Friday 31 July 2020

MWANAMKE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUWANYANYASA KINGONO WATOTO 7 WA KIKE


Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Irene James mwenye umri wa miaka 36 amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Tabora akituhumiwa kuwafanyia unyanyasaji wa kingono Watoto saba wa kike  jirani zake wenye umri kati ya miaka 4 hadi 7 kwa kuwaingizia vidole sehemu za siri.

Akisoma maelezo ya kosa jana Julai 30,2020 Wakili upande wa Jamhuri Gladness Senya ameieleza mahakama kwamba mtuhumiwa anadaiwa kutenda makosa hayo saba ya udhalilishaji wa kingono wa hali ya juu kinyume cha kifungu cha 138 C (1) (a)na kifungu kidogo cha 2(b) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019,Kitendo ambacho amekifanya kwa Watoto hao saba ambao majina yao yamehifadhiwa.

Mbele ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora John Mdoe Wakili huyo wa Jamhuri Gladness Senya alidai kuwa mtuhumiwa aliwatendea makosa hayo watoto hao saba wa majirani zake kwa nyakati tofauti majira ya mchana terehe zisizojulikana kati ya mwezi Januari hadi Julai mwaka huu huko katika Kata ya Kanyenye manispaa ya Tabora.

Hata hivyo mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora imemnyima dhamana mshitakiwa huyo kwa madai ya usalama wake na kwamba amepelekwa mahabusu mpaka pale kesi hiyo itakapotanjwa tena tarehe 13 mwezi Agust.
Share:

SWALA YA EID AL - ADHA YAFANYIKA MSIKITI WA TAWQWA KIOMBOI SINGIDA...WATANZANIA WASISITIZWA AMANI KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI


Na Ismaily Luhamba,Singida.

Waislam mkoani Singida leo wameungana na Waislam wenzao Duniani kutimiza Nguzo ya Tano ya Uislamu ya Sala ya Eid Al Adha ambapo swala hiyo mkoani Singida imefanyika kimkoa Wilayani Iramba kwenye Msikiti wa Tawqwa mjini Kiomboi.

Swala hiyo iliongozwa na Kadhi wa mkoa, Sheikh Ramadhani Kahoja.

Akisoma Khutuba, Mwandishi Maalum wa Mufti wa Tanzania Sheikh Harith Othman Nkusa atoa rai watu wapendanae hasa katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu ili nchi iweze kuvuka salama kama tulivyo weza kuvuka salama kwenye  Janga la Corona.

"Pia Waumini na Wananchi tuwe watiifu kwa Viongozi wetu wa Serikali na wa dini zetu kwani kuwa Mtiifu sio utumwa ila ni kufuata sheria na kupenda Nchi yako.  Sisi ndiyo tunaoweza kuijenga hii nchi na sisi pia tunaweza kuibomoa. Ndio maana nasisitiza utiifu kwa Waumini na wananchi kwa ujumla", alisema  Sheikh Othman.

Naye, Katibu wa Bakwata mkoa wa Singida,  Alhaji Burhani Mlau  ametoa pole kwa Taifa kutokana na kifo cha Rais Mstaafu awamu ya tatu,  Benjamin Mkapa aliyezikwa kijijini kwake,  Lupaso wilayani Masasi mkoani Mtwara Jumatano hii.

"Kupitia swala hii ya Idd, napenda kusema tunakwenda kwenye Uchaguzi Mkuu wa nchi, sisi kama viongozi wa dini tuwe karibu sana na waumini wetu kwa kuwajenga kiimani na kuliombea Taifa letu ili liweze kuvuka salama kwenye uchaguzi huu" alisema Burhani.


Share:

Video Mpya : NYANDA MAYEBELE - DUNIA

Msanii wa Nyimbo za Asili Nyanda Mayebele anakualika Kutazama Video ya Wimbo wake Mpya unaitwa Dunia.
Tazama Hapa chini
Share:

RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA KIKWETE AONGOZA SWALA YA EID EL-ADHA KIMKOA LINDI


Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya waumini wa dini ya Kiislam katika swala ya Eid Al-Adha Kimkoa iliyoswaliwa leo katika uwanja wa Ilulu Lindi mjini. Dkt Kikwete ameongozana na mke wake Mama Salma Kikwete.
Share:

Picha: SWALA YA EID EL - ADHA YAFANYA UWANJA WA SABASABA SHINYANGA MJINI...SHEIKH BALISUSA ATAKA AMANI ITAWALE UCHAGUZI MKUU


Na Marco Maduhu - Shinyanga
Shekh Balilusa Khamisi wa mjini Shinyanga, amewataka viongozi wa vyama mbalimbali vya kisiasa hapa nchini pamoja na wanachama wao, kudumisha amani katika uchaguzi mkuu, utakaofanyika Oktoba mwaka huu wa kuchagua madiwani, wabunge na Rais.

Amebainisha hayo leo mara baada ya kumaliza kuongoza  swala ya Eid El-Adha iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Shinyanga, kuwa matarajio ya viongozi wa dini ni kuona uchaguzi mkuu unakuwa tulivu na amani, na kusiwapo vurugu zozote zile za uvunjifu wa amani.

Sheikh Khamisi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamti ya amani mkoa wa Shinyanga, amesema viongozi wa siasa pamoja na wanachama wao, wanapaswa kutanguliza maslahi ya taifa mbele na siyo maslahi yao binafsi katika kipindi cha uchaguzi mkuu, na kutofanya vurugu ambazo zitavunja amani ya nchi na kuingia kwenye machafuko.

“Sisi kama viongozi wa dini tunawaomba sana viongozi wa kisiasa hapa nchi pamoja na wanachama wao, katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, watangulize maslahi ya taifa na siyo maslahi yao binafsi, ili kulinda amani ya nchi yetu na kutofanya vurugu zozote kwenye uchaguzi,” amesema Sheikh Khamisi.

Katika hatua nyingine amewataka wakuu wote wa shule binafsi kutowanyima wanafunzi muda wa kwenda kuswali masomo ya dini, kwa madai ya kufidishia muda uliopotea wakati wa kipindi cha likizo ya Corona, bali wawaruhusu ili wapate masomo hayo ya kiimani ambayo yatawajenga kimaadili.

Naye mjumbe wa baraza la Masheikh mjini Shinyanga Shekh Khalfan Ally, akitoa mawaidha amewataka waumini wa dini hiyo ya kiislam hasa vijana, kuzingatia miiko na sheria ya dini hiyo ili kutoporomoka kimaadili, pamoja na kuacha kuzaa watoto kabla ya kufunga ndoa na kutolelewa na majimama.

Aidha amesema baadhi ya vijana wa dini hiyo hawana maadili kabisa, ambapo wamekuwa wakifanya uzinzi na kuzaa watoto nje ya ndoa, kutovaa mavazi ya heshima, kunyoa mitindo ya nywele, pamoja na kupenda mteremko na kwenda kuoa wanawake wenye pesa bila hata ya kujali tabia zao wala umri bali wao wanajali pesa tu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Sheikh Balilusa Khamis akizungumza mara baada ya kumaliza kuongoza swala ya Eid El-Adha  katika uwanja wa Sabasaba mjini Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog

Mjumbe wa Baraza la Mashekh mjini Shinyanga Shekh Khalfan Ally, akitoa mawaiza kwenye swala ya Eid El-Adha 

Shekh Balilusa Khamisi akiongoza maombi kwenye ibada ya Eid Al Adha kwenye uwanja wa uhuru mjini Shinyanga.

Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa kwenye swala ya Eid El-Adha  katika uwanja wa Sabasaba mjini Shinyanga.

Swala ikiendelea.

Swala ikiendelea.

Swala ikiendelea.



Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa kwenye  swala ya Eid El Adha.

Swala ikiendelea.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog

Share:

Magereza Yaruhusu Wananchi Kuanza Kutembelea Wafungwa

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
kufuatia kupungua kwa maambukizi ya virusi vya COVID 19 Jeshi la Magereza nchini limefuta masharti ya katazo la huduma ya kuwatembelea wafungwa na mahabusu na huduma mbalimbali katika magereza ikiwamo huduma ya chakula kwa mahabusu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma msemaji wa Jeshi la Magereza SSP Amina Kavirondo amesema kutokana na serikali kuruhusu shughuri mbalimbali kuendelea Jeshi la Magereza limeondoa katazo hilo kuanzia Augusti 1, 2020.

''Jeshi la magereza limelegeza masharti ya katazo kuanzia 01/08/2020 huduma za kuwatembelea wafungwa na mahabusu kwa huduma mbalimbali magerezani zimerejeshwa'' amesema Amina.

Aidha jeshi la Magereza limewataka wageni wote pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya jeshi na Wizara ya Afya wakati wa upokeaji wa huduma hiyo wageni watatakiwa mambo ikiwamo mfungwa au mahabusu atatembelewa na ndugu wasiozidi wawili kwa siku za jumamosi na jumapili.

Pia limebainisha kuwa mazungumzo yatatakiwa kuto zidi dakika tano na wale wenye vibali vya kuleta chakula italazimika kuletwa na mtu mmoja tu, pia mgeni atatakiwa kukaa umbali wa mita moja kati ya mfungwa au mahabusu huku wakitakiwa kuvaa barakoa na kunawa kwa maji tiririka huku likibainisha kuwa mazungumzo ya kisheria kati ya wakili na mteja wake yasizidi saa moja.

Aidha amebainisha kuwa kwa kipindi ambacho jeshi liliweka katazo hilo wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ikiwamo baadhi ya wafungwa kukosa haki zao ambazo zilikuwa zinahatarisha au kusababisha kusambaa kwa virus vya corona katika magereza lakini wamekuwa wakiwaelimisha lengo la kufanya hivyo.


Share:

Jeshi La Polisi Dar Lauwa Majambazi Watatu

JESHI la Polisi  Kanda Maalum  Dar es Salaam limewaua majambazi watatu na kukamata silaha mbili aina ya Short Gun Pump Action na Bastola aina ya Browning.

Mnamo tarehe 26.07.2020 majira ya saa mbili usiku  Jeshi la Polisi Kanda Maalum lilipata taarifa kuwa huko maeneo ya Mbagala Chamanzi kuna gari lenye namba T 855 ATE aina ya Nissan X-Trail likiwa na watu wanne  wanaosadikiwa  kuwa ni majambazi wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu.

Baada ya kupata taarifa hizo kikosi kazi cha kupambana na ujambazi kiliweka   mtego  katika eneo hilo na baada  majambazi hao kuhisi wanafuatiliwa na Polisi ghafla   walianza kupiga risasi hovyo kwa hofu na ndipo askari wakaamua kujibu mapigo kwa kulishambulia gari la majambazi hao  na kufanikiwa  kuwaua papo hapo majambazi watatu na jambazi mmoja akafanikiwa kukimbia.

Askari walifanya upekuzi ndani ya gari la majambazi hao na kumkuta jambazi mmoja akiwa amevalia mavazi ya Jeshi la Polisi aina ya kombati za kijani (JUNGLE GREEN) na kofia aina ya bareti nyeusi ya Jeshi la Polisi, redio Call, Pingu, namba za gari T 832 DCW ambazo ndiyo namba halisi za usajili wa gari hilo na silaha mbili aina ya Short gun Pump Action ikiwa na risasi nne ndani ya magazine iliyofutwa namba na Bastola aina ya Browning iliyofutwa namba ikiwa na risasi nne ndani ya Magazine.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa majambazi hao walifanya matukio ya uhalifu Mkoa wa Pwani Wilaya ya Mkuranga maeneo ya Vikindu na Kisemvule ambapo mnamo tarehe 25/07/2020  majira ya saa mbili usiku majambazi hao walimteka na  kumpora mfanyabiashara wa UWAKALA wa Benki na Mitandao ya simu aliyefahamika kwa jina la  SALEHE  MASOUD kiasi cha Tsh 19,600,000/=  .

POLISI KANDA MAALUM KUIMARISHA ULINZI SIKUKUU YA EID EL-HAJJI.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa  kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi cha sikukuu ya Eid El-Hajji inayotarajiwa kuadhimishwa tarehe 31/07/2020.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawaasa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kusherehekea sikukuu  kwa amani na utulivu na kujiepusha  na vitendo vya uvunjifu wa sheria kwani tumejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za Ibada, fukwe za bahari na tunawatadharisha watembea kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani.

Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawaomba Wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu  kwani jukumu la kuzuia uhalifu ni la kila Mtanzania.
 
SACP- LAZARO B. MAMBOSASA,
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.
30/07/2020.              


Share:

Boti yazama Ziwa Tanganyika, yaua 10

Watu kumi wamekufa maji na wengine themanini na saba wameokolewa baada ya boti kuzama katika ziwa Tangayika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, – James Manyama amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika  kijiji cha Rufugu wilayani Uvinza na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dhoruba iliyotokana  na upepo mkali katika ziwa Tanganyika na kusababisha boti kupinduka na kuzama.

Aidha Kamanda Manyama amesema kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa boti hiyo ilikuwa na abiria tisini na saba.


Share:

Waziri Simbachawene Aitaka Polisi Kukaa Mguu Sawa Uchaguzi Mkuu, Aipongeza Rufiji Kusambaratisha Wahalifu

Na Mwandishi Wetu, MOHA, Rufiji.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amelitaka Jeshi la Polisi kudhibiti vurugu zozote au uvunjifu wa sheria hasa katika kipindi hiki nchi inapoelekea katika uchaguzi mkuu.

Amewataka muda wote wawe tayari kwa kujipange vizuri na pia intelejensia wahakikishe kila kinachotekea katika jamii wanakijua ili kuhakikisha nchi inakua salama na uchaguzi umalizike salama.

Akizungumza na Viongozi Wakuu wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Mjini Ikwiriri leo, wakati alipokuwa safarini akitokea Mkoani Mtwara kuelekea Jijini Dar es Salaam, Simbachawene amewataka Polisi wasije kujisahau na kudhani kuwa wapo salama sana bali muda wote wawe macho kujilinda, kulinda raia na mali zao.

“Msije mkajisahau mkadhani mpo salama sana, hawa watu huvamia pale mnapojisahau ndipo wanafanya hayo mambo. Tunapoelekea kipindi hiki cha uchaguzi  ni vizuri mkawa katika tahadhali, intelejensia ikae vizuri kuhakikisha kila kinachotokea kwenye jamii mnakijua,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa, “Mshirikiane na vyombo vingine kudhibiti uhalifu, Serikali ni moja, dola ni moja, Mamlaka ni moja na Amiri Jeshi Mkuu ni mmoja, kwahiyo pale mnapopungukiwa tumia taarifa kutoka kwa wenzenu.”

Pia Simbachawene alilitaka Jeshi hilo lithibiti matukio ya uhalifu kuanzia chini na pia wasilipuuze kwa kuwa tukio likidharauliwa ndipo baadaye linbakuja kuwa kubwa na kuleta matatizo makubwa katika jamii.

“Mdhibiti matukio kuanzia chini, utakuta tukio lina cheni fulani lakini halishughulikiwi, hivyo linazaa lingine na matokeo yake linakua kubwa zaidi, matukio yanayotokea yathibitiwe kwa kiasi cha kutosha ili yasije kuleta madhara makubwa hapo baadaye,” alisema Simbachawene.

Aidha, Waziri huyo aliahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji, ambapo atahakikisha anamfikishia ombi Rais Dkt. John Pombe Magufuli aweze kusaidia kuanza kwa ujenzi wa ofisi hiyo.

“Nitamuomba mheshimiwa Rais aone uharaka wa kutupa fedha ya ujenzi wa ofisi, ambayo ni shilingi milioni mia tatu, bila ofisi mnawezaje kufanya kazi, hatuwezi kuwaacha watu kwenye vijumba vyenye joto, itakua ni mateso, tutajitahidi tuweze kufanikisha hili kwa kulifanyia kazi kwa uharaka zaidi,” alisema Simbachawene.

Waziri huyo pia alimpongeza Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wa kipolisi pamoja na wasaidizi wake, kuhakikisha wanadhibiti uhalifu kwa kiasi kikubwa na sasa eneo hilo lina amani na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wa Kipolisi, SACP Onesmo Lyanga alisema Mkoa wa Kipolisi Rufiji hali ya usalama imeimarika na Wilaya zote nne za Kiserikali ambazo ni Rufiji, Kibiti, Mkuranga na Mafia zipo salama.

“Mkoa huu wa Kipolisi ulianzishwa mwaka 2017, na mpaka sasa, hali ya uhalifu ni shwari, tunaendelea kufanya misako na doria kupambana na uhalifu mdogo na mkubwa unaofanyika katika Mkoa wa Kipolisi Rufiji,” alisema Lyanga.

Pia Lyanga alimshukuru Waziri huyo kwa kuwatembelea, na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote aliyowapa, na wataendelea kufanya kazi kwa weledi muda wote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika Mkoa huo.


Share:

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mbeya

KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE] BILA KIBALI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia AMANI MPINDULE [68] Mkazi wa Lualaje kwa tuhuma za kumiliki silaha bunduki aina ya Gobole bila kuwa na kibali.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 25.07.2020 majira ya saa 15:00 Alasiri huko katika Hifadhi ya Mwenje – Ruaha iliyopo Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya katika msako wa pamoja kati ya Jeshi la Polisi na Askari wa TANAPA.

Mtuhumiwa alikutwa akiwa na:-
  1. Silaha [Gobole] isiyo kuwa na namba za usajili iliyotengenezwa kienyeji ambayo anaitumia kwa shughuli za uwindaji haramu,
  2.  Goroli tano [05],
  3.  Vipande vinne [04] vya nondo ambavyo hutumika kama risasi na
  4.   Unga wa baruti.
Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

KUKAMATA SILAHA BASTOLA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kukamata silaha bastola yenye namba ya usajili TGT.10582 / PT.809E aina ya TAURUS ikiwa na risasi moja ndani ya magazine iliyotengenezwa nchini Brazil.

Silaha hiyo ilikamatwa mnamo tarehe 25.07.2020 majira ya saa 19:30 Usiku huko Mtaa wa Maendeleo nyuma ya ofisi ya serikali ya Mtaa wa Iyela, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na kubaini mmiliki halali wa silaha hiyo.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI KWA NJIA YA MTANDAO.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewatia kumtia mbaroni watuhumiwa wanne 1. ISSA SAID [28] Mkazi wa Ilemi 2. JONATHANI FIKIRI TANGANYIKA [23] Mkazi wa Mwambenja 3. OBEDY MWASELELE [24] Mkazi wa Mwamfupe na 4. WILLIAM SALVATORY JONAS @ CHINA TZ [20] Mkazi wa Igoma “B” Jijini Mbeya kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwa njia ya mtandao.

Awali mnamo tarehe 24.07.2020 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipokea taarifa za siri toka kwa moja ya kampuni ya simu kuwa baadhi ya watumishi wake waliopo mkoani Mbeya ambao ni “Freelancer” wanaosajili laini za simu kwa mfumo wa kisasa kwa kutumia “Biometric Machine” kuwa wamekiuka taratibu za usajili wa laini za simu kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA].

Kufuatia taarifa hizo, ni kwamba mnamo tarehe 27.07.2020 majira ya saa 17:30 Jioni Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako katika maeneo ya Igodima, Iganzo, Ilemi na Isanga Jijini Mbeya na kufanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wanne na katika upekuzi uliofanyika walikutwa na vitu vifuatavyo:-

  1.     Biometric Machine Moja.
  2.     Simu Smartphone aina ya TECNO Camon inayotumika kusajilia laini.
  3.     Simu mbili Smartphone aina ya TECNO zinazotumika kufanya utapeli.
  4.     Laini 06 za Halotel.
  5.     Laini 11 za Vodacom.
  6.     Laini 01 ya Airtel.
  7.     Laini 48 za Airtel ambazo hazijatumika.
  8.     Laini 02 za Tigo.
  9.     Laini 02 za Zantel.
  10.     ICC ID Card 33 za Halotel.
  11.     ICC ID Card 46 za Vodacom.
  12.     ICC ID Card 17 za Tigo.
  13.     Daftari 02 zenye namba za NIDA za watu mbalimbali ambazo hutumika kufanya uhalifu wa kimtandao.
Watuhumiwa wamekiri kuwa baadhi ya laini huzitumia kufanya utapeli na uhalifu wa kimtandao kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno [SMS] kuhitaji kutumiwa pesa kwenye mitandao mingine “ILE PESA TUMA KWENYE NAMBA HII, JINA LITAKUJA…….”

Aidha watuhumiwa wamekiri kuuza laini hizo ambazo wamesajili kwa majina ya watu wengine kwa bei ya Shilingi 2,000/= kwa kila laini. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

WITO WA KAMANDA.
Ninatoa wito kwa wananchi kuwa makini pindi wanapofanya usajili wa laini zao za simu ili kuepuka kadi zao kutumika kusajili laini za watu wengine. Pia Jeshi la Polisi linasisitiza wananchi kuendelea kuhakiki usajili wa laini zao kwa kubonyeza *106#, kisha chagua namba 2, ingiza namba ya kitambulisho chako cha NIDA kisha utapata ujumbe utakaoonyesha orodha ya namba za simu zilizosajiliwa kwa kitambulisho chako.

Aidha natoa rai kwa makampuni ya simu kuajiri mawakala waaminifu ili kuepuka kuwasajilia watu laini kwa namba za vitambulisho visivyo kuwa vyao na kusababisha kuongezeka kwa wahalifu wa kimtandao na matapeli. Sambamba na hilo ninatoa wito kwa mamlaka husika kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya kielektroniki hasa simu za mkononi ili kuepuka utapeli na uhalifu wa kimtandao.

Pia ninawataka vijana kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato halali badala ya kujiingiza kwenye vitendo vya kihalifu ambavyo vitawasababisha kupata adhabu kali kwa mujibu wa sheria na kupoteza dira ya maisha yao.

Sambamba na hilo, nitumie fursa hii kuwatakia Waislamu wote na Watanzania kwa ujumla sikukuu njema ya EID AL-HAJI. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejipanga vizuri kuhakikisha ulinzi na usalama katika maeneo yote. Aidha wananchi wanakumbushwa kuzingatia usalama wao kwanza katika makazi yao, katika matumizi ya barabara na katika swala ya EID AL-HAJI itakayofanyika katika Misikiti mbalimbali.


Share:

Takukuru Manyara wamnasa Alute kwa kufanya biashara ya Mikopo Kitapeli akitumia jina la Halmashauri.

Na John Walter-Babati
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa  (TAKUKURU) mkoa wa Manyara inamshikilia mfanyabiashara Japhet Samwel Alute kwa kukwepa kulipa kodi ya serikali na kufanya biashara bila kuwa na leseni.

Mkuu wa Takukuru mkoani hapa Holle Makungu amesema kuwa mtu huyo pia anatoa mikopo umiza kwa wananchi kwa riba kubwa na kisha kuwadhulumu mali zao wanazoweka kama dhamana.

Makungu amesema kuwa Alute pia anawatishia wananchi wanaochelewa kufanya marejesho  kwa kutumia jina  la Halmashauri ya Mji wa Babati kwa kuwatumia ujumbe wa kuwauzia maeneo yao au nyumba walizoweka kama dhamana kwa mikopo umiza.

Amesema katika upekuzi walioufanya kwa mfanyabiashara huyo  wamekuta  mikataba ya kitapeli 99 ambayo inaonyesha ameuziwa maeneo mbalimbali zikiwemo nyumba na viwanja vya baadhi ya wananchi wa Mji wa Babati.

Aidha mtuhumiwa amekutwa akiwa na vitambulisho vya watumishi wa Umma na uraia wa Tanzania ambavyo si Mali yake.

Mkuu huyo  wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara Holle Makungu ametoa wito  kwa wote waliokumbana na mikopo hiyo umiza ya Alute au Mali zao kuchukuliwa kutokana na mikopo hiyo, wafike Ofisi za Takukuru Manyara Mtaa wa Miomboni mjini Babati siku ya Jumatatu Agosti 3,2020 ili Changamoto za mikopo umiza ziweze kupatiwa ufumbuzi.


Share:

BOTI YAUA WATU 10 KUJERUHI 100 BAADA YA KUGONGA MWAMBA ZIWA TANGANYIKA


Ziwa Tanganyika

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP James Manyama, amesema kuwa watu 10 wamefariki dunia huku wengine 100 wakiokolewa, baada ya Boti iliyokuwa ikitokea maeneo ya Sibosa kupigwa na dhoruba kisha kugonga mwamba na kupasuka ndani ya Ziwa Tanganyika.

Kamanda Manyama ametoa taarifa hiyo hii leo Julai 31, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ambapo amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana Julai 30 majira ya saa 5:00 Asubuhi.

"Boti iloikuwa na watu karibia 100, na ilipokuwa ndani ya maji ilikumbwa na dhoruba kali na kugonga mwamba kisha kupasuka, na watu takribani 100 wameokolewa na kusababisha vifo vya watu 10, Wanawake3, Mwanaume 1 na watoto 6, zoezi la uokoaji linaendelea leo tuna mashaka huenda kuna miili ndani ya maji" amesema Kamanda Manyama.

Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Uvinza Dkt Ruben Mwakilima, amesema kuwa miili imehifadhiwa katika Zahanati ya kalya na tayari miili ya watu wanne imekwishachukuliwa na ndugu zao.
Share:

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO

Zati 50
Full Power
Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.



FULL POWER



⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.



⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50


⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4


⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.



Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama



Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

AJALI YA BOTI ZIWA TANGANYIKA YAUA WATU 10

Na Mwajabu Kigaza, Kigoma

WATU 10 wamekufa kutokana na ajali ya boti iliyozama katika Ziwa Tanganyika kwenye eneo la kambi ya wavuvi makakara Kijiji cha Rufugu wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma ACP, James Manyama alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu jana alisema kuwa taarifa za awali zinaeleza kuwa watu sita wamekufa huku idadi kamili ya abiria waliokuwa katika boti hiyo haijulikani.

Baadhi ya mashuhuda na wakazi wa eneo hilo wakizungumza kwa njia ya simu akiwemo Juma Yakuti na Kaliya Kazibure wameeleza kuwa tukio hilo limetokea saa nne asubuhi ambapo boti hiyo lilikuwa likitoka Kijiji cha Sibwesa kuelekea Ikora mkoani Katavi.

Walisema chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na boti waliyopanda abiria hao kujaza watu kupita uwezo wa boti hiyo na hivyo kusababisha kuzama majini.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ameeleza kuwa taarifa zaidi juu ya tukio hilo zitaendelea kutolewa. Mwezi mmoja iliopita ajali kama hii ilitokea katika eneo la kijiji cha Simbwesa ambapo watu tisa walifariki kati ya abiria 60 waliokuwemo katika boti.

Share:

Waziri Wa Kilimo Atoa Siku 14 Kwa Mkurugenzi Wa Bodi Ya Nafaka Na Mazao Mchanganyiko Kukamilisha Malipo Ya Wakulima Wa Korosho

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ametoa siku 14 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko Dkt Anslem Moshi kukamilisha malipo ya wakulima wote waliouza korosho msimu wa mwaka 2018/2019.

Waziri Hasunga ametoa agizo hilo wakati alipotembelea na kukagua shughuli za utendaji kazi zinazofanywa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Jijini Arusha.

Amesema kuwa Bodi hiyo ilipewa dhamana la kununua korosho mwaka 2018 kwa niaba ya serikali na tayari serikali imeshatoa fedha zote kwa ajili ya wakulima lakini bado CPB haijakamilisha malipo hivyo ni lazima malipo yakamilike ndani ya siku hizo.

“Ndani ya siku 14 sitaki kusikia malalamiko ya wakulima lazima wakulima wote wawe wamelipwa fedha zao haraka iwezekanavyo” Alisisitiza

Katika ziara hiyo pia Waziri Hasunga amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko kuwasilisha haraka mpango kazi wa namna viwanda hivyo vitakavyofanya kazi kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zitakazohitajika na wateja na kukidhi matarajio ya serikali ikiwa ni pamoja na kuainisha idadi ya watumishi wanaohitajika.

Hasunga ameiagiza kampuni ya Monaban ambayo ilikuwa imekodisha kiwanda hicho kutekeleza maagizo ya serikali yaliyotolewa mwaka jana ya kuhamisha mali zao zote zilizopo katika eneo hilo la serikali kwani kesi mahakamani na notisi ilishaisha.

Akiwa kiwandani hapo Waziri Hasunga amebaini uchakavu wa mitambo iliyopo pamoja na uchache wa watumishi wanaofanya kazi katika kiwanda hicho hivyo ameagiza kufanyika ukarabati wa majengo hayo kuanzia mwezi Agosti badala ya Octoba kwa taasisi hiyo ilivyopanga.

“Tukisubiri mpaka mwezi wa kumi tutakuwa tumechelewa kwa kuwa mvua zitaanza kunyesha jambo ambalo litapelekea kushindikana kufanyika ukarabati” Amesema

Amesema kuwa Lengo la serikali ni kufufua viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao ya nafaka nchini ili kuzalisha bidhaa mbalimbali kama unga N,k na kuuza katika masoko ya ushindani ndani na nje ya nchi.

MWISHO


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa July 31





















Share:

Thursday 30 July 2020

Rais Magufuli Atengua na Kuteua Mkuu Mpya wa Wilaya ya Rufiji




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger