Thursday, 28 February 2019

Picha : MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU ALIVYOTUA KWA KISHINDO KISHAPU LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia wananchi waliokuja kumlaki wakati akiwasili kwenye mgodi wa Almasi Mwadui mkoani Shinyanga. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia wanafunzi waliokuja kumlaki wakati akiwasili kwenye mgodi wa Almasi Mwadui mkoani Shinyanga.
Meneja wa Huduma za Kiufundi wa Mgodi wa Williamson Diamond Richard Jumanne akimuonyesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan eneo ambalo uchimbaji wa almasi unafanyika katika mgodi huo uliopo Mwadui, Shinyanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiangalia shughuli ya uchambuaji wa almasi klatika mgodi wa Wiliamson Diamond Ltd, wengine pichani ni Naibu Waziri Madini Mhe. Stanslaus Nyongo (kushoto) na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelline Mabula pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara (kulia). Makamu wa Rais yupo mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiangalia shughuli ya uchambuaji wa almasi klatika mgodi wa Wiliamson Diamond Ltd, wengine pichani ni Naibu Waziri Madini Mhe. Stanslaus Nyongo (kushoto) na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelline Mabula pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara (kulia). Makamu wa Rais yupo mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi wa ujenzi wa maabara ya shule ya Sekondari Shinyanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga mara baada ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa maabara . 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga mara baada ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa maabara .
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Shinyanga wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye yup kwenye ziara ya kikazi mkoani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Kishapu kwenye uwanja wa mikutano Mhunze mkoani Shinyanga.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa Makamu wa Rais Mhunze, Kishapu mkoani Shinyanga. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Share:

MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA AUAWA KWA KUPIGWA NA MWALIMU

Picha haihusiani na habari hapa chini
Mwanafunzi mmoja wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Mikuyuni eneo la Kibwezi kaunti ya Makueni nchini Kenya kufariki dunia baada ya kupigwa na mwalimu. 

 Akidhibitisha kisa hicho, kamanda mkuu wa polisi kata ndogo ya Kibwezi Ben Chagulo alisema mwanafunzi huyo alikimbizwa katika hospitali ya AMREF lakini alifariki dunia kabla ya kuhudumiwa na madaktari. 

Kulingana na ripoti ya maafisa wa polisi mvulana huyo alifariki baada ya kuchapwa vibaya na mwalimu huyo.

Mamaake mwathiriwa Josephine Ndunge amesema kuwa alipokea habari za kifo cha mwanawe kupitia kwa mwalimu mmoja aliyempigia simu. 

"Nilipigwa simu na mmoja wa walimu aliyeniambia kuwa kijana wangu hajihisi vema baada kuadhibiwa na mwalimu. Nilifululiza hadi shuleni humo ambapo nilimpata mwanangu akivunja damu kwa wingi," Mamake marehemu alisema.

 Aidha, Chagulo alisema tayari uchunguzi umeanzishwa kufuatia kisa hicho na atatoa taarifa kamili. 

Mwalimu huyo aliyetambulikana kwa majina kama Stanley Kithyaka alikamatwa baada ya kutorokea mafichoni kwa saa chache na anashikiliwa katika kituo cha polisi cha kibwezi.

 Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi wafu cha hospitali ya Makindu ukisubiri kufanyiwa upasuaji kubaini chanzo cha kifo chake. 

Share:

BABU WA MIAKA 71 MWENYE WATOTO 11 AAMUA KUPANGA UZAZI KUPITIA NJIA YA UPASUAJI

Mwanaharakati mmoja  Rubaramira Ruranga mwenye umri wa miaka 71 kutoka Uganda na ambaye ni baba wa watoto 11 ameamua kupanga uzazi kupitia njia ya upasuaji ili kuzuia kuzaa watoto wengine.

Ruranga aliwataka wanandoa wachanga kupanga vema uzazi na kujadili idadi ya watoto wanaotaka kupata kabla ya kupitwa na wakati. 

Babu huyo alisema anajutia kuwa na mtoto wa miaka 2 kwa sasa kwani ingekuwa vema kwa angekuwa akiwalee wajukuu kulingana na umri wake. 

"Niliamua kupanga uzazi kupitia njia ya upasuaji ili nisiwe nikimtatiza mke wangu kila mara eti apange uzazi, yuko na miaka 41 na mimi niko na miaka 71, ningependa wanandoa kupanga uzazi kwa njia ifaayo na wajadiliane ni watoto wangapi wanaotaka kupata kulingana na uwezo wao wa kifedha, msizae watoto hadi uzeeni ambapo badala ya kulea wajukuu eti bado mnalea watoto wenu kama mimi hapa," Ruranga alisema. 


Ruranga alisisitiza kuwa upangaji uzazi kupitia njia ya upasuaji yaani vasectomy ni bora zaidi na wanaume wengi kutoka nchi za Afrika Kusini na Nambia wamekumbatia njia hii. 

 Hata hivyo, utafiti unaonyesha kuwa asilimia 0.1% peke ya Wakenya wamepanga uzazi kupitia njia hii. 
Share:

MSIBA WA RUGE WAKWAMISHA KESI YA HALIMA MDEE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha usikilizaji wa kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, kufuatia shahidi wa upande wa mashitaka kushindwa kufika mahakamani. 

Wakili wa Serikali, Ashura Mzava ameiambia mahakama kuwa shahidi huyo ameshindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi wake, kutokana na msiba wa bosi wake, Ruge Mutahaba. 

Shahidi aliyeshindwa kufika Mahakamani, ni Abdul Mchembea, mfanyakazi wa Clouds Media Group Limited (CMG). Amefiwa na bosi wake – mkurugenzi wa matangazo -aliyefariki dunia juzi tarehe 26 Februari 2019, nchini Afrika Kusini.

Taarifa zinasema, Ruge alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya ini na figo.

Kesi hiyo ambayo iko mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Hakimu Simba amesema, kutokana na dharura hiyo kesi imeahirishwa mapaka tarehe 21 Machi mwaka huu.

Mdee anadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 3 Julai 2017 akiwa makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Mdee anatuhumiwa kutamka maneno kuwa “anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afunge breki;” na kwamba kitendo hicho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Share:

MWILI WA RUGE KUWASILI KESHO SAA NANE MCHANA DAR


Mipango ya kuurejesha nchini mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba, imekamilika Afrika Kusini na mwili wake unatarajiwa kuwasili kesho majira ya saa 8:00 mchana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa familia Bw. Annick Kashaha amesema kuwa mara baada ya kuwasili mwili wa Ruge hapo kesho utapokelewa na kupelekwa katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhifadhiwa hadi Jumamosi.

Amesema kuwa mwili wa Ruge ambaye pia alikuwa moja ya muasisi wa Clouds Media Group, utaagwa Jumamosi majira ya saa tano katika eneo la Karimjee, ambapo wakazi wa Dar es Salaam watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.

Mwili wa Ruge aliyefariki dunia nchini Afrika Kusini juzi wakati akipatiwa matibabu ya figo utawasili mjini Bukoba kwa ndege Jumapili na maziko yake yatafanyika siku ya Jumatatu Kizuku Bukoba.
Share:

KABURI LA RUGE MUTAHABA LAANZA KUANDALIWA

Maandalizi ya kumzika marehemu Ruge Mutahaba katika kijiji cha Kiziru Wilaya ya Bukoba yamepamba moto na ujenzi wa kaburi umeanza leo.

Siperatus Mbeikya ambaye ni mmoja wa wanafamilia amesema taratibu zinaendelea ikiwa ni pamoja na kupokea wageni kutokana maeneo mbalimbali.

Pia, amesema maandalizi hayo yamekwenda sambamba na kukubaliana na kikosi cha usalama barabarani sehemu utakapopita msafara wenye mwili wa marehemu Ruge.

Pilikapilika zimeongezeka katika eneo la msiba ikiwa ni pamoja na kumwaga vifusi kwenye maeneo korofi.

Marehemu Ruge anatarajiwa kuzikwa Jumatatu, wakati mwili wake utawasili Dar es Salaam kesho Ijumaa na kuagwa Jumamosi.
Share:

Picha : SAVE THE CHILDREN YATAMBULISHA MRADI WA LISHE ENDELEVU DODOMA


Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Binilith Mahenge akizungumza wakati mradi wa Lishe endelevu ukitambulishwa Dodoma

Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Delloite,Manoff na PANITA limetambulisha rasmi mradi wa lishe endelevu kwa viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma ili kuimarisha hali ya lishe kwa wanawake,vijana na watoto.

Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 28,2019 katika ukumbi wa Morena Hoteli Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa Dodoma,Mheshimiwa Binilith Mahenge.

Mradi huo wa Lishe Endelevu unalenga kuimarisha hali ya lishe kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa, wajawazito na wanaonyonyesha, vijana wa rika la balehe na watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano ambao ni waathirika wakubwa wa lishe duni.

Mahenge alisema mradi wa Lishe Endelevu ni fursa kwa wananchi wa Dodoma hivyo kuwaomba watendaji wa serikali kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau wanaotekeleza mradi huo ili wafanye kazi katika mazingira ya amani na utulivu kufikia malengo ya mradi.

“Malengo ya mradi huu kimsingi yanaimarisha afya na lishe ya jamii ambayo ni mtaji mkubwa katika kuimarisha nguvu kazi ya taifa haswa katika kipindi hiki cha mpito kuelekea uchumi wa kati”,alieleza mkuu huyo wa mkoa. 

“Tunawakaribisha sana wadau wetu wa Lishe Endelevu na tuwatakia heri na mafanikio makubwa katika utekelezaji wa malengo ya mradi. Twendeni tukiwa tunakumbuka kuwa lishe bora ni msingi wa maendeleo ya Jamii, mkoa na Taifa kwa ujumla, viongozi na watendaji wa mradi huu tekelezeni majukumu yenu kama yalivyoainishwa kwenye malengo ya mradi”,alisema.

Katika hatua nyingine alisema Lishe duni haiathiri tu maendeleo ya mtoto lakini pia inaathiri ukuaji wake kimwili na kiakili kutoka kipindi cha ujauzito na hatimaye kuathiri mchango wake katika maendeleo ya taifa kwa kipindi chote cha uhai wake hivyo mradi huo utasaidia kuondokana na changamoto hizo.

Aidha aliwaomba wadau wa lishe mkoani Dodoma kuongeza jitihada kupunguza utapiamlo kwa watoto walio chini ya miaka mitano ingawa  takwimu za hivi karibuni (TDHS 2015/16) zimebaini kuwa Udumavu umepungua kutoka asilimia 56.0 (2010) hadi asilimia 36.5 mkoani humo. 

“Hali ya lishe ya wanawake walio katika umri wa uzazi (miaka 15-49) nayo bado ni mbaya; sote tunajua, hali ya lishe ya mama ikiwa mbaya inaathiri hali ya mtoto toka tumboni pamoja na malezi na makuzi ya mtoto. Tafiti za hivi karibuni zimebaini kwamba, kati ya wanawake kumi, wastani wa wawili wana utapiamlo",aliongeza. 

Alibainisha kuwa lishe duni kwa wanawake wajawazito inachochea hatari ya kujifungua watoto njiti, waliodumaa au kuharibu mimba hivyo vifo vya wanawake wajawazito vitapungua sana endapo serikali kwa kushirikiana na wadau watakuwa na mikakati ya pamoja ya kutatua changamoto mbalimbali zinazomkabili mama mjamzito, aliyejifungua na mtoto chini ya miaka mitano.

Kwa upande wake,Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Dodoma Benety Malima aliwaomba wadau wa lishe mkoani humo na serikali kushirikiana katika kutekeleza mradi huo ambao utasaidia kuimarisha hali ya lishe kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa, wajawazito na wanaonyonyesha, vijana wa rika la balehe na watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.

Malima alisema mradi huo mradi huo unatekelezwa katika mikoa minne ya Dodoma, Rukwa, Iringa na Morogoro kwa kipindi cha miaka minne Kwa miaka minne mradi utagharimu USD 19.7 Milioni ukifadhiliwa na Mfuko wa watu wa Marekani ‘USAID’.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Binilith Mahenge akitoa hotuba wakati Shirika la Save the Children kwa kushirikiana na Delloite,Manoff na PANITA likitambulisha mradi wa lishe endelevu kwa viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Binilith Mahenge akitoa hotuba wakati mradi wa lishe endelevu ukitambulishwa kwa viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Dodoma Benety Malima akiandika dondoo muhimu wakati Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Binilith Mahenge akitoa hotuba wakati mradi wa lishe endelevu ukitambulishwa kwa viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma.
Viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma wakiwa ukumbini.
Picha ya pamoja viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma baada ya mradi mradi wa lishe endelevu kutambulisha.

Share:

FISI WANAOTAFUNA NYETI WAZUA GUMZOUchungu wa kufinywa nyeti ni wa ajabu zaidi kwa wanyama na hata binadamu na hivyo kwa kutaja tu kisa cha aina hiyo, mwili husisimuka. 


Katika Mbuga ya Kitaifa ya Aberdare, nyati dume wanaishi kwa uoga mkubwa sana baada ya fisi katika mbuga hiyo kugeuka katili na kuanza kufanya sehemu hizo muhimu kwa wanayama hao kuwa mlo.

Kulingana na ripoti ya K24 TV, Shirika la Huduma ya Wanyama Pori nchini (KWS) limeanza kuchunguza visa hivyo ili kuokoa nyeti za nyati dume katika Aberdare. 

Shirika hilo sasa linachunguza kuhusu tabia ya fisi ya kuwatesa nyati kwa kunyofoa nyeti zao hali inayoweza kuhatarisha uwepo wa nyati.

 Uchunguzi uliotolewa awali umeonyesha kuwa, sababu ya fisi kufanya hivyo ni kukosekana kwa simba, chui na hata duma ambao kawaida huwaua wanyama wengine na kula nyama kisha kuachia fisi mabaki.

 "Katika hifadhi zingine kuliko na simba, fisi hula mabaki lakini katika Aberdare kunakokosekana simba, wanalazimika kuwinda na katika hali hiyo hawawaui walengwa wao lakini huishia kunyofoa sehemu za miili yao," Lilian Ajuoga, afisa mkuu katika KWS Aberdare alisema.

 "Wakiwinda nyati wadogo na nyeti zao kunyofolewa, basi nyati hao hukua bila ya ishara za kuonyesha wao ni dume," aliongezea. 

Katika hali ya kujilinda, nyati katika mbuga hiyo sasa wameanza kutembeaakundi lakini kwa upande mwingine, fisi nao wameanza kujiweka katika makundi ili kuimarisha uwezo wao wa kufanikiwa katika kuwinda. 

 Hapa itakuwa ni mwenye nguvu mpishe. 


Share:

SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA AJIRA 4,549 ZA WALIMU

Serikali imetangaza nafasi za ajira 4,549 za walimu wa shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2018/19 ili kupunguza uhaba wa walimu ulipo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,amesema Serikali inajua kuwa kuna changamoto nyingi katika sekta ya elimu nchini hasa uhaba wa walimu hivyo itaajiri walimu ili kupunguza uhaba uliopo.

Hata hivyo Jafo amesema kuwa ajira hizo mpya kwa waombaji zinapaswa kuombwa kwa njia ya mtandao na mwisho wa kupokea maombi utakuwa Machi 15, mwaka huu.

”Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli inaendelea kuongeza idadi ya watumishi katika sekta ya umma kwa kutoa nafasi mbalimbali za ajira kwa vijana wa kitanzania katika sekta ya Elimu”amesema Jafo.

Waziri Jafo amesema kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi inawatangazia walimu wenye sifa hizo kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao (Online Teacher Employment Application System-OTEAS).

Jafo amesema kuwa kwa walimu wa shule za msingi wanaotakiwa kutuma maombi ni wenye sifa za kitaaluma Daraja la IIIA wenye Astashahada ya ualimu, na wenye daraja la IIIB wenye Stashada (Diploma ya ualimu katika masomo ya Kingereza, Uraia, Historia, Jiografia na kiswahili.

Aliongeza kuwa walimu wenye sifa ya Daraja la IIIC wenye shahada ya ualimu kwa masomo ya Kingereza,Uraia,somo la ziada,Historia,Geographia na Kiswahili.

Jafo ametangaza kundi jingine lenye sifa ni Mwalimu mwenye Daraja la IIIC na mwenye mahitaji maalum aliyehitimu Shahada kwa masomo ya English,Uraia,somo la ziada,Historia,Geographia na kiswahili.

Kwa walimu wa sekondari Waziri Jafo amesema kuwa wao wanaotakiwa kufanya maombi ni Mwalimu wenye Daraja la IIIC mwenye Shahada ya ualimu aliyesomea Elimu maalum.

Jafo amesema wengine ni wenye Daraja la IIIB wenye Stashahada (Diploma) ya ualimu waliosomea Elimu maalum na mwalimu Daraja la IIIB mwenye Stashahada ya ualimu somo la Mathematics, Biology, Physics,na Chemistry.

Amesema wengine wenye sifa za kuomba ni mwalimu daraja la IIIC mwenye shahada ya ualimu somo la Agriculture Science, na mwalimu wa Daraja la IIIC mwenye Shahada ya ualimu somo la Home Economics na mwalimu Daraja IIIC mwenye Shahada ya ualimu somo la Physics, Mathematics, Chemistry na Biology.

Aidha Jafo ameongeza kuwa walimu wengine ni wa Daraja IIIC wenye shahada ya ualimu somo la Book keeping, Commerce, Accounts na Economics na mwalimu daraja la IIIC mwenye Shahada ya ualimu somo la English, Civics na General Studies.

Hata hivyo Jafo amesisitiza kuwa waombaji wenye sifa zote hizo wanatakiwa kuwa watanzania, wawe wamehitimu kati ya mwaka 2014 hadi 2017 isipokuwa kwa kundi maalum la wahitimu wa elimu ya ualaimu wa masomo ya Fizikia na Hisabati.

Jafo amesema kuwa sifa nyingine ya jumla kwa muombaji asiwe na umri zaidi ya miaka 45, na wakati wa kutuma maombi walimu ambao waliwahi kutuma na hawajaajiriwa wanapaswa kutuma upya.
Na.Alex Sonna/Fullshangwe
Share:

MKUTANO WA TRUMP NA KIM JONG UN WAVUNJIKA

Katika hali ambayo haikutegemewa, Mkutano kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un umevunjika.


Mkutano wa siku mbili kati ya viongozi hao waliokutana nchini Vietnam umelazimika kuahirishwa baada ya kutofautiana katika masuala ya msingi, hivyo hawakufikia lengo la kutia saini nyaraka zozote.

Waandishi wa habari walishangazwa na taarifa ya kuahirishwa kwa chakula cha mchana kati ya viongozi hao ambacho walitarajia kushiriki kuchukua matukio.


Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba alitoka kwenye mkutano huo kwasababu ya masharti yasiyowezekana ya kiongozi hiyo ya kutaka nchi yake iondolewe vikwazo ilivyowekewa kwa uchochezi wa Marekani.

“Ndoto yetu na ndoto yao havikushabihiana. Wao walitaka kuondolewa vikwazo katika maeneo yote, na hatukuweza,” alisema Trump.

“Hatujakata tamaa, kuna uwezekano. Anataka kuachana na silaha za nyuklia, [Kim] anataka kufanya kwenye maeneo ambayo yana umuhimu kidogo kuliko tunavyotaka. Wakati mwingine inabidi kuondoka na wakati huo ulikuwa leo,” aliongeza.

Hata hivyo, Trump amemuelezea Kim kama kiongozi mzuri na kwamba anaamini wakati mwingine watafikia muafaka. Amesema ingawa mkutano huo haukuzaa matunda yaliyotarajiwa, kuna hatua ambazo zimepigwa kulinganisha na ilivyokuwa awali.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amewaambia waandishi wa habari kuwa katika makubaliano ya awali walibaini kuwa hakukuwa na kitu ambacho kingeifaidisha ipasavyo Marekani.

Amesema timu ya nchi hizo mbili itakutana tena kuendelea kujadiliana kwa mara nyingine ili wafikie muafaka.
Share:

HATMA YA DHAMANA YA MBOWE,MATIKO KESHO

Hatma ya dhamana ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko inatarajiwa kujulikana kesho March 1, 2019 katika Mahakama ya Rufani ambapo mahakama hiyo inatarajia kutoa uamuzi wa rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) dhidi ya Mbowe na Matiko.

Katika uamuzi huo, mahakama inatarajiwa ama kukubali Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuendelea kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mbowe na Matiko, kutokana na kufutiwa dhamana katika kesi ya uchochezi iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu au kuitupilia mbali rufaa hiyo.

Mapema Leo Februari 28.2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesi ya uchochezi inayowakabili vigogo hao na wenzao saba wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), iliitwa kwa ajili ya kutajwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon akadai kuwa bado wanasubiri hatua za rufaa zilizopo Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu.

Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Profesa Abdallah Safari alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi kuwa ni muhimu mahakama ikapewa taarifa ya maendeleo ya rufaa zote na kwamba wao wamepata taarifa kuwa kesho Mahakama ya Rufaa itatoa uamuzi dhidi ya rufaa hiyo.

Wakili Wankyo alipoulizwa alidai kuwa yeye bado hajapata taarifa kuhusu uamuzi huo na kwamba hata kama isingekuwa hivyo bado wanaomba tarehe ya kutajwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 14, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Novemba 23, 2018 Jaji Wilbard Mashauri akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, alifuta dhamana ya Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Wawili hao walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa Kisutu kufuta dhamana yao ambapo rufani yao ilipangwa kwa Jaji Sam Rumanyika.

Hata hivyo, baada ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika kusikiliza mapingamizi ya pande zote iliamua kuanza usikilizaji wa rufaa hiyo.

Upande wa serikali ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi ulidai kuwa wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga maamuzi yaliyotolewa na Mahakama Kuu.
Share:

Picha : LOWASSA AFIKA NYUMBANI KWA RUGE MUTAHABA KUWAFARIJI WAFIWA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa leo asubuhi wamefika nyumbani kwa Prof. Mutahaba ambaye ni baba mzazi wa Ruge Mutahaba aliyekuwa mkurugenzi wa uzalishaji vipindi wa Clouds Media Group kutoa pole na kuwafariji wafiwa.

Ruge Mutahaba Alifariki dunia Juzi nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu ya figo zilizoanza kumsumbua mwaka jana. 

Mwili unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam kutokea Afrika Kusini siku ya kesho Ijumaa, Machi 1, 2019.
Share:

BENKI YA NMB YAMWAGA MISAADA KUSAIDIA SHULE MKOANI KATAVI


Benki ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa kwa ajiri ya shule za Sekondari na msingi vyenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa shule za Sekondari tano na tatu za msingi mkoani Katavi.

Hafla za makabidhiano hayo zilifanyika jana katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Rungwa katika Manispaa ya Mpanda na kuhudhuriwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Katavi ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga na wakuu wa Wilaya za Tanganyika , Mlele, Meya wa Manispaa ya Mpanda , Wenyeviti wa Halmashauri na wakurungezi wa Halmashauri hizo.

Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni pamoja na mabati 1,248 ambayo yatatumiwa kwa ajiri ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika sekondari za Mizengo Pinda katika Wilaya ya Mlele , Simbesa sekondari , Bulamata Sekondari zilizopo katika Wilaya ya Tanganyika na Sekondari ya Kakese katika Manispaa ya Mpanda .

Shule za Msingi zilizonufaika na msaada huo ni Katavi katika Manispaa ya Mpanda , Luchima na Ikulwe katika Halmashauri ya Mpimbwe .

Pia Benki ya NMB imetoa msaada wa wa viti na meza za kusomea 62 kwa ajiri ya Sekondari ya Rungwa ambayo ilikuwa inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu viti na meza za kusomea 402 hali ambayo ilikuwa ikiwafanya wanafunzi washindwe kusoma kwa raha.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,   Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola alisema kuwa msaada huo wameutowa ni katika kuunga mkono juhudi za Serikari kwa jamii ya Kitanzania ,na kwa kuwa Benki ya NMB imeguswa na uhitaji wa shule hizo wamejisikia faraja kuzisaidia .

Chilongola alisema kwa mwaka 2018 NMB imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajiri ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusidia sekta ya afya na elimu ,Kiasi hiki kinaifanya kuwa benki ya kwanza katika kuchangia maendeleo kuliko benki yoyote hapa nchini.

"Kiasi hiki kinaweza kuonekana si kikubwa sana lakini kimekuwa msaada mkubwa kwa jamii hasa katika sekta ya afya na elimu kwani vifaa vya Afya na Elimu vimekuwa ni changamoto kubwa katika katika Hospitali na vituo vya afya vingi na shule zetu hapa nchini", alisema Meneja huyo wa Kanda.

Alieleza kuwa NMB imezifikia Wilaya zote nchini kwa asilimia 100 na wanaendelea kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya mitandao ili kuwafikishia huduma za kibenki wananchi wengi zaidi.

Benki hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau wake wakubwa katika kuhakikisha kuwa changamoto za jamii zinapatiwa ufumbuzi katika kujenga elimu bora kwa jamii ya Kitanzania.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga alisema Benki ya NMB imekuwa karibu sana na Serikali katika kusaidia maendeleo hapa nchini .

Alisema msaada huo waliotoa kwa shule hizo katika Mkoa wa Katavi utasaidia katika kusukuma maendeleo ya elimu hivyo aliomba wadau mbalimbali waweze kusaidia kwenye elimu kama ambavyo walivyofanya benki hiyo kwani changamoto ya elimu na afya bado ni kubwa .

Mkuu wa Wilaya ya Mlele,  Rachael Kasanda aliipongeza benki ya NMB kwa kutoa msaada huo na kubainisha kuwa wameonyesha jinsi wanavyoijali jamii ya Wanzania kwani fedha hizo walizotumia shilingi milioni 40 wangeweza kuziingiza kwenye biashara yao.

Afisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Mpanda Raphael Mkupi alisema msaada wa viti na meza uliotowa na NMB kwa shule ya Sekondari ya Rungwa utasaidia sana kupunguza tatizo la upungufu wa viti na meza kwa wanafunzi hapo shuleni yenye kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita ambapo wanafunzi 62 kati ya 402 ambao walikuwa hawapati huduma ya viti na meza sasa watapata huduma ya samani nzuri kutoka Benki ya NMB.

Na Walter Mguluchuma - Katavi.
Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola (wa nne kutoka kushoto pichani) akimkabidhi bando za bati katika shule ya sekondari Rungwa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Charles Matinga  (wa tatu kutoka kushoto pichani) msaada huo ni mwendeleza wa NMB kuchangia katika sekta ya elimu na afya -Picha na Walter Mguluchuma.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Charles Matinga (katikati) akikata utepe wakati akipokea madawati 62 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Charles Matinga (katikati) akipokea madawati 62 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla.

Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola akielezea kuhusu madawati waliyokabid
hi.
Picha na Walter Mguluchuma.
Share:

DUDUBAYA AANZA KUSHUGHULIKIWA... ANASHIKILIWA POLISI OYSTERBAY MAKOSA YA MTANDAO


Mwanamuziki Godfrey Tumaini maarufu ‘Dudu Baya' anashikiliwa na polisi katika kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema Msanii huyo anashikiliwa kwa mahojiano.

Dudu Baya aliyewahi kutamba na wimbo Mwanangu Huna Nidhamu, amekamatwa baada ya kuamriwa na Baraza la Sanaa la Taifa kufanya hivyo.

Jana, Waziri wa Habari na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliagiza Jeshi la Polisi na Basata wamchukulia hatua mwanamuziki huyo kwa makosa ya kumkashifu, aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Ruge Mutahaba.

Baada ya amri hiyo, Basata ilimtaka mwanamuziki huyo kujisalimisha katika kituo cha polisi Oysterbay asubuhi ya leo.

Mwanamuziki huyo ameshtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya mtandao.

Chanzo - Mwananchi
Share:

WENYE MAKALIO MAKUBWA WATUA KWA SPIKA KULALAMIKA SHINDANO LAO KUZUIWA


Waandaaji wa shindano la wanawake walio na maumbo makubwa nchini Uganda wamewasilisha malalamiko yao kwa spika wa bunge kufafanua madhumuni yao.

Wamesema kuwa lengo lao sio kutumia shindano la 'Miss Curvy Uganda'' kuvutia watalii kuja nchini humo.

''Haya ni mashindano ya urembo wa wanawake wanene''alisema Annie Mungoma, mkurugenzi mkuu wa mashindano hayo.

Bi. Mugoma aliongeza kuwa mtazamo wao itaondosha fikra za kimagharibi kuwa urembo unamaanisha mtu kuwa mwembamba.

''Tunataka kuwapatia motisha wanawake wenye maumbo makubwa kujiamini kwamba wao pia ni warembo''.Baadhi ya waandalizi wa Miss Curvy Uganda wakizungumza na Spika wa Bunge la Uganda Rebecca Kadaga

Siku mbili zilizopita spika wa bunge Rebecca Kadaga aliyepinga vikali mashindano hayo amebadili msimamo wake baada ya kupokea ufafanuzi huo.

Ameahidi mkono juhudi zao na kutoa ufafanuzi kwa bunge ili kuondoa fikra kwamba mashindano hayo ni ya aibu kwa jinsia ya mwanamke.

Tangu shindano shindano hilo lilipozinduliwa mapema mwezi huu, wanasiasa,wanaharakati wa haki za wanawake na viongozi wa kidini wamejitokeza na kulishtumu vikali.
Waziri wa utalii nchini Uganda Godfrey Kiwanda alipendekeza kuwe na onyesho la wanawake wenye maumbo makubwa ili kuvutia wageni zaidi wanaoitembelea nchi hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi wa shindano hilo , waziri huyo alisema kuwa itakuwa "tukio la kipekee ambalo litawaonesha mabanati wakionesha maumbo yao mazuri yaliyo nona"

Kauli hiyo ilizua mjadala mkali hasa katika mitandao ya kijamii huku baadhi ya watu wakimshutumu bwana Kiwanda kwa kuzungumza juu ya wanawake wanene kama wananyama huku mwanamke mmoja akihoji kama ingewezekana basi wawekwe bustanini ili watazamwe kama wanayama watendewavyo ".
Licha ya mjadala huo kufikia sasa washiriki 200 kutoka sehemu mbalimbali za Uganda pamoja na nchi jirani ya Rwanda wamejisajili kushiriki shindano la Miss Curvy Uganda linalotarajiwa kufanyika mwezi wa June mwaka huu.
Chanzo- BBC
Share:

TAPELI AWALIZA WATUMISHI WA UMMA.....SERIKALI YATOA TAHADHARI
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

FUNGUA PAZIA

NDOA ZA UTOTONI

Narudi nyumbani

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger