Monday 31 May 2021

JAJI MKUU PROF JUMA AWATAKA MAJAJI KUZINGATIA MAADILI ,UADILIFU NA KUMTANGULIZA MUNGU MBELE


Jaji mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akifungua mafunzo hayo
Jaji mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amewataka majaji wa mahakama ya rufaa na mahakama kuu kutoogopa kusema au kutoa taarifa katika vyombo husika wanapobaini mapungufu katika sheria.

Jaji Mkuu Juma ametoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo elekezi kwa majaji 31 wa mahakama ya rufaa na mahakama kuu Tanzania Bara na Visiwani ambao waliteuliwa na kuapishwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan yaliyofanyika katika Chuo Cha Uongozi wa mahakama (IJA) kilichopo Lushoto Tanga.

Jaji Mkuu Juma aliwataka majaji kuzingatia maadili na uadilifu na kumuweka Mungu mbele katika maamuzi yao kwa sababu maamuzi hayo yanagusa maisha ya watu wengi.

Akisisitiza juu ya jukumu la majaji kuwa watafsiri wakuu wa sheria, alisema kuwa wanapokwenda kufanya kazi watakutana na mapungufu ya sheria na kusema kuwa kazi kubwa ya majaji ni kutafsiri sheria na katiba.

Profesa Juma alisema kuwa majaji wajielewe kuwa wao ni viongozi na sehemu ya maboresho hivyo wasikae kimya wanapobaini mapungufu katika sheria ili zifanyiwe maboresho kwa faida ya watanzania.

Alisema kuwa katiba imewakopesha viongozi hao wa mahakama mambo Fulani na kubakisha mambo mengine ambayo ni haki za wananchi zinazotakiwa kulindwa.

Kwa upande wake Jaji Kiongozi Eliezer Feleshi alisema mafunzo hayo ni ya pili kufanyika kwa majaji wa rufaa, ya sita kwa majaji wa mahakama kuu, na mara ya pili kwa majaji wa Tanzania bara na visiwani.

Alisema mafunzo hayo ni uthibitisho kuwa maboresho yanajengewa misingi bora ya utekelezaji.

Pia jaji huyo kiongozi alikisifu Chuo cha Mahakama kwa kuwa msaada kwa kuandaa mafunzo hayo yanayoongozwa na jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa, jaji salimu masati.
Jaji kiongozi wa mahakama nchini Eliezer Feleshi akizungumza kwenye mafunzo hayo

Share:

TBS NA KEBS KUSHIRIKIANA KUONDOA VIKWANZO VYA KIBIASHARA

MASHIRIKA ya viwango ya Kenya na Tanzania yamejipanga kuhakikisha yanashirikiana ili kuhakikisha hakuna vikwazo vya kibiashara vinavyohusiana na viwango vinavyoweza kutokeaa baina ya nchi hizo biashara.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Yusuf Ngenya, wakati wa ziara katika kituo cha pamoja cha mpaka wa Namanga ambayo ilihusisha Mawaziri na Viongozi mbalimbali kutoka nchi za Tanzania na Kenya.

Ziara hii kwa viongozi imefanyika baada ya kukamilika kwa Mkutano wa tano baina ya Tanzania na Kenya kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya biashara ikiwemo vikwazo vya biashara.

Mkutano huo uliofanyika kuanzia Mei 26 hadi 29, mwaka huu jijini Arusha Alisema wao kama TBS na wenzao wa Kenya (KEBS) walizungumzia masuala yanayohusiana na viwango na waliyaweka vizuri.

Alisema kwenye mkutano huo alizungumza mambo mengi ya Afrika Mashariki yanayohusiana na viwango ambayo yameweka vizuri, kwani kuna viwango ambavyo wamepitisha kwa pamoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita imeishaweka wazi kwamba inataka kufungua nchi kibiashara na kutoa wito wa kushirikiana baina ya Kenya na Tanzania.

"Kwa upande wa pande hizi mbili (Tanzania na Kenya) kulikuwa na vikwazo ambavyo vinahusiana na viwango na hivyo tumeishazungumza na wenzetu wa Kenya na tumeishayaweka vizuri na Serikali ya Awamu ya Sita imeweka wazi muelekeo wake wa kibiashara," alisema Dkt. Ngenya na kuongeza;

"Na sisi tutashirikiana na KBS kuhakikisha hakuna vikwazo vya kibiashara vinavyoweza vinavyoweza kutokana na TBS au KEBS."

Kwa upande wake Bw. Gervas Kaisi, Meneja wa Uthibiti Ubora TBS alisema katika kutatua changamoto za kibiashara baina ya Kenya na Tanzania, wameangalia suala zima la ubora wa bidhaa zinazotoka Kenya kuja Tanzania na zile zinazotoka Tanzania kwenda Kenya.

Alisema hizo changamoto zinatatulika, hivyo alitoa wito kwa wafanyabiashara kutokuwa na wasiwasi.

Alitoa mfano kwamba kulikuwa na changamoto ya mahindi yanayotoka Tanzania kwenda Kenya yaliyokuwa yanazuiliwa mpakani.

"Lakini sasa tumeona kuna umuhimu wa kuwa na vifaa katika hayo maeneo ambavyo vitatupa vipimo vya haraka haraka ili kutuonesha kwamba kuna sumukuvu au hakuna sumukuvu," alisema.




Share:

Tiba Bora Ya Tatizo La Nguvu za Kiume


Je, unakosa hamu ya tendo la NDOA? Una upungufu wa nguvu za kiume au maumbile madogo ya UUME?Changamoto hizi zimesababisha wanaume wengi kushindwa kumudu tendo la NDOA nakusababisha wenza wao kutoka nje ya ndoa au mahusiano. Zijue dalili na tiba sahihi ya matatizo hayo kama ifuatavyo:-

    *DALILI NI KAMA:-

1.Kukosa ham ya tendo
2.Kuwahi kufika kelele ni
3.Kushindwa kurudia tendo
4.Maumbile kusinyaa katikati ya tendo
5.Kuchoka sana baada ya raundi moja
6.Kusimama kwa ulegevu

    *TIBA SAHIHI

1.GING SENG PILLS @220,000/=
>Hivi ni vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza ham na nguvu za kiume hata kwa wenye kisukari

2.VIGRX OIL @220,000/=
>Huongeza Maumbile  kwa 6-7 inch ndani ya wiki mbili

3.BIG PENIS, VIMAX, GOOD MAN @270,000/= (Vidonge)
>Huongeza  nguvu za kiume na kuimarisha misuli hata kwa waliothiriwa na kujichua

4.HANDSOME UP @270,000/=
>Mashine hii huongeza maumbile kwa saizi unayotaka pamoja na kuimarisha misuli

5.VIGA SPRAY @180,000/=
>Huchelewesha kufika kileleni na kuongeza parfomance.

       Tiba hizi zote zimefanyiwa majaribio na zimethibitishwa. Matokeo ni uhakika na garantii.

            Fuatilia huduma na vipindi vyetu ktk mitandao ya kijamii ili kupata ushauri na tiba.

           ***YOU TUBE***
           Markson Beauty

   *GOOGLE/FACE BOOK*
Markson Beauty Products

         ***INSTAGRAM***
      @markson_beauty_pr
      @markson_beauty_pr

    Wasiliana nasi popote ulipo duniani kwa call/whatsapp no (+255)

           0767447444
                     na
           0714335378
        
TAHADHARI:- Hakikisha ndani ya bidhaa kuna mhuri, risiti na kadi ya garantii ktk bidhaa unayonunua kwenye kampuni hii.
 
     FREE DELIVER IN:-
*D'salaam
*Arusha
*Morogoro
*Mwanza
*Moshi

#HipsNaMakalio
#BidhaaTz
#YodiPillsTz
#BotchoOg
#CosmeticsTz
#WeupeBilaDoa
#FashionsTz
        
   MARKSON BEAUTY CO
    #HOUSE OF BEAUTY#

         < WELCOME ALL>
.

Share:

JAFO ATOA MIEZI MIWILI KWA UONGOZI WA KIWANDA CHA QUAIM STEEL MILLS KUHAKIKISHA WANADHIBITI MOSHI

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa kiwanda cha Quaim Steel Mills limited mara baada ya kutembelea kiwanda hicho katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelekezo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kiwanda cha Kamel Steel Industry kinachozalisha nondo katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akikagua baadhi ya nyaya zilizotengenezwa na madini ya kopa kwenye kiwanda cha OK Plast Limited katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kiwanda cha OK Plast limited kinachotengeneza nyaya za umeme kwa kutumia madini ya kopa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na uongozi wa kiwanda cha OK Plast limited kinachotengeneza nyaya za umeme kwa kutumia madini ya kopa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo amekiagiza kiwanda cha Quaim Steel Mills limited kuhakikisha kufikia miezi miwili kiwe kimejitengenezea mkakati wa kuhakikisha moshi wa kiwanda hicho hautoki na kusambaa kusababisha uchafuzi wa mazingira.

Ameyasema hayo leo Mhe.Jafo mara baada ya kutembelea kiwanda hicho katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ziara hiyo Waziri Jafo amewaagiza wenye kiwanda hicho kuhakikisha wanakifanyia marekebisho kiwanda hicho kwaajili ya kulinda afya za wananchi hususani ajenda ya utiririshaji wa moshi hivyo amewataka NEMC baada ya miezi miwili kufika katika kiwanda hicho na kukagua kama kimeshafanyiwa marekebisho.

"Kiwanda cha Quaim Steel Mills limited nimewapa miezi miwili waweze kufanya marekebisho makubwa katika kiwanda chao kwa lengo la kukidhi sheria ya mazingira no.20ya mwaka 2004". Amesema Waziri Jafo.

Aidha Waziri Jafo mewataka wenye viwanda nchini kuhakikisha wanazingatia afya za wananchi kwa kuhakikisha viwanda hivyo havitirirshi moshi ama maji taka ambayo yataenda kuathiri watanzania.

Hata hivyo Waziri Jafo amesema atakaa na kuzungumza na Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha wanavisaidia viwanda vya ndani viweze kufanya kazi vizuri na kuhakikisha mazingira yanatunzwa na vijana wa kiktanzania kupata ajira kupitia viwanda hivyo.

Share:

Prof. Mkumbo: Serikali Inaendelea Kuboresha Mazingira Ya Biashara Mpakani, Wafanyabiasha Zingatieni Sheria Na Taratibu Za Kufanya Biashara.


Na Eliud Rwechungura
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (Mb) amewahakikishia Wafanyabiashara kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ili kuhakikisha wanafanikiwa huku akiwahasa wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya kuzingazia Sheria na taratibu zilizowekwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuondokana na vikwazo ambavyo vimekuwa vikiwekwa  kutoka na kutozingatia Sheria na taratibu za kufanya biashara mipakani.

Prof. Mkumbo ameyasema hayo 30 Mei 2021 alipoambatana na Mawaziri wa Kenya na Tanzania kutembelea Mpaka wa Namanga kujionea jinsi biashara na shughuli za upitishaji wa bidhaa na huduma zinafavyofanyika katika Mpaka huo baada ya nchi hizo kukubalina kuondoa vikwazo 30 vya biashara visivyokuwa vya kiushuru.

“Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anataka kuona Maisha ya Watanzania yanaboreka na biashara zinafanyika vizuri, niwahakikishie wafanyabiashara wa Watanzania, Serikali yenu ipo na nyie na itaendelea kuwaunga mkono na kuwapa msaada ili kuona mnafanikiwa lakini kwa upande wenu tunaomba katika kufanya kwenu biashara mzingatie sheria na taratibu zilizopo kwasababu nchi zetu zinaongozwa na utawala wa sheria” ameeleza Prof. Mkumbo

Ameongeza kuwa, lengo la ziara hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Waheshimiwa Marais wa Tanzania na Kenya ya kuhakikisha mahusiano ya wananchi wa nchi mbili yanaboreka lakini muhimu Zaidi biashara hazikwami ndo maana wamekutana Mawaziri kutatua mambo mengi yaliyokuwa yanakwamisha biashara ikiwemo changamoto ya mahindi hapa mpakani wameweza kuizungumzia  na anashukuru imetatuliwa na mambo mengine mengi yalikuwepo pande zote mbili za Tanzania na Kenya.

Aidha, Prof. Mkumbo amewapongeza wataalam wa pande zote mbili za Tanzania na Kenya kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya huku akiwahasa kuendelea kuimalisha mahusiano mazuri kwa kukaa Pamoja na kujadiliana kwa kuzitatua changamoto kwasababu ni jambo kubwa na la muhimu viongozi wetu wanalotaka kuliona

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda, Biashara na Maendeleo ya Wajasiliamali nchini Kenya Mhe. Betty Maina amefurahishwa na kuona changamoto 30 kati ya 64 zimetatuliwa na hizo nyingine zilizobaki wamejiwekea muda wa miezi mitatu kuzifanyia kazi huku akiwataka wafanyabiashara wa pande mbili kuendelea kuzingatia sheria ambazo zimewekwa kwa pande zote mbili za Kenya Tanzania wakati wa ufanyaji biashara.


Share:

ANAYEDAIWA KUWA JAMBAZI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI SHINYANGA MJINI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Idd Masasi (43) anayedaiwa kuwa ni Jambazi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi mguuni na mgongoni na askari polisi wakati akijaribu kuwakimbia katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Mei 31,2021, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema Mei 30,2021 Jeshi la polisi lilipata taarifa fiche za uwepo wa Jambazi aitwaye Idd Masasi mkazi wa Ndembezi Mjini Shinyanga na makazi mengine Kigamboni Jijini Dar es salaam.

“Mtuhumiwa huyo alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha hasa matukio yaliyotokea hivi karibuni Kigamboni jijini Dar es salaam. Taarifa fiche zilieleza kuwa jambazi huyo amekimbilia hapa Shinyanga baada ya kutenda matukio ya unyang’anyi jijini Dar es salaam hivi karibuni”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

“Taarifa zilisema mtuhumiwa huyo anapenda kutembelea maeneo ya Soko la Nguzo Nane Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kusoma maeneo ya kutenda uhalifu ikizingatiwa kuwa eneo hilo lina wafanyabiashara mbalimbali”,ameongeza.

Amebainisha kuwa kumbukumbu zinaonesha kwamba Idd Masasi alishawahi kuhukumiwa kufungwa miaka 30 kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha mwaka 2011 na kutumikia adhabu hiyo katika gereza la Butimba Mwanza na baadae alitoka kwa rufaa.

Amesema baanda ya Jeshi la polisi Shinyanga kupata taarifa hizo kwa kushirikiana na kikosi kazi cha askari polisi kutoka Dar es salaam, liliweka mtego maeneo ya Soko la Nguzo Nane na ilipofika majira ya saa tano asubuhi Mei 30,2021 Idd Masasi alifika maeneo hayo.

“Hata hivyo kikosi kabambe cha askari polisi wenye weledi mkubwa walikuwa tayari wameshamuona jambazi huyo na alipogundua kuwa anafuatiliwa jambazi huyo alianza kukimbia ndipo askari polisi walipompa ilani ya kusimama kwa kufyatua risasi hewani lakini hakusimama hivyo askari waliamua kumfyatulia risasi mbili kwa weledi wa hali ya juu bila kuleta madhara kwa watu wengine waliokuwepo eneo hilo”,

“Risasi hizo zilimjeruhi jambazi huyo mguu wa kushoto na sehemu ya mgongoni na hivyo kuweza kumkamata. Jambazi huyo alikimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu ya majeraha aliyoyapata na alifariki dunia wakati anapatiwa matibabu. Mwili wake umehifadhiwa hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi”,amefafanua Kamanda Magiligimba.

Kamanda Magiligimba ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la polisi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili mkoa wa Shinyanga uendelee kuwa salama.

“Natoa onyo kali kwa wahalifu wote kuwa mkoa wa Shinyanga siyo sehemu rafiki ya kutenda uhalifu au kukimbilia wahalifu kujificha baada ya kufanya uhalifu mikoa mingine kwani jeshi la polisi limejipanga vizuri kukabiliana nao”,amesema Kamanda Magiligimba.

“Mhalifu yeyote atakayethubutu kufanya uhalifu atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Wahalifu wote wafahamu kwamba sehemu ambayo wapo na sisi jeshi la polisi tupo”,ameongeza Kamanda Magiligimba.

Share:

Ajenda Kuu Ya Serikali Ni Kujitegemea Katika Uzalishaji Mbegu-waziri Mkenda


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha
Katika kuendeleza ushirikiano na Sekta binafsi, ambalo ni jukumu la kisheria la Serikali kuhamasisha sekta binafsi katika uzalishaji wa Mbegu Bora, Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda katika ziara yake Jijini Arusha, leo tarehe 30 Mei 2021 ametembelea moja ya kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO

Waziri Mkenda pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao wa Wizara ya Kilimo Ndg Nyasebwa Chimagu wamepata fursa ya kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kampuni hiyo binafsi hasa katika suala zima la uchakataji na utunzaji wa Mbegu Bora unavyofanywa na kampuni hiyo kutoka hatua za awali Mbegu zinapotoka shambani, zinapopokelewa, kuchakatwa, kupimwa na kupakiwa tayari kwa kumfikia mkulima.

Katika ziara hiyo Waziri Mkenda amesema kuwa moja ya ajenda kuu ya Wizara ya Kilimo ni kuhakikisha nchi inazalisha mbegu za kutosha za kilimo kupitia sekta binafsi kadhalika Mamlaka ya Mbegu ya Serikali (ASA) ili kufikia hatua ya kujitosheleza katika uzalishaji mbegu na kuanza kuuza nje ya nchi.

Amesema kuwa serikali inahimiza Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) pamoja na Taasisi zote zinazojihusisha na utafiti hususani wa mbegu kuhakikisha kuwa zinazendelea kufanya utafiti wa mbegu bora na zitakazo ongeza tija katika kilimo.

“Tunataka mtu aweze kuzalisha kiasi kikubwa zaidi kwa Hekari moja ili nguvu ya mkulima iwe inazaa matunda makubwa na vilevile itatusaidia sana kwenye masoko kwa sababu ukizalisha kwa wingi hata kama bei ya mazao imeshuka lakini kipato kinakuwa kikubwa” Amekaririwa Prof Mkenda

Waziri Mkenda amesema kuwa pamoja na juhudi za serikali za kutumia taasisi ya utafiti (TARI) na mamlaka ya Mbegu (ASA) ambayo ina kazi ya kuchukua mbegu bora na kuzalisha kwa wingi ili kuzipeleka kwa mkulima lakini pia serikali inafanya kazi kwa karibu na sekta binafsi ikiwemo kampuni ya mbegu ya SEED.CO

Prof Mkenda ameipongeza kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO kutokana na uzalishaji wa mbegu bora ambazo zimekuwa na matokeo mazuri kwa wakulima ambapo amewahakikishia hitaji lao kubwa la kukodi mashamba ya serikali kwa ajili ya uzalishaji mbegu bora linafanyiwa kazi kwa haraka iwezekanavyo.

“Lakini nimewaahidi endapo watajenga maabara kubwa ya kisasa kwa ajili ya shughuli za mbegu hapa Tanzania, nitajitahidi kuhakikisha kuwa wanapata mashamba makubwa angalau mawili kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mbegu” Amesema Mkenda

Amewasihi kuongeza zaidi uzalishaji wa mbegu ikiwa ni pamoja na kuanzisha uzalishaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali badala ya Nafaka na Mbogamboga pekee, Kwa kufanya hivyo kutakuwa na uwezekano wa kuongeza mbegu bora na zenye tija kwa wakulima nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mbegu (TASTA) Ndg Bob Shuma amepongeza Serikali kwa kuamua kulichukulia kwa msisitizo swala la uzalishaji wa mbegu bora nchini ambapo ameeleza furaha yake na kumuhakikishia Waziri wa Kilimo kuwa umoja huo unaendelea na mkakati madhubuti katika uzalishaji wa mbegu bora na kwa wingi.

Hata hivyo amerejea msisitizo wa Waziri wa Kilimo kuyaomba mashirika mengine nchini na nje ya nchi kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya mbegu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa karibu na serikali kupitia taasisi ya TARI na ASA ili kuongeza ufanisi katika sekta ya mbegu.


Share:

BABA MTAKATIFU FRANSISCO AMTEUA MSIMBE KUWA ASKOFU JIMBO LA MOROGORO



 

Share:

SHINDANO LA MISS KAHAMA KUFANYIKA JUMAMOSI HII JUNI 5

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha (wa tano kulia)  akiwa na mwaandaaji wa Mashindano ya Miss Kahama, Peter  Frank Alex pamoja na baadhi ya washiriki wa shindano la Miss Kahama 2021
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shindano la Urembo kutafuta mlimbwende wa Kahama ‘Miss Kahama 2021’ yanatarajia kufanyika Jumamosi hii June 5,2021 katika ukumbi wa African Lounge Mjini Kahama yakishirikisha warembo 12 huku Msanii Mr. Blue akinogesha mashindano hayo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Br.Black Social Partners ambao ni waandaaji wa Shindano la Urembo la Miss Kahama, Peter Frank Alex amesema maandalizi ya shindano hilo yamekamilika.

Amesema shindano la Miss Kahama litafanyika Jumamosi hii June 5, 2021 African Lounge. Washiriki wapo 12 ambao ni mabinti warembo kutoka Kahama ambao sasa wapo kambini wanaendelea na mazoezi.

“Maandalizi ya shindano la Miss Kahama ni makubwa hivyo wananchi wategemee mambo makubwa siku hiyo kuanzia saa moja usiku. Tiketi zinaendelea kutolewa maeneo mbalimbali ikiwemo Huheso FM kwa Zakazi, BSL College, African Lounge na tunasambaza mtaa kwa mtaa na siku ya shindano tiketi zitapatikana getini”,amesema.

Share:

OSHA YAZINDUA MPANGO WA KUSAJILI NA KUKAGUA MAENEO YA WAJASIRIAMALI WADOGO


Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza kutoka OSHA, Moteswa Meda, akionyesha namna ya kumhudumia mfanyakazi aliyezimia katika eneo la kazi wakati wa mafunzo ya usalama na afya yaliyotolewa na OSHA kwa wajasiriamali wadogo walioshiriki maonesho katika kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, akisaini kitabu cha wageni katika banda la OSHA alipotembelea banda hilo wakati wa maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji katika kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi Kahama. Pembeni yake ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda.
Afisa Usajili wa OSHA, Glory Bonventure, akiwaongoza wajasiriamali wadogo kusajili maeneo yao ya kazi kupitia mtandao wa WIMS (Workplace Information Management System) wakati wa maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama.
Afisa Usajili wa OSHA, Glory Bonventure, akiwaongoza wajasiriamali wadogo kusajili maeneo yao ya kazi kupitia mtandao wa WIMS (Workplace Information Management System) wakati wa maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama.
Baadhi ya washiriki wa maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji wakifuatilia mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa na OSHA wakati wa maonesho hayo.
***

 Na Mwandishi Wetu

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umezindua mpango maalum wa kuwasajili na kuwahudumia wajasiriamali wadogo kupitia ukaguzi wa sehemu za kazi, kuwapa mafunzo na ushauri wa kitaalam kuhusiana na masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.

Mpango huo umezinduliwa rasmi katika maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji yaliyohitimishwa mwishoni mwa wiki katika kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi mjini Kahama mkoani Shinyanga.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema mpango huo mahsusi umeandaliwa na Taasisi yake baada ya kuendesha programu ya mafunzo kwa wajasiriamali wadogo kwa miaka mitano na kubainisha ombwe katika usimamizi wa usalama na afya miongoni mwa kundi hilo muhimu. 

“Tumekuwa na programu ya mafunzo kwa wajasiriamali wadogo kwa zaidi ya miaka mitano lakini hivi karibuni tulifanya tathmini ya mpango husika na tukabaini kwamba tunahitaji kuwa na utaratibu mzuri na rahisi zaidi kwa ajili ya kundi la wajasiriamali wadogo kuweza kukidhi viwango vya usalama na afya mahali pa kazi. Hivyo, tukaone tutengeneza mfumo wa kieletroniki utakaotuwezesha kuwasajili na kisha kuwafikia katika maeneo yao ili kuwaelimisha pamoja na kushauri namna bora ya kuboresha mazingira yao ya kazi,” alisema Mwenda.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania ambao ndio waratibu wa maonesho hayo kwa kushirikiana na kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi Kahama, Fatma Kange, amesema Taasisi yake inashirikiana na OSHA katika kuwawezesha wajasiriamali kukuza biashara zao pamoja na kuwapa miongozo ya kuboresha mazingira yao ya kazi. 

“Miaka kumi ijayo tunaanza kazi na OSHA na ndio maana unaona katika maonesho haya OSHA amekuwa mdhamini muhimu sana kwa lengo la kuja kuelimisha wajasiriamali wetu ili wafanye uzalishaji kwa kuzingatia afya na usalama wao. Kama tunavyofahamu OSHA wana wajibu mkubwa wa kulinda rasilimali uhai na afya ya kila mtanzania. Hivyo, tunataka wazalishaji wetu watambue nafasi ya afya katika shughuli zao za kila siku” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania",alisema.

Baadhi ya wajasiriamali walioshiriki katika maonesho hayo na kupata fursa ya kusajili maeneo yao ya kazi pamoja na kupatiwa mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi wameeleza jinsi walivyoupokea mpango huo pamoja na mafunzo waliyoyapata.

“Kupitia maonesho haya kuna mafunzo mbali mbali na miongoni mwa mafunzo hayo ni mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa na OSHA. Kwakweli mafunzo haya nimeyafurahia sana kwasababu yametupatia nyenzo za kujikinga zaidi katika kazi zetu ili kujiepusha na madhara tunayoweza kuyapata tukiwa kazini au baada ya kustaafu,” alisema Amina Madeleka, Mjasiriamali aliyeshiriki maonesho na mafunzo yaliyotolewa na OSHA.

OSHA ni taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambayo husimamia utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003. Majukumu yake ya msingi ni pamoja na kusajili maeneo ya kazi, kufanya kaguzi za usalama na afya mahali pa kazi, kuchunguza afya za wafanyakazi, kufanya tafiti na kuishauri serikali kuhusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi. 


Share:

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA USHIRIKIANO WA ELIMU DUNIANI (GPE)

Bodi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) imemkaribisha Rais mstaafu wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete kuwa Mwenyekiti mteule wa Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Shule ya Uchumi na Sayansi ya Siasa ya London, Dk. San Liautaud kuwa, Makamu Mwenyekiti mteule.

Dk. Kikwete na Makamu wake wanatarajia kuanza kutekeleza rasmi majukumua yao Septemba 15, 2021.

Uthibitisho wa Dk. Kikwete umeonyesha umuhimu ambao GPE inaweka juu ya uongozi wa nchi washirika na ushiriki.
Katika kipindi chote cha utumishi wa Dk Kikwete, katika serikali ya Tanzania na mashirika ya kimataifa na ya kikanda, alijitolea kuendeleza sera zinazoendelea za elimu na afya ya wanawake na watoto.

Mwenyekiti wa Bodi ya GPE na Waziri Mkuu wa zamani wa Australia Julia Gillard amewakaribisha viongozi hao wawili na kueleza namna alivyofurahishwa na uteuzi wao.

"Nimefurahi kuwakaribisha Dk. Jakaya Kikwete na Dk. Susan Liautaud sote tunafahamu kuwa Dk. Kikwete ni kiongozi anayeheshimika juu ya elimu na afya ya umma barani Afrika na kwingineko, ambaye uzoefu na taaluma yake ya utumishi wa umma itasimamia kazi ya GPE katika miaka ijayo lakini pia ustadi mkubwa wa Dk. Liautaud katika utawala na maadili utaimarisha mfano wa ushirikiano wa GPE kwa faida ya mamilioni ya watoto ulimwenguni, " amesema.

Kwa upande wake Dk. Kikwete amesema, “Ninaamini hakuna mabadiliko makubwa zaidi ambayo kiongozi anaweza kufanya ili kutumikia watoto walio katika mazingira magumu na waliotengwa zaidi ya elimu. Nimeheshimiwa kuongoza Bodi ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Elimu, shirika ambalo linajishughulisha na kushughulikia shida ya kujifunza ambayo imezidishwa na janga la corona," amesema Kikwete.

Naye Makamu Mwenyekiti mteule wa bodi hiyo, Susan Liautaud amesema "Elimu ni ufunguo wa kutatua changamoto nyingi sana ulimwenguni kutoka kwenye haki za binadamu na afya hadi kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kutokomeza viwango visivyokubalika vya ukosefu wa usawa ulimwenguni.

Nimeheshimiwa kuchukua jukumu hili la Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya GPE," amesema.
Share:

SHAMBA LENYE EKARI 100 LINAUZWA,LIMEPIMWA


Shamba lenye Ekari 100 ambalo tayari limeishapimwa linauzwa .

Mahali: Shungumbweni, Mkuranga karibu na Kiwanda cha Chumvi Neel Salt

Bei: Mil.150,000,000 (mazungumzo yapo) .

Umbali: Kilomita 5 kutoka baharini, Kilomita 26 kutoka barabara kuu ya Dar-Lindi, (Unaweza Ingilia kwa njia ya Kibada-Mwasonga pia).

Shamba lina miti ya mikorosho na mianzi,kisima cha maji safi mita 72, kinatoa lita 20,000 kwa saa.

KWA MAWASILIANO ZAIDI 0763000053


Share:

WASH Specialist, NOD, FT at UNICEF

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job no: 535233 Contract type: Fixed Term Appointment Level: NO-4 Location: Tanzania,Uni.Re Categories: WASH (Water, Sanitation and Hygiene), NO-4 UNICEF works in some of the world’s toughest places, to reach the world’s most disadvantaged children in order to save their lives, defend their rights and to help them fulfill their potential. Across 190 countries and territories, we work for every […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

CAMILIUS WAMBURA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI (DCI)


CP Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) mteule
 **
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amempandisha cheo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Camilius Wambura, na kuwa Kamishna wa Polisi (CP) ambapo pia amemteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, na kueleza kuwa uteuzi huo umeanza jana Mei 30, 2021.

Mei 17, 2021, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, alimhamisha Wambura kutoka kuwa 'Chief of Operations Upel' kuu Dodoma na kumhamishia Dar es Salaam kuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum akichukua nafasi ya SACP Lazaro Mambosasa.
Share:

Regulatory Compliance Specialist at Vodacom

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

At Vodacom, we’re working hard to build a better future. A more connected, inclusive and sustainable world. As a dynamic global community, it’s our human spirit, together with technology, that empowers us to achieve this. We challenge and innovate in order to connect people, businesses, and communities across the world. Delighting our customers and earning […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Assistant Facilities Supervisor at International School Of Tanganyika

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Title Assistant Facilities Supervisor Reports to: Facilities/Site Supervisor Department: Operations Start date: June, 2021 IST Foundational Documents IST Mission Challenging, inspiring and supporting all our students to fulfil their potential and improve the world IST Vision IST will be a global leader in the education of internationally-mobile young people. All students, regardless of their starting […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Library Assistant at International School Of Tanganyika

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Title Library  Assistant Category   (cf Policy 5.101) Teaching Assistance Reports to: Elementary School Principal    Department: Elementary School Job Holder     Start date: 1 August 2021   IST Foundational Documents IST Mission Challenging, inspiring and supporting all our students to fulfill their potential and improve the world IST Vision IST will be a global […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Regional Managing Director at Nature Conservancy

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

A LITTLE ABOUT US Founded in 1951, the Nature Conservancy (TNC) is a global conservation organization dedicated to conserving the lands and waters on which all life depends. Guided by science, we create innovative, on-the-ground and scalable solutions to our world’s toughest challenges so that nature and people can thrive together. This decade is critical […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

KONGAMANO WOMEN'S FOR CHANGE LATIKISA SHINYANGA ANTI SADAKA, MAHIBA, PASTOR MGOGO WATEMA CHECHE

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, na Mwenyekiti wa Chama cha Women's For Change, Getrude (kushoto) wakikata Keki kufungua Kongamano la Wanawake Mkoani Shinyanga (Shy Women's Day Out)

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Kongamano la Chama Cha Wanawake mkoani Shinyanga, Women's For Change' Shy Women's Day Out'  limefanyika mjini Shinyanga kwa kukutanisha wanawake, kubadilishana mawazo pamoja na kupewa masomo mbalimbali ya kuwajenga.

Kongamano hilo limefanyika Mei 30,2021 katika ukumbi wa mikutano wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa  Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga  Mhe. Hoja Mahiba.

Aidha kwenye Kongamano hilo, watoa mada za kuwajenga wanawake, alikuwa mama Edina Shoo, Khadija Liganga, Dkt. Mfaume Salum, Sadaka Gandi (Anti Sadaka) pamoja na Pastor Daniel Mgogo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, watoa mada hao wamewataka wanawake kujiamini, wajitambue,kupendana, kushikamana, pamoja na kujituma kufanya kazi ili wasiwe tegemezi kutoka kwa waume zao.

Akitoa mada kwenye Kongamano hilo Anti Sadaka, amewataka wanawake wasiwe watumwa wa fikra, na wasishindane na mtu, bali washindane na nafsi zao ndipo watapata kufanikiwa.

Naye mtoa mada Khadija Liganga ,amesema nguvu ya mwanamke ipo kwa mwanamke mwenzake ,hivyo ni vyema washikamane na kushirikiana katika nyanja mbalimbali katika mapambano ya kimaisha.

Mtoa mada mwingine Edna Shoo, amewataka wanawake pale wanapokumbana na matatizo au changamoto mbalimbali, wazipokee pamoja na kuzitafutia ufumbuzi na wasiwe wepesi wa kukata tamaa.

Mchungaji Daniel Mgogo 'Pastor Mgogo' akitoa mada kwenye Kongamano hilo, amewapongeza wanawake kwa kuanza kupendana, kuinuana, kujishughulisha, pamoja na kushikamana, tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa na hali mbaya.

"Nawapongeza wanawake kwa kuanza kubadilika na muendelee kupendana na msirudi nyuma, mkichukiana ni furaha kwetu sisi wanaume, kwani mtakwama mambo yenu na tutaendelea kuwatalawa,"amesema Mgogo.

Pia Mchungaji Mgogo, amewataka wanawake ambao wamefanikiwa kimaisha wasiwadharau waume zao, pamoja na kuwanyanyasa, bali wawatunze na kuwahudumia kwa kila kitu ikiwamo kuwanunulia mavazi.

Aidha Dkt. Mfaume Salum ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa Shinyanga, amewataka akina mama hao, licha ya kujituma katika shughuli za kiuchumi, wasisahau pia kupima afya zao hasa Saratani ya mlango wa Shingo ya kizazi, ambapo wakiiwahi inatibika.

Kwa upande wake mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, amewataka wapinge masuala ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii, pamoja na kuzingatia malezi bora kwa watoto wao.

Katika hatua nyingine Mahiba amewataka wanawake mkoani Shinyanga, wachangamkie mikopo ya Halmashauri asilimia 4 ambayo hutolewa kwa wanawake na haina riba, ili wapate mitaji na kufanya shughuli za kuwainua kiuchumi.

Mwenyekiti wa chama cha wanawake mkoani Shinyanga Women's For Change Getrude Munuo, akisoma risala amesema wapo wanachana 20, na walikianzisha mwaka 2013 na kusajiliwa rasmi mwaka 2014.

Amesema kazi kubwa ambayo wanazifanya ni kusaidiana, na kusaidia pia watu wenye uhitaji zikiwamo na shughuli zingine za kijamii, ambapo mwaka huu wametoa msaada wa madawati katika Shule ya Sekondari Salawe, na kukarabati vyoo Kambi ya wazee Usanda wilayani Shinyanga.

Wadau waliofadhili Kongamano hilo NMB, NBC, CRDB, Tpb bank, Jambo, Shuwasa, Omyfashion, Shybest, Lulekia, Gvenwear, Fresho, Vai Saloon, Nuru Fashion, Wine Keki, Bomba Security, Tahosa Stationary.

Wadau wengine ni Little Treasure, chuo cha afya Kolandoto, Sene Open Bussnes, Virgmark na Kalena Hotel, Love Decoration,Vivak Investment, VRK Trader,Kanvolpics, Diamond Autolink, VIHAS, fk , Manka Electronics, Vihas, na Vanson Microfinance.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akizungumza kwenye Kongamano la wanawake mkoani Shinyanga, Women's For Change.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akina mama kutoka Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga Dkt Mfaume Salum, akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake..
Pastor Daniel Mgogo akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Anti Sadaka, akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Mama Shoo akitoa Mada kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Khadija Liganga akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Mwenyekiti wa Chama cha Women's For Change Getrude Munuo, akizungumza kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Mwenyekiti wa Kongamano hilo Faustina Kifambe, akizungumza kwenye Kongamano hilo la wanawake Shy Women's Day Out.
Wanachama wa Women's For Change wakiwa kwenye Kongamano la Shy Women's Day Out.
Wanawake wakiwa kwenye Kongamano la Shy Women's day Out.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Awali Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Women's For Change,Getrude wakikata Keki kufungua Kongamano la Wanawake, Shy Women's day Out.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akitoa vyeti kwa wadau ambao wamefadhili Kongamano hilo la wanawake, "Women's day Out" lililoandaliwa na Chama cha Women's For Change.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
 
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Burudani zikitolewa kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Burudani zikiendelea kutolewa.
Wanachama wa Women's For Change wakipiga picha ya Pamoja na watoa mada kwenye Kongamano la Wanawake Mkoani Shinyanga( Shy Women's Day Out), pamoja na Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba.
Wafadhili wa Kongamano hilo la Wanawake wakipiga picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi pamoja na watoa mada.
Picha za pamoja zikipigwa kwenye Zuria Jekundu na watoa mada kabala ya kuanza Kongamano la wanawake "Shy Women's day Out"
Wanachama wa Womens' For Change, wakipiga picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, wapili kutoka Kulia.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger