Saturday 30 April 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 1,2022










Share:

LATRA YATANGAZA NAULI MPYA ZA DALADALA NA MABASI YAENDAYO MIKOANI


Mamlaka ya udhibiti wa usafiri Ardhini LATRA imetangaza viwango vipya vya bei ya nauli za daladala na mabasi ya mikoani huku nauli ya daladala kwa wanafunzi ndio nauli iliyobaki kama ilivyokuwa.

Akitangaza viwango hivyo Mkurugenzi wa LATRA Gillard Ngewe amebainisha kuwa viwango hivyo vipya vya nauli vitaanza kutumika May 14, 2022, huku nauli iliyokuwa shilingi 400 ikiongeka na kuwa shilingi 500.

Ngewe amefafanua kuwa kwa sasa umbali wa Kilometa 0 – Kilometa 10 nauli yake ilikuwa shilingi 400 sasa hivi itakuwa shilingi 500, umbali wa Kilometa 15 nauli kwa sasa itakuwa shilingi 550, umbali wa Kilometa 20 nauli itakuwa shilingi 600, Kilometa 25 Nauli itakuwa shilingi 700 na kwa Kilometa 30 nauli itakuwa shilingi 850.

Haya yanajiri katika kipindi hiki ambapo bei ya mafuta imepanda, huku sababu kubwa ikitajwa kuwa vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, inayoathiri pia uchumi wa dunia.

CHANZO- EATV
Share:

MBUNGE ANASWA AKIANGALIA VIDEO ZA NGONO BUNGENI


Neil Parish Mbunge aliyenaswa akiangalia video za ngono Bungeni
***

MBUNGE wa Jimbo la Tiverton na Honiton nchini Uingereza Neil Parish yupo chini ya uchunguzi kutokana na kitendo chake cha kuangalia video za ngono akiwa Bungeni.


Mashuhuda wawili ambao ni wabunge wa kike wanadai walimuona Parish akiangalia video za ngono katika matukio mawili tofauti, kwanza alikuwa anaangalia akiwa Bungeni katika vikao vya kawaida lakini pia akaangalia tena kwa mara ya pili katika kikao cha kamati.



Katika hatua nyingine mke wa mbunge huyo amemtetea mume wake kwa kudai kuwa ni mtu mwema na hajawahi kuwa na tabia hiyo ingawa amesisitiza kuwa watu hawatakiwi kuangalia video za ngono kwani ni udharirishaji kwa wanawake.



Kutokana na kashfa hiyo mbunge Neil Parish amekubali kuwa atakuwa tayari kutoa ushirikiano wote kwa wahusika wa uchunguzi huku akikiri kuwa alifungua file hilo kwa bahati mbaya.



Kumekuwa na wito kutoka kwa waheshimiwa mbalimbali wakimtaka Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kumuwajibisha kwa kumuondoa madarakani.



Wabunge wengine hasa wa kike akiwemo Harriet Harman Kutoka chama cha Labour amemtaka ajiuzulu wadhifa wake kwani hafai kuwa mbunge na haoneshi picha nzuri kwa jamii.



Waziri Rachel Maclean amepigilia msumari kuwa mbunge huyo anatakiwa kujiuzulu mara moja akisema:

Neil Parish amesema yupo tayari kutoa ushirikiano na ikibainika ana hatia basi atakuwa tayari kujiuzulu

“Aina hizi za tabia hazina nafasi katika mazingira yoyote yale ya kazi ya Bunge lolote lile, Lakini kila mtu lazima atambue kuwa inapotokea shutuma ya jambo lolote lile siyo kazi yetu sisi kunyoosheana vidole bali ni mamlaka husika kuchukua hatua.”


Katika hatua nyingine Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kwa mara ya kwanza ameliongelea tukio hilo kwa kudai kuwa ni jambo ambalo halikubaliki katika mazingira yoyote yale ya kazi kuanzia ngazi ya juu hadi ngazi ya chini ya utendaji kazi.
Share:

SHEIKH KABEKE AWATAKA WANANDOA WASIISHI KWA MAZOEA..."NDOA HAIZOELEKI"


Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke ametoa rai kwa wanandoa kuacha kuishi kwa mazoea na badala yake kila siku waifanye ndoa kuwa kitu kipya kinachowapa furaha maishani huku wakilea familia kwa kuzingatia maadili na misingi bora.


Sheikh Kabeke alitoa rai hiyo wakati akitoa nasaha kwenye kongamano la malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa lililofanyika katika Msikiti wa Nyehunge Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema.


Sheikh Kabeke alisema kuna baadhi ya wanandoa wanaume kwa wanawake wanaleta mazoea kwenye ndoa na matokeo yake ni ndoa zao kuvunjika na kusababisha watoto kukosa malezi ya wazazi wa pande zote mbili jambo ambalo ni hatari kwani husababisha watoto kukimbilia mitaani.


"Ndoa haizoeleki, kila siku unatakiwa kuifanya iwe mpya, kuna baadhi ya wanaume na wanawake wanaleta mazoea kwenye ndoa na matokeo yake hazidumu. Tumekuja kupeana elimu hii ili turejeshe misingi ya ndoa kwani yapo mazoea ya kudhani mke au mme ni kiburudisho matokeo yake ndoa zinafungwa mwezi wa Shaaban na kuvunjika baada ya Ramadhan" alitahadharisha Sheikh Kabeke


Wakichangia mada kwenye kongamano hilo baadhi ya washiriki akiwemo Bi. Rehema Fundi na Seif Sungura waliomba BAKWATA kuendelea kutoa elimu ya malezi bora ili kurejesha misingi ya ndoa iliyopotea hatua itakayosaidia kutibu changamoto ya ndoa nyingi kuvunjika mapema.


Kongamano hilo ni mwendelezo wa makongamano ya 'malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa' yaliyoandaliwa na BAKWATA Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI katika Wilaya za Mkoa Mwanza katika kipindi cha mwezi wa Ramadhan lengo likiwa ni kurejesha maadili katika jamii, kutokomeza ukatili wa kijinsia na kuondoa watoto wa mitaani ambapo maoni yaliyokusanywa kwenye makongamano hayo yatawasilishwa katika Kamati ya MTAKUWWA mkoani Mwanza kwa ajili ya utekelezaji.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kaneke akizungumza kwenye kongamano la malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa lililofanyika katika Msikiti wa Masjid Tanbih Nyehunge katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema ambapo pamoja na mambo mengine aliwahimiza wanandoa kuishi kwa kuthaminiana lakini pia kuwa na utamaduni wa kupeana zawadi ili kusisimua mahaba miongoni mwao.
Sheikh wa Buchosa, Ahmed Jaha akichangia mada kwenye kongamano hilo ambapo aliwahimiza waumini wa dini ya kiislamu kuzingatia mafundisho ya Mwenyezi Mungu na maelekezo ya Mtume Mohamed hatua itakayosaidia kuishi kwa amani bila mifarakano.
Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo, Seif Sungura akichangia mada juu ya nini kifanyike kudumisha misingi ya ndoa ambapo alihimiza elimu zaidi kuendelea kutolewa kwa wanandoa kabla na baada ya kufunga ndoa.
Naye Zawadi Yusuph alisema darasa la ndoa ni muhimu kabla ya vijana kufunga ndoa na hivyo kuomba BAKWATA kuhakikisha hilo lunatekelezeka.
Kwa upande wake Bi. Rehema Fundi aliwahimiza wanawake kuwa watulivu na kuzingatia misingi ya ndoa hatua itakayosaidia kuishi kwa maelewano na waume zao na ndoa zao kudumu.
Katika Kongamano hilo, Sheikh wa Mkoa Mwanza Hassan Kabeke (kushoto) alimtangaza rasmi Omari Bausi kuwa Sheikh wa Kata ya Nyakaliro wilayani Sengerema baada ya aliyekuwa Sheikh wa Kata hiyo ambaye ni baba mzazi wa Sheikh Omari Bausi kufariki dunia. Uamuzi huo ulipitishwa na Halmashauri Kuu ya BAKWATA Mkoa Mwanza.
Picha ya pamoja
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke na ujumbe alioambatana nao alifika katika malalo ya aliyekuwa Sheikh wa Kata ya Nyakaliro kwa ajili ya kumsomea dua.

Share:

Friday 29 April 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 30,2022

Share:

BENKI YA CRDB YASHINDA TUZO MBILI ZA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI KITAIFA DODOMA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wanyeulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo ya mshindi wa pili Sekta za Fedha katika maadhimisho ya Usalama na afya Mahala pa Kazi iliyokwenda kwa Benki Benki ya CRDB ambayo ilipokelewa na Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki hiyo, Misana Mutani. Tuzo hiyo pamoja na ile ya Mshindi wa Jumla wa Huduma za Jamii ya OSHA zilitolewa wakati wa ufungaji wa maonesho ya OSHA kitaofa jijini Dodoma tarehe 28 Aprili,2022. Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Patrobas Katambi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wanyeulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo ya mshindi wa pili Sekta za Fedha katika maadhimisho ya Usalama na afya Mahala pa Kazi iliyokwenda kwa Benki Benki ya CRDB ambayo ilipokelewa na Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki hiyo, Misana Mutani. Tuzo hiyo pamoja na ile ya Mshindi wa Jumla wa Huduma za Jamii ya OSHA zilitolewa wakati wa ufungaji wa maonesho ya OSHA kitaofa jijini Dodoma tarehe 28 Aprili,2022. Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Patrobas Katambi.
Wananchi mbalimbali waliotembelea Banda la Benki ya CRDB katika maonesho ya OSHA wakipata huduma katika banda hilo.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts (wapili kulia) akiongozana na Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki ya CRDB, Misana Mutani (kulia) wakipata maelezo ya huduma mbalimbali za usalama na afya mahala pa kazi katika banda la Benki ya CRDB.

Meneja Uangalizi Majengo wa Benki ya CRDB, Elia Mnonjela (kushoto) akizungumza na wateja waliotembelea Banda la benki hiyo lililopo katika Maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete.
Afisa wa Usalama na Afya mahala pa kazi wa Benki ya CRDB, Narsisa Kasinde (kushoto) akizungumza na wateja waliotembelea Banda la benki hiyo lililopo katika Maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete.

Meneja Uangalizi Majengo wa Benki ya CRDB, Elia Mnonjela (kushoto) akizungumza na wateja waliotembelea Banda la benki hiyo lililopo katika Maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete.
Mgeni Rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akiwa katika picha ya pmoja na Maofisa wa Benki ya CRDB.

**********Benki ya CRDB imeibuka mshindi wa tuzo mbili za masuala ya usalama na afya mahala pa kazi wakati wa kilele cha madhimisho ya Usalama na Afya mahala pa kazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma leo tarehe 28 April, 2022.


Tuzo hizo za sekta bora ya fedha inayozingatia usalama na afya mahala pa kazi na ile ya utoaji huduma za kijamii (CSR) zilizotolewa na OSHA na kukabidhiwa kwa CRDB na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenyeulemavu, Prof. Joyce Ndalichako wakati akifunga maadhimisho hayo.


Maadhimisho hayo yalifanyika sambamba na Maonesho ya huduma mbalimbali za usalama na afya mahala pa kazi ya siku tatu Yenye kaulimbiu “Kwa pamoja tushirikiane kujenga utamaduni bora wa usalama na afya mahali pa kazi” yalifunguliwa rasmi tarehe 26 April ikiwa ni utekelezaji wa sera na jitihada ya Serikali katika kuhakikisha uhamasishwaji wa Usalama na afya mahali pa kazi unatekelezwa ili kulinda afya na usalama wa wafanyakazi.


Aidha Serikali imekuwa ikishirikiana kwa pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika masuala yote yanayohusu kazi na ajira. Kwa kutambua hilo Benki ya CRDB imekuwa mdau kwa kuipa kipaumbele sera ya afya na usalama mahali pa kazi kwakushirikiana na OSHA ambao ndio wasimamizi wa mpango huo.


Akizungumza katika maonesho hayo baada ya kukabidhiwa tuzo hizo, Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki ya CRDB, Misana Mutani alisema, kuongezeka kwa vifaa vya digitali na matumizi ya teknolojia kumebadilisha kabisa mazingira ya kazi hususani kuongezeka kwa vihatarishi mahali pa kazi. Uchafuzi wa mazingira kutokana na baadhi ya shughuli za uzalishaji Viwandani, Migodini na baadhi ya shughuli nyingine za binadamu umesababisha mabadiliko ya tabia nchi.

“Mahitaji ya dunia yanayotokana na utandawazi yamepelekea kuwepo na idadi kubwa ya wafanyakazi wanaofanya kazi kwa saa nyingi kuliko kawaida na matumizi ya vifaa vya kieletroniki, hivyo kwa kulitambua hilo, Benki ya CRDB imekuwa ikilipa kipaumbela swala la afya na usalama kazini,” alisema Mutani.


Mutani amesema Benki imekuwa ikiendesha program mbalimbali kwa wafanyakzi Tanzania nzima ikiwa ni pamoja na upimaji wa afya kwa wafanyakzazi wote kila mwaka, uwepo wa siku ya Afya ya Benki ya CRDB “CRDB Bank Wellness Day” inayofanyika kwa matawi yetu yote, lakini pia kuwa na Chumba maalumu cha huduma ya kwanza, Chumba cha akina mama na watoto (Lactation Room) pamoja na uanzishwaji wa mfuko wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.


“Mustakabali wa kazi hasa wakati nchi yetu inaendelea kujenga uchumi wa viwanda na kuelekea uchumi wa kati na ukuaji wa haraka wa teknolojia inayotumika katika viwanda na maeneo mengine ya kazi kunagusa moja kwa moja afya na usalama wa wafanyakazi,” alisema Mutani.


Katika juhudi za kupambana na hali hiyo kwa sasa duniani kote msisitizo umekuwa ni kuhamasisha kazi kijani (green jobs) na viwanda vinahimizwa kupunguza hewa ukaa hali ambayo itasaidia kupunguza vihatarishi sehemu za kazi na hatimaye kupunguza madhara ya kiafya kwa wafanyakazi.


“Muhimu sana kwa sasa kuliko wakati wowote kuanza kutambua vihatarishi vipya katika maeneo ya kazi. Kutambua vihatarishi hivyo ni hatua muhimu ya kwanza kabisa itakayopelekea kuweka mikakati ya kuzuia vihatarishi hivyo ili wafanyakazi wasipate ajali na magojwa yatokanayo na kazi,” alisema Mutani.


Ajali na magonjwa yatokanayo na kazi ni mambo ambayo yanaweza kuzuilika kwa kuwa vyanzo vyake vinaweza kutambulika na kuonekana tangu mapema kama tutakuwa makini. Ili kutambua vyanzo hivyo Benki yetu ya CRDB imeona uwepo wa umuhimu wa kujenga utamaduni wa masuala ya afya na usalama mahali pa kazi miongoni mwa jamii.


Katika kujenga utamaduni wa kuzuia vihatarishi sehemu za kazi ni wakati muafaka sasa kwa nchi yetu kuingiza masuala ya afya na usalama kazini”. Alisema Misana.


Benki ya CRDB imeshiriki maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kiwete Convation Centre, Jijini Dodoma. Maonesho yalisimamiwa na kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara cha Benki ya CRDB kilichopo Makao Makuu - Dar es salaam na kushirikiana na wawakilishi wa Osha wa Benki ya CRDB Kanda ya Dodoma. Shughuli mbalimbali zinazohusu usalama na Afya kazini zinazosimamiwa na Benki zilionyeshwa katika Banda la Benki ya CRDB katika viwanja hivyo.
Share:

BARRICK YAIBUKA MSHINDI BORA TUZO ZA WIKI YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI (OSHA)


Wafanyakazi wa Kampuni ya Barrick Tanzania wakifurahia tuzo walizojishindia katika maonesho ya OSHA jijini Dodoma.
 **

Kampuni ya Barrick Tanzania, imeshinda tuzo nane katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ya mwaka 2022 iliyofanyika jijini Dodoma huku Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, ukinyakua Tuzo ya mshindi wa jumla ya kufuata kanuni za Usalama ipasavyo (the Top OSHA Compliance Award).

Mbali na ushindi huo mkubwa, Bulyanhulu, pia iliibuka kidedea kwa kushinda Tuzo za kuelezea kwa ufasaha shughuli za kampuni, na ushindi wa jumla wa mshiriki wa maonesho na katika kipengele cha Ubunifu katika uchimbaji wa Madini katika maonesho ya OSHA ya mwaka huu.

Kwa upande wa Mgodi wa Barrick North Mara, ulishinda Tuzo za juu katika Mpango Bora wa uhamasishaji kanuni za Afya na Usalama na wadau wake na imeshinda kipengele cha Huduma za Usalama. Pia ilikuwa Mshindi wa pili katika kipengele cha uhamasishaji kuzingatia Usalama kwa Wajasiriamali Wadogo (SMEs) na Tuzo la OSHA katika Sekta ya Madini.

Maonesho ya mwaka huu ya OSHA yalifanyika katika Viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mjini Dodoma. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mheshimiwa Profesa Joyce Lazaro Ndalichako, alikuwa mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za mwaka huu.

Ushindi wa Barrick Tanzania wa mwaka 2022 unatokana na mafanikio ya kampuni ya 2021 ambapo ilipata ushindi wa jumla wa Tuzo za Utekelezaji wa Majukumu ya kusaidia Jamii (CSR),Mshiriki Bora katika maonyesho na Tuzo ya Ubunifu katika Usalama na Afya (OHS Innovation).

Akiongea baada ya hafla ya utoaji wa Tuzo hizo, Meneja wa Barrick Tanzania, Georgia Mutagahywa alisema, "Huu ni wakati mzuri kwa Barrick kwa ushindi wa Tuzo hizi ambao unadhihirisha kazi kubwa inayofanywa na Wafanyakazi wetu na Washirika wetu kibiashara ili kuifanya Kampuni kuwa mahali salama na pazuri pa kufanya kazi.

"Usalama ni suala kuu tunalolipa kipaumbele cha kwanza, hivyo tumejitolea kufanya kila kuweka mifumo itakatayofanikisha kusiwepo na matukio ya kujeruhiwa katika maeneo yetu ya Kazi", alisema Mutagahywa”.

 Tuzo hizi ni ushuhuda wa dhamira ya Kampuni ya kuhakikisha kanuni za usalama zinatekelezwa na kuzingatiwa wakati wote na Wafanyakazi , Washirika na Wadau wake.

Afisa Afya wa mgodi wa Bulyanhulu,Dk. Said Kudra, akipokea Tuzo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mheshimiwa Profesa Joyce Lazaro Ndalichako (kushoto) katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Patrobas Katambi.
Afisa Afya wa mgodi wa Bulyanhulu,Dk. Said Kudra,akifurahia tuzo na baadhi ya wafanyakazi wenzake.
Wafanyakazi wa Mgodi wa North Mara wakifurahia Tuzo walizojishindia katika maonesho ya OSHA jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu wakifurahia tuzo walizojishindia katika maonesho ya OSHA jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Barrrick walioshiriki maonesho ya OSHA wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Kampuni kushinda Tuzo
Share:

DKT.MPANGO AWASILI NCHINI KENYA KUMUWAKILISHA RAIS KATIKA MAZISHI YA HAYATI MWAI KIBAKI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Aprili 2022 akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta uliopo Nairobi nchini Kenya alipoenda kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Kenya ,Hayati Mwai Kibaki. Makamu wa Rais ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM-Bara) Komredi Abdulrahman Kinana
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger