, ambapo kuna idadi kubwa ya wafungwa ambao wapo Magerezani kwa makosa ya kawaida sana.

“Nilitembelea Magereza nikashuhudia kuna mlundikano wa wafungwa, mpaka leo kuna Wafungwa 17,547 na Mahabusu 18,256, hii ni idadi kubwa, kwa hao wafungwa kuna baadhi wamefungwa makosa madogo, sijui kaiba kuku, kujibizana na mpenzi wake.

“Leo natangaza kuwasamehe wafungwa 5,533, ni mara ya kwanza kwa msamaha mkubwa kama huu kutokea, najua watu watashangaa lakini nimetumia siku hii ya Uhuru kusamehe, sifurahi kuongoza nchi yenye watu wengi Magerezani.

“Msamaha huu utawahusisha wafungwa waliofungwa kati ya kipindi cha siku moja hadi mwaka mmoja, na wale Wafungwa waliofungwa Miaka mingi kama 30, 20, 10 au mitano na wamebakiza muda mfupi kumaliza. Aliyewasamehe ni Mungu.” Rais Magufuli.


Share:

Form One Selection 2020 Ruvuma Region 2020/2021

Form One Selection 2020 Ruvuma Region 2020/2021 The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://Ruvuma.go.tz/ Form one selection for the academic year 2019/2020  The following students have been selected to join form one for Ruvuma Secondary schools for… Read More »

The post Form One Selection 2020 Ruvuma Region 2020/2021 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ruvuma Form one selection 2020

Form one selection – Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ruvuma Form one selection 2020 The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://ruvuma.go.tz/ Form one selection for the academic year 2020/2021  The following students have been selected to join… Read More »

The post Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ruvuma Form one selection 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Form One Selection 2020 Geita Region

Form One Selection 2020 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2020/2021  Geita Region for 2020/2021  Geita The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here http://Geita.go.tz/ Form one selection for the academic year 2020/2021  The following students have been selected to… Read More »

The post Form One Selection 2020 Geita Region appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

KAULI YA MBOWE LIVE MBELE YA RAIS MAGUFULI KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA UHURU


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowea,amehudhuria maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni hakuvaa sare maalum za chama wala kombati ambazo zinatumiwa kama vazi maalum chama chao lakini amepigilia suti nyeusi, shati jeupe na tai.


Taarifa ya kushiriki kwenye maadhimisho kwa Mwenyekiti wa CHADEMA ilitolewa juzi na Kamati Kuu ya chama hicho kwa kumuagiza Mwenyekiti wake kwenda kukiwakilisha chama hicho kwenye Sherehe hizo za Uhuru. Hii ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kushiriki kwenye maadhimisho ya Uhuru tangu mwaka 2015.

Akizungumza baada ya kupewa nafasi na rais Magufuli leo,Mhe. Mbowe ametoa kauli zifuatazo

"Nimekujua kuhudhuria maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru kama Uthibitisho wa Ulazima wa uwepo wa maridhiano,uwepo upendo,uwepo mshikamano katika taifa letu.

Nawapongeza sana Watanzania kwa siku ya leo na namuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama taifa la watu wanaopendana,tuvumiliane,tukosoane turuhusu demokrasia tujenge taifa lenye upendo na mshikamano 

Na Mhe. Rais kwa nafasi ya pekee tuna nafasi ya kuweka historia ya maridhiano katika taifa kwani kuna wengine wanalalamika,wengine wanaumia,Mhe. Rais tumia nafasi ukaliweke taifa katika hali ya utengamano" - Mbowe

Share:

Form One Selection 2020 Lindi Region

Form One Selection 2020 – Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2020 Lindi Region for 2020/2021 Lindi The List of Selected Candidates is available for each Ward Education Coordinator, Each Board’s Advertising Boards and the Office of the Regional Head Office, Check it here>> http://www.lindi.go.tz/ Form one selection for the academic year 2020/2021  The following students have been selected to… Read More »

The post Form One Selection 2020 Lindi Region appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Tangazo La Nafasi Za Masomk Form One, Darasa la Kwanza, Pili na Wanaotaka Kuhamia shule za lake Tanganyika

Tangazo ! Tangazo ;
Uongozi wa shule za lake Tanganyika zilizopo kijiji cha Mkigo wilaya ya kigoma vijijini mkoani kigoma unapenda kuwatangazia nafasi za masomo kwa mwaka 2020 kama ifuatavyo;


1.Nafasi za masomo kwa nursery, darasa la  kwanza, pili na tatu 

2.Nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza,na pia nafasi za kuhamia kwa kidato cha pili na tatu 

3.Pia kuna nafasi kuhamia za kidato cha tano  kwa comb HGK,HKL,HGL 

Shule ina  mazingira mazuri na ina  walimu wazoefu
Shule za lake Tanganyika zinamilikiwa na waktisto (SDA ) 

Ada zetu ni nafuu sana na zinalipwa awamu nne  kwa mwaka kwa upande wa secondary ada kwa mwaka ni 700000/= laki saba tu,na A- level karo ni laki saba na hamsini elfu ,750000/= na kwa upande wa  primary ada ni laki Tisa 900000/= tu kwa mwaka 

Nyote mnakaribishwa lake Tanganyika high school and pre and primary English medium 

Shule zote ni za bweni na kutwa kwa primary tu na pia ni mchanganyiko wavulana na wasichana 

Karibu lake Tanganyika ndo   suhulisho la  mwanao 

Kwa mawasiliano; 0769697667
0763091810
0756417203
0742208879
0692212326
0627557839 


Share:

WASHINDI WA WIKI PROMOSHENI YA KISHINDO CHA KUFUNGA MWAKA WALAMBA MIL.5


Mkurugenzi wa Tigo Kanda Ya Kaskazini Aidan Komba Akimkabidhi Elizabeth Makala Mshindi Wa Milioni Tano Katika Promosheni Ya Kishindo Cha Kufunga Mwaka Mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazin Aidan Komba akimkabidhi Julita Kimaro Mshindi Wa Milioni Moja katika promosheni ya kishindo cha kufunga Mwaka mkoani Arusha.
Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya Akimkabidhi. Tegemeo Enos Mshindi Wa Milioni Tano katika promosheni ya kishindo ch kufunga Mwaka mkoani Mwanza. 
Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Gwamaka Mwakilembe Akimkabidhi Mausel Magesa Mshindi Wa Milioni Tano katika promosheni ya kishindo ch kufunga Mwaka mkoani Mwanza.

Share:

JINSI MBOWE NA NYALANDU WALIVYOINGIA CCM KIRUMBA


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda yaKati, Lazaro Nyalandu wamewasili katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza,  kuhudhuria maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru.


Hata hivyo, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu hawakuvaa sare maalum za chama wala kombati ambazo zinatumiwa kama vazi maalum chama chao lakini wamepigilia suti nyeusi, mashati meupe na tai.

Taarifa ya kushiriki kwenye maadhimisho kwa Mwenyekiti wa CHADEMA ilitolewa juzi na Kamati Kuu ya chama hicho kwa kumuagiza Mwenyekiti wake kwenda kukiwakilisha chama hicho kwenye Sherehe hizo za Uhuru.

Hii ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kushirii kwenye maadhimisho ya Uhuru tangu mwaka 2015.


Share:

Picha: RAIS MAGUFULI ALIVYOPOKELEWA KWA SHANGWE UWANJA WA CCM KIRUMBA


Rais Magufuli ameingia Uwanjani wa CCM Kirumba Mwanza jijini Mwanza huku akipokewa kwa shangwe na vigeregere kutoka kila kona ya uwanja huo uliofurika.Rais Magufuli aliingia uwanjani hapo saa 3: 14 asubuhi leo Jumatatu Desemba 9, 2019 akiwa kwenye gari la wazi akiongozwa na pikipiki nane gari moja mbele na nyingine nyuma.


Ameingilia mkono wa kushoto mwa uwanja na kuuzunguka akiwapungia wananchi mikono huku akishangiliwa kila alipopita wakati ukiimbwa wimbo wa taifa.
Share:

LIVE: Sherehe Za Miaka 58 Ya Uhuru Wa Tanzania Bara CCM - Kirumba Jijini Mwanza

Live: Maadhimisho Ya Miaka 58 Ya Uhuru Mwanza


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu December 9


Share:

Sunday, 8 December 2019

Bilionea Ali Mufuruki Afariki Dunia

Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Infotech Investment Group ambaye aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, Ali Mufuruki (60), amefariki  Dunia usiku wa kuamkia leo Disemba 8, 2019  akiwa Afrika Kusini akipatiwa matibabu.

Mufuruki ni kati ya matajiri wakubwa 10 wa Tanzania akiwa ni mmiliki wa Kampuni ya Infotech Investment Group Limited na maduka ya Wolworth.

Oktoba 18, 2019 Mufuruki alijiuzulu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania ili kupata muda zaidi wa kuendelea na biashara zake.

Mwenyekiti wa sasa wa Ceort, Sanjay Rughan amethibitisha kutokea kwa kifo hicho kilichotokea saa tisa alfajiri katika Hospitali ya Morningside.Share:

Job Opportunities at Tazama Pipelines Limited

Overview: Tazama Pipelines Limited, an interstate organization owned by the United Republic of Tanzania and the Republic of Zambia and which deals in transportation of crude oil from Dar es Salaam to Ndola, Zambia, wishes to invite applications from suitably qualified candidates to fill the under-mentioned posts below: Vacancy title: Cook  MAIN DUTIES: Undertakes timely the provision of meals… Read More »

The post Job Opportunities at Tazama Pipelines Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Executive Editor Job Opportunity at BBC Media Action

Executive Editor Job Opportunity at BBC Media Action Job Title: Executive Editor Location: Dar es Salaam, Tanzania Special Requirements: Right to work in Tanzania Reports to: Country Director, Tanzania Contract:  Full-time, 24 months with possible extension Salary: Highly competitive within Tanzania, NGO market rates Please do not send certificates or other attachments. Applicants with no separate cover letter will not… Read More »

The post Executive Editor Job Opportunity at BBC Media Action appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Senior Policy Adviser Job Opportunity at BBC Media Action

Job Opportunity at BBC Media Action, Senior Policy Adviser – Gender Equality & Social Inclusion (GESI) Job Title:  Senior Policy Adviser – Gender Equality & Social Inclusion (GESI) Location: Dar es Salaam, Tanzania Special Requirements: Right to work in Tanzania Reports to: Country Director, Tanzania Contract:  Full-time, 24 moinths with possible extension Salary: Highly competitive within Tanzania, NGO market rates Please do not send… Read More »

The post Senior Policy Adviser Job Opportunity at BBC Media Action appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Project Officer Gender Job Opportunity at BBC Media Action

Project Officer Gender Job Opportunity at BBC Media Action Job Title: Project Officer- Gender Location: Dar es Salaam, Tanzania Special Requirements: Right to work in Tanzania Reports to: Project Manager, Tanzania Contract:  Full-time, 24 months with possible extension Salary: Highly competitive within Tanzania, NGO market rates Please do not send certificates or other attachments. Applicants with no separate cover letter will… Read More »

The post Project Officer Gender Job Opportunity at BBC Media Action appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

48 Data Clerks  Positions  at The USAID Boresha Afya Southern Zone

Data Clerks 48 Positions   VACANCY ANNOUNCEMENT The USAID Boresha Afya Southern Zone is a five-year (1 October 2016 – 30 September 2021) PEPFAR supported program through USAID. Deloitte Consulting Limited implements the program in 42 councils in Iringa, Njombe, Morogoro, Lindi, Mtwara and Ruvuma with its technical partners Family Health International (FHI360), Engender Health and Management and Development for… Read More »

The post 48 Data Clerks  Positions  at The USAID Boresha Afya Southern Zone appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

9 District Data Officers Job Opportunities at USAID Boresha Afya

District Data Officer 9 Positions VACANCY ANNOUNCEMENT The USAID Boresha Afya Southern Zone is a five-year (1 October 2016 – 30 September 2021) PEPFAR supported program through USAID. Deloitte Consulting Limited implements the program in 42 councils in Iringa, Njombe, Morogoro, Lindi, Mtwara and Ruvuma with its technical partners Family Health International (FHI360), Engender Health and Management and Development… Read More »

The post 9 District Data Officers Job Opportunities at USAID Boresha Afya appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Program Officer, Clinical Services (3 posts) at The Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI)

Program Officer, Clinical Services (3 posts) The Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) is a non-governmental organisation that plays a pivotal role in complementing the Government of Tanzania’s efforts towards the attainment of its development goals. AGPAHI strives to provide quality and integrated HIV/AIDS health services to children and families. AGPAHI supports the provision of high-quality HIV and… Read More »

The post Program Officer, Clinical Services (3 posts) at The Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Program Officer- Pediatrics HIV and AIDS Job Opportunities at AGPAHI

 Program Officer, Pediatrics HIV and AIDS (2) The Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) is a non-governmental organisation that plays a pivotal role in complementing the Government of Tanzania’s efforts towards the attainment of its development goals. AGPAHI strives to provide quality and integrated HIV/AIDS health services to children and families. AGPAHI supports the provision of high-quality HIV… Read More »

The post Program Officer- Pediatrics HIV and AIDS Job Opportunities at AGPAHI appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

UDOM: Tentative approval list for the students who requested to be transferred 2019/2020.

UDOM: ANNOUNCEMENT TO STUDENTS WHO APPLIED FOR TRANSFERS (INTER-AND INTERNAL UNIVERSITY TRANSFERS) FOR THE 2019/2020 ACADEMIC YEAR The University of Dodoma (UDOM) would like to inform students who applied for transfers that their tentative approval within the University has been already established pending to the final approval. The following is the tentative approval list for the students who… Read More »

The post UDOM: Tentative approval list for the students who requested to be transferred 2019/2020. appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Jingu Aipeleka Kampeni Ya Makazi Bora Monduli

Na Mwandishi Wetu Arusha
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewataka wananchi kuhakikisha wanaboresha makazi yao kutoka makazi ya nyumba za nyasi na tembe kwenda nyumba za tofali na bati.

Aliyasema hayo leo Wilayani Monduli mkoani Arusha alipokuwa akitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoamasishwa na wataalam kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli kwa kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika miradi ya Maendeleo.

Dkt. Jingu aliwataka wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini kuhakikisha wanakuwa chachu ya mabadiliko na wanawezesha jamii kuwa na mawazo chanya ya kujiletea maendeleo na kubadili changamoto kuwa fursa za kimaendeleo.

"Wataalam wa Maendeleo ya Jamii tuweke nguvu katika kuhakikisha tunabadili jamii zetu kuwa na mawazo chanja hasa ya kujitegemea na kujiletea maendeleo" alisema Dkt. Jingu.

Dkt. Jingu aliongeza kuwa Sekta ya Maendeleo ya Jamii inapaswa kuwa chachu ya maendeleo katika taifa letu hivyo Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinatakiwa kutoa wataalam wenye weledi na stadi za kubwa za kuleta mabadiliko katika jamii.

"Vyuo vya Maendeleo ya Jamii tutoe wataalam wenye weledi  wa kuhakikisha tunatumia fursa zilizopo katika jamii kutatua changamoto zilizopo" alisema Dkt. Jingu.

Wakati huohuo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Dkt. Jingu amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatumia stadi watakazopata kubadilisha maisha yao na jamii kwa ujumla.

Dkt. Jingu aliwataka wanafunzi hao kuitumia bahati ya kuwa mmoja ya wanafunzi katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli kwa kuhakikisha wanafanikisha ndoto zao walizozilenga kuzitimiza katika maisha yao kwa kuzingatia masomo na nidhamu.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Bw. Elibariki Ulomi alimuhakikishia Katibu Mkuu kuwa Chuo hiyo kitahakikisha kinashirikiana na wananchi wa Wilaya ya Monduli katika kutekeleza Kampeni ya Makazi Bora ili kuwawezesha wananchi kuboresha makazi yao na kuhakikisha kinatoa Wataalam wa Maendeelo ya Jamii watakosaidia kuleta mabadiliko katika taifa.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli Bi. Rose Mhina alisema kuwa Halmashauri hiyo imeshaanza kutekeleza kampeni ya Makazi bora kwa kuipeleke ajenda hiyo kwa madiwani na kutoa michoro maalum kwaajili ya ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu.

Aliongeza kuwa Kampeni hiyo ya kuhamaisha ujenzi wamakazi bora itahamasishwa na katika jamii na maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka wilayani maoaka kwemye kata ili kuhakikisha wananchi wanajitoa na kuboresha makazi yao.

Kampeni ya Kuboresha makazi inalenga kuiwezesha jamii ambayo inaishi katika makazi yasiyo bora kuweza kuboresha makazi yao kwa kutumia ramani ziliziotolewa na Halmashauri walizopo zikiwa ni nyumba za gharama nafuu.

MWISHO.


Share:

TRA Yang’ara Tuzo Za NBAA , Yapata Ushindi Wa Jumla

Na Veronica Kazimoto-Dar es Salaam
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeshinda tuzo mbili ikiwemo mshindi wa jumla katika uandaaji bora wa taarifa za hesabu mwaka 2018 kwa kufuata viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu katika Taasisi za Umma yaani mfumo wa IPSASs.

Katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam, TRA imeibuka mshindi wa kwanza katika uandaaji bora wa taarifa za hesabu kwenye kipengele cha Wakala wa Serikali na mshindi wa jumla kwa taasisi, wakala, kampuni na mashirika mbalimbali ambayo yamefanya vizuri katika kuandaa taarifa za fedha katika shughuli zao za kila siku.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hizo, Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Edwin Mhede, ameipongeza Idara ya Fedha na idara nyingine ndani ya mamlaka hiyo kwa kufanikisha upatikanaji wa tuzo hizo.

“Nachukua nafasi hii kumshukuru mkuu wa idara anayehusika na Idara ya Fedha pamoja na wakuu wa idara nyingine ndani ya mamlaka maana zote zinatoa mchango mkubwa kuhakikisha idara hii inatoa taarifa sahihi na zenye kuleta mipango sahihi kwa mamlaka na serikali kwa ujumla,” alisema Dkt. Mhede.

Dkt. Mhede alieleza kuwa, taarifa sahihi ni msingi wa mipango kwa kuwa taasisi isiyopanga kushinda ni sawa na taasisi inayopanga kushindwa hivyo suala la uandaaji bora wa taarifa za hesabu ni moja ya ufanisi wa ofisi yoyote hapa ulimwenguni.

Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) ndio hutoa tuzo hizo kila mwaka ambapo mwaka 2017 TRA iliibuka mshindi wa kwanza tena katika uandaaji bora wa taarifa za hesabu katika kipengele cha Wakala wa Serikali.

Mwisho.Share:

Jafo Akerwa Na Utendaji Kazi Wa Watumishi Manispaa Ya Shinyanga

SALVATORY NTANDU
Waziri wa nchi ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo amemwagiza katibu Mkuu wake TAMISEMI kuwahamisha vituo vya kazi Maafisa wawili wa Manispaa ya Shinyanga baada ya kubainika kufanya kazi kwa makundi hali ambayo inaweza kukwamisha shughuli za Umma.

Waziri Jafo amewataja maafisa hao kuwa ni pamoja na Ofisa utumishi wa manispaa ya Shinyanga, Magedi Magezi pamoja na Mweka hazina Paschal Makoye, wahamishwe na  kuwapelekwa katika katika vituo vingine vya kazi.

Jafo ametoa agizo hilo jana baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Shinyanga, kutoka kwa  mkuu wa mkoa wa shinyanga,  Zainab Telack, katika ziara yake ya kikazi ya siku moja iliyoenda sambamba  na ukaguzi wa  ujenzi wa hospitali halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

“Kuna tabia ya watumishi katika manispaa hii wanafanya kazi kwa  makundi na hakuna umoja hasa wakuu wa idara kila mtu ni  mtawala na kusababisha utendaji kazi mbovu nimeamua kuwaondoa ili wakafanya kazi katika sehemu nyingine kuliko kuliko kuwaacha wakiendelea kuwagawa watumishi”alisema Jafo.

Waziri Jafo amesema TAMISEMI itaendelea kufuatilia nyendo za watumisho wote  wa Halmshauri nchini ambao wanafanya kazi kwa mazoea ambao hawaendi na kasi ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli kwa kuwachukilia hatua za kidhamu ikiwanipamoja ka kuwahamisha katika vituo vya kazi.

“Mimi niko hapa kumsaidia Mh,Rais na siwezi kukubali kuona watumishi wanafanya kazi kwa makundi,nimeshatoa maelekezo kwa wakuu wote wa idara kufanya kazi kwa kushirikiana ili ufanisi wa shughuli za serikali ziweze kufanikiwa na wananchi wapate huduma bora”alisema Jafo.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo, amepongeza ujenzi wa hospitali halmashauri ya wilaya ya Shinyanga baada ya kuyakagua na kuridhika na ujenzi wake na kusema kuwa  Rais Dk John Magufuli amekubali kutoa  Shilingi Milioni 500 ziwezekutumika kuongeza majengo mengine.

Nae  mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, alibainisha kuwa  kuwa  Serikali ilitoa Shilingi, Bilioni 3 kwaajili ya kujengwa hospitali mbili za wilaya katika mkoani huo, katika Halmashauri za Ushetu na Shinyanga  ambazo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 90.

Mwisho.


Share:

Rais Magufuli Pamoja Na Mkewe Mama Janeth Magufuli Wasali Misa Takatifu Dominika Ya Pili Ya Majilio Katika Kanisa Kuu La Epifania Parokia Ya Bugando Jijini Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wamejumuika pamoja na waumini wengine wa Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza  katika Misa Takatifu ya Dominika ya pili ya Majilio iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande leo tarehe 8/12/2019.Share:

Kijana Wa Kazi Amuibia Bosi Wake Hati Na Kuikopea

Na. Hassan Mabuye, WIZARA YA ARDHI-Iringa
Mkazi wa Iringa mjini Bi. Lugano Mwadini amejikuta katika deni linalopelekea karibu nyumba yake kupigwa mnada baada kijana wake wa kazi kukopa pesa kiasi cha shilingi 1,000,000 kwa kutumia hati yake ya umiliki wa ardhi ambayo amemuibia.

kadhia hiyo imetokea wakati wa mkutano wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kupitia programu yake ya 'Funguka kwa Waziri' mkoani Iringa alipokuwa akisikiliza na kutatua kero za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Iringa katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo katika Manispaa ya Iringa.

katika mkutano huo Bi. Lugano alimtuhumu Kijana wake wa kazi kwa kumuibia hati na kuenda kukopa kwa Bw. Laurence Panklas ambaye ni askari wa jeshi la polisi mkoani Iringa anayekopesha kwa riba ya 400,000 kila mwezi ambazo kijana huyo hakuweza kuzirudisha kwa wakati jambo lililopelekea kutaka kuuzwa kwa nyumba yake ili kufidia deni hilo.

Bi. Lugano Mwadini aligundua hayo baada ya kupigiwa simu na mkopeshaji huyo kumtaka kwenda kubalisha umiliki wa hati hiyo ili apewe mtu mwingine kwa kuwa hati yake imekopewa na inadaiwa shilingi 1,400,000.

"Mi nilikuwa sipo lakini nikaja kupata taarifa kwa kupigiwa simu kwamba kijana wangu wa kazi ameniibia hati yangu wakati nikiwa katika kazi zangu na amekopea kwa askari mmoja ambaye anakopesha kwa riba ya laki nne kila mwezi, kwa hiyo kijana wangu anadaiwa 1,400,000 na hajalipa hadi sasa" Alisema Bi. Lugano Mwadini.

Waziri Lukuvi alimuagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire kushughulikia suala hilo, kwanza kwa askali wa jeshi la polisi ambaye anafanya biashara ya pesa na kama ana kibali cha biashara hiyo na analipa kodi, kama halipi basi alipe kodi kwa miamala yote aliyowahi kufanya.

Aidha Waziri Lukuvi aliagiza kukamatwa kwa kijana huyo wa kazi ili alipe deni hilo kwa Bosi wake na kueleza kwanini amefanya uhalifu huo wa kuiba hati ya mtu mwingine.

Katika mkutano huo Waziri Lukuvi aliweza kusikiliza na kutatua migogoro ya wakazi wa mkoani Iringa takribani 200 kwa siku moja ambapo baadhi ya wananchi walieleza kuridhishwa kwa juhudi za waziri lukuvi kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi ya wakazi wa maeneo mbali mbalibila nchini bila kubagua.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

FUNGUA PAZIA

NDOA ZA UTOTONI

Narudi nyumbani

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger