Saturday 31 December 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 1,2023





Share:

WAANDISHI WA HABARI WAWANYOOSHA WATUMISHI MANISPAA YA SHINYANGA...BODABODA WAKIWATWANGA MILUNDA FC

Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakifurahia zawadi ya Mbuzi baada ya kuibuka washindi kwa kuichapa Timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga bao 3-2

 Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Sherehe za kumaliza mwaka 2022 na kukaribisha mwaka 2023 katika mkoa wa Shinyanga zimependezeshwa na bonanza la mpira wa miguu lililoshirikisha timu nne ndani ya Manispaa ya Shinyanga ambapo Timu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga imewachapa Watumishi wa Manispaa ya Shinyanga bao 3-2.


Bonanza hilo la michezo lililoongozwa na Kauli Mbiu 'Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu  inawezekana' limefanyika leo Jumamosi Desemba 31,2022  viwanja ya shule ya msingi Balina kata ya Ndembezi limendaliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga  kwa kushirikiana na MC Mzungu Mweusi ambapo Mgeni rasmi alikuwa Kamanda wa jeshi la pollisi mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi.


Bonanza hilo lililoambatana na michezo ya sarakasi  limeshirikisha Timu  nne za mpira wa miguu ambazo ni Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Watumishi wa manispaa ya Shinyanga, Bodaboda wa kata ya Ndembezi na Wauzaji wa miti ya ujenzi (Milunda FC).

Akizungumza wakati wa Bonanza hilo, Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ,ACP Janeth Magomi amesema ,michezo ni afya na michezo inajenga mahusiano katika jamii.

Kamanda Magomi ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi Mkoa wa Shinyanga kusherehekea sikukuu ya Mwaka Mpya 2023 kwa amani na utulivu huku akibainisha kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote.

Katika mchezo wake Timu ya waandishi wa habari iliweza kushinda na kuwanyakua mbuzi mnyama kwa kupata penati 3 dhidi ya 2 za wapinzani wao ,Timu ya watumishi Manispaa ya Shinyanga huku waendesha bodaboda kata ya Ndembezi wakiichapa Milunda FC bao 7-6 kwa mikwaju ya penalti. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi
MC Mzungu Mweusi (Amos John) akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa Timu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakifurahia zawadi ya Mbuzi baada ya kuibuka washindi kwa kuichapa Timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga bao 3-2
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakifurahia zawadi ya Mbuzi baada ya kuibuka washindi kwa kuichapa Timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga bao 3-2
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakifurahia zawadi ya Mbuzi baada ya kuibuka washindi kwa kuichapa Timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga bao 3-2
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakifurahia zawadi ya Mbuzi baada ya kuibuka washindi kwa kuichapa Timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga bao 3-2
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa Timu ya Waendesha Bodaboda
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa Timu ya Waendesha Bodaboda
Timu ya Waendesha Bodaboda wakifurahia zawadi ya Mbuzi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya Juisi kwa Timu ya Milunda FC
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya Juisi na Soda kwa timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga


Share:

AZIZI KI AITUNGUA MTIBWA SUGAR, YANGA SC IKIONDOKA NA USHINDI 1-0


************************

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya yanga immeweza kuondoka na alama tatu mbeleya Mtibwa Sugar baada ya kufanikiwa kuichapa bao 1-0, mchezo ambao ulipigwa katika dimba la Manungu mkoani Morogoro.

Katika mchezo huo Yanga Sc iliwakosa baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza lakini haikuwazuia kupata alama tatu kwenye mchezo wao huo muhimu ambapo Yanga alikuwa ugenini.

Bao pekee la Yanga Sc limewekwa kimyani na nyota wao Azizi Ki ambaye alipiga mpira wa adhabu ambao ulimshinda kipa wa Mtibwa Sugar Razaki na kutinga moja kwa moja wavuni na Yanga Sc kuondoka na ushindi.
Share:

MWAMALA WAJANJARUKA KULAZA WATOTO CHUMBA KIMOJA NA WAGENI.... "HII HAIKUBALIKI SASA, TUNATAKA KUKOMESHA UKATILI"


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na viunga vyake kupitia kipindi maalumu cha Redio Faraja Fm, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Afisa Mtendaji wa kata ya Mwamala Suzana Kayange
Sehemu ya Wakazi wa kata ya Mwamala Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakizungumza na Mwandishi wa habari, Kadama Malunde (kulia).

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wakazi wa kata ya Mwamala Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wameanza kuchukua hatua kudhibiti vitendo vya kuacha kulaza watoto chumba kimoja na wageni ikiwa ni sehemu ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto.

Wakizungumza na Malunde 1 blog kwa nyakati tofauti wakazi wa Mwamala wamesema hivi sasa wamejanjaruka na kuacha tabia ya kulaza watoto chumba kimoja na wageni ili kudhibiti ukatili dhidi ya watoto.

Mmoja wa wakazi hao Bundala Pius amesema licha ya kwamba ni hatari kulaza watoto chumba kimoja lakini wamekuwa wakilazimika kutokana na uwezo mdogo wa kiuchumi kujenga nyumba kubwa yenye vyumba vingi lakini ili kudhibiti vitendo vya ukatili dhidi ya watoto sasa wameanza kuachana na tabia ya kulaza watoto chumba kimoja na wageni.

“Watoto wasilale chumba kimoja na wageni. Hivi sasa kulaza watoto na wageni hatuwezi kuivumilia, haikubaliki sasa, hatukujua madhara ya kulaza chumba kimoja na wageni”, wamesema Masanja Malale na Ngasa Mhoja.


“Kulaza watoto na wageni siyo vizuri, wageni wengine hawana adabu, hawana maadili, ukiwalaza chumba kimoja na watoto wanawafanyia vitendo vya ukatili ikiwemo kuwabaka na kuwalawiti”,amesema Mboje Malale Luhaga.

Naye Monica James amesema vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vimekuwa vikifanywa na ndugu wa karibu hivyo ili kuepuka ukatili dhidi ya watoto ni lazima kudhibiti tabia ya kulaza watoto chumba kimoja na wageni.


Afisa Mtendaji wa kata ya Mwamala Suzana Kayange amesema mwamko huo wa wananchi kuacha kulaza watoto chumba kimoja na wageni unatokana na elimu ambayo serikali kwa kushirikiana na wadau yakiwemo mashirika yamekuwa wakiwapa wananchi katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Tumekuwa tukiwaelimisha wazazi wasilaze chumba kimoja na wageni/ndugu hata kama ni jinsi moja kutokana na kwamba vitendo vya ukatili vimekuwa vikifanywa na watu wa karibu.Tunawaelimisha pia watoto wasilale chumba kimoja na wageni”,amesema Afisa Mtendaji kata ya Mwamala.


Akiwa Mkoani Shinyanga Desemba 5,2022 , Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima alisema ukatili ni ajenda inayohitaji juhudi za pamoja kupinga vitendo hivyo, kwa kuwa takwimu zinaonesha kuwa asilimia 60% ya ukatili wa kijinsia kwa Watoto hutokea majumbani wakati asilimia 40% hufanyika shuleni.


Alisema kuwa Mwaka 2021 Watoto 11,499 walifanyiwa ukatili wa kijinsia ikiwemo kubakwa,kulawitiwa na mimba katika umri mdogo ,hali ambayo inahitaji kuongeza kasi ya kukabiliana na vitendo hivyo ambavyo ni kikwazo dhidi ya maendeleo na ustawi wa jamii.


Dkt. Gwajima alieleza kuwa takwimu za Mwaka 2021 zinaonesha kuwa watoto 5,899 walibakwa, wakati 1,114 walilawitiwa na wengine 1677 walipata mimba katika umri mdogo,vitendo ambavyo watoto wanafanyiwa wakiwa katika mazingira ya nyumbani au shuleni.


“Tunajenga shule ili watoto wasome na kuhitimu lakini wanaishia kupata mimba katika umri mdogo, tafiti zinaonyesha vitendo vya ubakaji na ulawiti hutokea nyumbani kwa asilimia 60,na asilimia 40 hutokea shuleni,serikali haitaweza kujenga shule kwa ajili ya kutunza watoto ili waendelee na kustawi katika maisha yao lakini kumbe huko huko wanabakwa,huko huko wanalawitiwa,lakini ulawiti unaanzia nyumbani walipo Baba,Mama,ndugu na jamaa na baadaye unaenea shuleni kwa watoto wengine ambao pengine wazazi wao wanajitahidi kuwalinda lakini wanakuja kushawishiwa wakiwa katika mazingira ya shuleni”, alisema Dkt. Gwajima.
Share:

MTO TISHIO KWA KUUA WATU, WAUA TENA GEITA


Benjamin John mkazi wa kata ya Kasamwa halmashauri ya mji Geita, amefariki dunia huku wengine wakinusurika kifo baada ya kusombwa na Maji wakati wakijaribu kuvuka katika mto Nyampa kuelekea kijiji cha jirani.

Baadhi ya mashuhuda wanaeleza kuwa mtu huyo alisombwa na maji akijaribu kuvuka huku wakiiomba serikali kuwajengea daraja kwani eneo hilo limekuwa likichukua uhai wa watu kipindi cha mvua.

"Yule mvukaji mwingine alipita lakini yule mwingine wakati anajaribu kupita akawa amezidiwa na maji, basi mwenzake akashindwa jinsi ya kumuokoa akaona kwamba na yeye anaweza kuvutwa kwa sababu mto ulikuwa umefurika maji", alisema Juma moja ya mashuhuda wa tukio hilo

"Hizi ajali za watu kuzama kwenye mto zinatokea mara kwa mara, ningeomba serikali iangakie utaratibu, ikiwezekana watutengenezee madaraja sehemu ambayo watu wanavuka wengi ili kuepusha sanasana hizi ajali na pia huu mto, huwa wanapita mara kwa mara huwa unabeba vitu vingi Sana ikiwemo wakulima hivyo unaharibu mpunga wao", alisema Aloyce.

"Kwangu mimi nilikuwa naomba serikali itusaidie kuweka daraja inapotokea swala la mto unapita watu wawe wanavuka wanaenda kwenye kazi zao za mashambani", alisema Kabeho.

Mwenyekiti wa mtaa wa Nyampa Helena Maneno anasema katika eneo hilo wameshafariki watu nane kwa kusombwa na maji nyakati tofauti tofauti.

"Mto huu tuseme miaka miwili huwa haipiti bila kuua, mara kwa mara huu mto unakuwa unaua watu, kuna kipindi watoto watatu walifia ndani ya mto huu, kuna kipindi tena kijana mmoja akawa amefia kwenye mto huu ni kama watu wanane wanafika, kwa kweli huu mto ni tishio", alisema Maneno

Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita limefanikiwa kupata mwili wa marehemu huku mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Kasamwa akikiri kupokea mwili wa marehemu.

"Kwamba kipindi hiki ni mvua za masika na mito inajaa, kwahiyo tuchukue tahadhari, usalama wetu kwanza najua watu wanafanya shughuli za uchumi, kilimo baada ya hapo wanakuwa wamechafuka na kwenda kuoga kwenye mto kwahiyo niwashauri bora waende na ndoo achote maji anawe pembeni au akaoge nyumbani na asijaribu kuyapima maji kwa mguu maji yana pressure Kalu yanaweza yakakupelekea kupoteza maisha", alisema Lukuba.

"Tumempokea wakampeleka Mochwari, baada ya kupelekwa Mechwari kufanyiwa uchunguzi wa haraka yani uchunguzi wa awali ambao uliinvolve kumwangalia marehemu kuaniza juu mpaka chini sehemu zote za mwili wake na hatukukuta jeraha licha ya michubuko, obvious ilikuwa ni miba ambao alipokuwa amezama kwenye maji", alisema Alex.
Share:

SERIKALI KUMEGA HEKTA 33,132.24 ZA HIFADHI KUWAPATIA WANANCHI RUVUMA


Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakiongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa tatu kulia) wakiondoka mkoani Ruvuma baada ya kumaliza kazi ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika mkoa huo 30 Desemba 2022. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza katika kikao baina ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Ruvuma tarehe 30 Desemba 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza katika kikao baina ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Ruvuma tarehe 30 Desemba 2022. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas.
Sehemu ya washiriki wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Ruvuma tarehe 30 Desemba 2022.
Sehemu ya washiriki wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Ruvuma tarehe 30 Desemba 2022.


Na Munir Shemweta, WANMM RUVUMA

Serikali itamega jumla ya hekta 33,132.24 katika mkoa wa Ruvuma kutoka maeneo ya hifadhi na shamba la NAFCO na kubakizwa kwa wananchi kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Aidha, imeelekeza wananchi wote waliovamia Hifadhi ya Msitu wa Lihanje uliopo halmashauri ya wilayani Songea kusitisha shughuli zozote za kibinadamu katika maeneo ya mlimani na bondeni mwaka huu,

Hayo yameelezwa tarehe 30 Desemba 2022 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula katika kikao cha Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Ruvuma wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kwa ajili ya kutoa mrejesho wa Maamuazi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na Utatuzi wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi katika vijiji 975.

Dkt Mabula ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta alisema, mkoa wa Ruvuma unahusisha vijiji/mitaa 38 yenye migogoro ya matumizi ya ardhi ambapo maamuzi ya Kamati ni kumega sehemu ya maeneo ya hifadhi kuwaachia wananchi sambamba na kusitishwa shughuli za kibindamu kwenye hifadhi .

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, wakati wa zoezi la tathmini kuhusu migogoro ya matumizi ya ardhi kwenye mkoa wa Ruvuma timu ya wataalamu ilivifikia vijiji/mitaa 38 katika wilaya za Mbinga, Nyasa, Tunduru, Namtumbo na Songea ambapo zoezi la uwandani lilihusisha na kufanya vikao na uongozi wa serikali za vijiji husika na kisha kutembelea maeneo yenye migogoro.

‘’Pamoja na maamuzi haya ya serikali ya kumega maeneo kwa ajili ya vijiji mkoa unalo jukumu la kusimamia utekelezaji wa maamuzi hayo kwa kusimamia utekelezaji huo kwa kushirikiana na taasisi na mamlaka zote zilizopo ndani ya mkoa na ni muhimu maeneo haya yaliyomegwa kuandaliwa mpango wa matumizi ya ardhi ili kuepuka matumizi holela ’’ alisema Dkt Mabula

Akigeukia umauzi wa serikali kusitisha shughuli za kibinadamu kwa wananchi waliovamia hifadhi ya msitu wa Lihanje, Dkt Mabula ameelekeza mkoa kwa kushirikiana na timu atakayoiunda kufanya tahmini ya kina ya mahitaji halisi ya ardhi kulingana na idadi ya watu waliopo katika vijiji hivyo na kuahidi timu yake ya mawaziri wa wizara za kisekta kurejea tena mapema januari 2023 kwa ajili ya kupokea taarifa na kutoa maamuzi.

‘’wananchi wote waliovamia hifadhi yam situ wa Lihanje kwa kuendesha shughuli za kilimo kwa maeneo ya mlimani na bondeni wanaelekezwa kusitisha shughuli zozote za kibinadamu katika maeneo hayo kwa mwaka huu’’ alisema Dkt Mabula.

Msitu wa Lihanje unasimamiwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na ni vyanzo muhimu vya maji vyenye mradi wa maji mtiririko Luyelela na Kilagano ambapo wananchi wamevamia takriban asilimia 60 ya msitu na kuendesha shughuli za kilimo,

Aliushukuru mkoa wa Ruvuma kwa kuweza kuratibu vyema zoezi la tahmini alilolieleza kuwa limewezesha kazi hiyo kufanyika kwa amani na utulivu huku akitambua mkoa huo unazo changamoto nyingi zinazosababishwa na muingiliano wa matumizi ya ardhi.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana amewataka wananchi kukemea wale wanaoharibu vyanzo vya maji na kuzitaka mamlaka zote kuanzia ngazi ya vijiji kuhakikisha zinadhibiti uvamizi wowote unaofanyika katika hifadhi za misitu na mapori ya akiba.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma Comredi Odo Mwisho amesema chama chake kinaungana na serikali kuhakikisha inalinda maeneo yote yaliyotamkwa kuwa ni hifadhi ya asili ili kuepuka uharibifu wa mazingira n auto wa asili.

Timu ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta imehitimisha ziara yake katika mkoa wa Ruvuma na januari nne , 2023 inatarajiwa kuendelea na ziara yake katika mkoa wa Mara.

Share:

BENKI YA CRDB YAONYESHA NJIA MFUMO WA MALIPO KIDIJITALI WA BANDARINI

Mkurugenzi wa Benki ya CRDB nchini Congo, Jesca Nachiro (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Plasduce Mbossa wakiwa wameshika banngo lenye kutambulisha mfumo mpya wa malipo ya kadi kwa wateja wa Bandari uliorahisishwa kupitia Benki ya CRDB, katika hafla ya uzinduzi huo huo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Bandari, jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha na Uondoshaji Shehena Bandarini, Edward Urio akishuhudia pamoja na wadau wengine.
Wakati Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ikizindua mfumo wa Malipo kwa njia ya ya kidijitali jijini Dar Es Salaam Desemba 30, 2022, imeelezwa kuwa sehemu kubwa ya uanzishwaji wa mfumo huo imefanikishwa na Benki ya CRDB ambayo imekuwa kinara wa mifumo ya malipo hapa nchini kwa miaka mingi.

Akizungumza kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Nchini Congo, Jesca Nachiro amesema uzoefu mkubwa ambao benki hiyo unao katika katika mifumo ya malipo ndio iliyopelekea kuishauri Mamlaka ya Bandari kuanzisha kwa mfumo huo ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato lakini na kurahisha huduma za malipo kwa wadau.

Nyachiro ameishukuru Mamlaka hiyo kwa kuichagua Benki ya CRDB kuwa mshiriki katika utengenezwaji wa mfumo huo utakao wawezesha wateja wa bandari kufanya malipo popote walipo.
“Tunajivunijia kuona Benki yetu imeshiriki kwa kiasi kikubwa kuanzisha mfumo huu, tukiwa Benki ya kwanza kuunganisha huduma setu na mfumo. Ni imani yetu kuwa mfumo huu uleta mapinduzi makubwa kwa kuwezesha wateja wa Bandari kufanya malipo duniani kote,” alisema.

Akizungumzia kuhusu mfumo huo Nyachiro amesema kuwa utaenda kufunga mianya yote ya udanganyifu ambayo wateja walikuwa wakilalamikia kwa kupewa kiwango cha malipo kisicho sahihi.

Aliongezea kuwa Mfumo huo utaleta mapinduzi kwa TPA kwani pia unabadilisha fedha za kigeni bila mtu yeyote kuhusika.

Aidha alisema kwa kuzingatia kuwa TPA inahudumia nchi nyingi hivyo mfumo huo utawarahisishia kupata huduma kwa urahisi kwakufanya malipo kwa urahisi zaidi, ambapo malipo yatafanyika popote mteja alipo bila kulazimika kwenda benki.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa amesema kuwa mfumo huo utaenda kurahisisha utendaji wa bandari kwani ulipaji wa kutumia 'Control number' utatumika katika ufanyaji malipo yote ya bandari.

Amesema kuwa mfumo huo utasoma kila hatua ya malipo yanayofanyika kwa wateja katika kulipia malipo mbalimbali ambayo yatakuwa yamefanyika.

Mbossa aliishukuru Benki ya CRDB kwa kushiriki mchakato mzima wa uanzishwaji wa mfumo huo ambao pia umeunganishwa na mifumo ya kimataifa ya malipo ya Visa na MasterCard. Alibainisha kuwa VISA na Master Card ni mhimu katika biashara zinazofanyika kimataifa kwani zinatambulika kimataifa hivyo mfumo huo utarahishisha hata utendaji kazi wa Mamlaka kwa Ujumla.

Pia amesema mfumo huo utapunguza urasimu na foleni ambazo zilikuwa zinajitokeza hapo awali, pia amesema kuwa TPA itafungua kituo kikubwa cha huduma kwa wateja ili kuweza kutoa huduma kwa wateja pale wanapopata changamoto mbalimbali za Kiteknolojia wakati wa kufanya malipo.
Akizungumza wakati anazindua mfumo huo Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha na Uondoshaji Shehena Bandarini, Edward Urio aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali katika nyanja mbalimbali hususani katika kuleta mapinduzi ya kidigitali kwakurahisisha ukusanyaji wa mapato nchini. Aliipongeza Benki hiyo kuweza kubuni na kukamilisha mfumo ambao utakwenda kuleta mapinduzi makubwa na hivyo kuongeza ukusanyaji wa mapato katika Bandari zetu.

“Mfumo huu ni mahususi katika kusaidia ulipaji wa huduma zitolewazo na mamlaka ya bandari kwa wateja mbalimbli wa ndani na wa nje kutoka nchi nufaika zinazo pata huduma katika mamlaka ya badari nchini,” alisema.
Taasisi mbalimbali za kifedha zikiongozwa na Benki ya CRDB zimeunganisha mifumo yao ya malipo katika mfumo huo jambo ambalo linatarajiwa kuwawezesha Watanzania wengi wanaaotumia bandari hiyo kufanya malipo kwa urahisi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger