MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini Hamisi Mwinyuma alimaarufu Mwana FA amesema kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa kimemuumiza na ni pigo kubwa kwa wasanii kutokana na mchango wake wa kuanzisha Cosota.
Mwana FA aliyasema hayo leo wakati akizungumza katika wa ibada maalumu ya maombolezo iliyofanyika wilayani Muheza kwenye viwanja wa Jitegemee na kuongozwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo na wananchi wakiwemo viongozi wa dini.
Alisema kutokana na msiba huo mzito ndio maana akaamua kuungana na wananchi wa wilaya ya Muheza katika halfa hiyo kwa sababu katika kipindi chake ndio miongoni mwa taasisi aliyonzisha katika kusimamia haki za wasanii.
Msanii huyo alisema Cosota ni taasisi inayoshughuli na haki miliki za wasanii tokea ilipoanzishwa 1996 na imekuwa na mchango mkubwa kwani kabla ya hapo kazi za wasanii zilikuwa huwezi kumpeleeka mtu mahakamani.
Hata hivyo alisema kutokana na hilo wana mshukuru Hayati Mkapa kutokana na mambo makubwa aliyowafanyia wasanii hapa nchini ambayo yamekuwa na tija kubwa kwao .
0 comments:
Post a Comment