Thursday 29 February 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 1, 2024



Share:

HAKUNA MTU ATAKAYEKOSA MATIBABU, MKATABA BAINA YA NHIF NA APHFAT HAUJAVUNJWA - Dkt. SAGWARE

Mwenyekiti wa Kamati ya kupitia kitita cha mafao cha NHIF 2023 Dkt. Baghayo Saqware akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 29,2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya kupitia kitita cha mafao cha NHIF 2023 Dkt. Baghayo Saqware akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 29,2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya kupitia kitita cha mafao cha NHIF 2023 Dkt. Baghayo Saqware akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 29,2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Kamati ya kupitia kitita cha mafao cha NHIF 2023 Dkt. Baghayo Saqware amesema maamuzi ya ujio wa Kitita hicho ni matokeo ya makubaliano ya pande zote ambazo ni watoa huduma binafsi za Afya na BAKWATA kwa maslahi ya serikali na sekta binafsi.

Akizungumza leo Februari 29,2024 Jijini Dar es Salaam, Dkt Saqware amesema hakuna atakayekosa huduma ya matibabu kwa kuwa mkataba baina ya mfuko na watoa huduma za afya wa sekta binafsi (APHTA) haujavunjwa.

“Kamati ilikuwa huru kumsikiliza kila mtu, tulikubaliana kwa pamoja na tuliamua kitita kianze kutumika kwa faida ya nchi na taasisi zetu.

“Kwahiyo tunapenda kutoa msimamo wa kitaalam kwamba Wizara kupitia NHIF iendelee na utekelezaji wa kitita cha mafao kilichoboreshwa cha NHIF cha mwaka 2023 kama ilivyoshauriwa na kamati,” amesema Dk Saqware.

Aidha amesema kuwa mapendekezo ya kamati ya wataalam ni pamoja na kuanza kutumika kwa kitita cha mafao cha mwaka 2023 pamoja na maboresho yaliyopendekezwa na kamati katika sehemu ya ada ya ushauri na kumuona daktari, huduma za dawa, upasuaji na vipimo.

Sambamba na hilo amesema Kitita kinachotumika hivi sasa kilifanyiwa maboresho kwa mara ya mwisho mwaka 2016 hivyo Mfuko umelazimika kufanya mapitio katika Kitita hicho ili kwenda sambamba na mahitaji yaliyopo na hali halisi ya utoaji wa huduma za afya nchini.

Share:

TEAM FEBRUARY SHINYANGA YATOA MSAADA KITUO CHA MALEZI YA WATOTO ST. JOHN BINGEN HOME OF CHILDREN

Kikundi cha Team February cha mkoani Shinyanga kimefanya matendo ya huruma kwa kutoa msaada katika kituo cha malezi ya watoto Saint John Bingen Home of Children ilichopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Wametoa msaada huo leo February 29, 2024 katikakituo cha malezi ya watoto Saint John Bingen Home of Children kilichoo kata ya Mwadui wilayani Kishapu.

Akitoa shukrani mara baada ya kukwa kupatiwa msaada huo msimamizi wa kituo cha malezi Saint John Bingen Home of Children Esta Livision amewashukuru Team February kwa kuwakumbuka watoto wenye uhitaji katika kituo hicho.

"Kituo cha malezi ya watoto Saint John Bingen kilianzishwa mwaka 2022 kikiwa na watoto watano ambapo mkapa sasa tuna watoto 39, malengo ya kituo chetu ni kuhakikisha watoto wote wanapata elimu, changamoto ni nyingi kama vile mahitaji mbalimbali ikiwemo mafuta maalum ya kujipaka kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi, mashine ya kufulia nguo, mavazi, vifaa vya kujifunzia ikiwemo daftari pamoja na mahitaji mengine,"amesema Esta Livision.

"Awali tulikuwa na tv mmoja tu ambayo tulikuwa tukitumia kuangalia watu wote tunashukuru kwa hiki mlichotupatia ni moyo wa upendo mliouonesha kwa watoto hawa kupitia sadaka hii MUNGU akawabariki sana, zipo sehemu nyingi zenye uhitaji lakini mmetuona sisi, tunashukuru sana", ameongeza Esta Livision.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Team February Eva Chaulema amesema moja ya jukumu la umoja wa kikundi hicho ni kusaidia, kushirikiana na kuungana na jamii kwenye mambo mbalimbali sambamba na kusherehekea mfano wa siku ya kuzaliwa kwa pamoja na wale waliozaliwa mwezi wa pili.

"Sisi kama Team February kwa umoja wetu tumefika katika kituo hiki kwaajili ya kujumuika na kusherehekea pamoja na watoto wetu, ni moja ya jukumu letu kuungana na kuisaidia jamii lakini pia kusherehekea pamoja katika mwezi huu wa pili, tunawakabidhi Flat Screen inchi 43 pamoja na king'muzi cha Azam Tv kwa lengo la kusherehekea pamoja", amesema Eva Chaulema.


Team February wakikabidhi msaada kwa watoto wa Kituo cha malezi ya watoto Saint John Bingen.



King'amuzi kilichotolewa na Team February kwa watoto wa Kituo cha malezi ya watoto Saint John Bingen.








Picha ya pamoja.




Picha ya pamoja.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger