Sunday, 25 February 2024

SAGINI AFIKA ENEO LA AJALI ILIYOUA WATU 25 ARUSHA...ATOA MAELEKEZO JESHI LA POLISI

...
 
Na. Abel Paul, Jeshi la Polisi- Arusha
 
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimimiwa Jumanne Sagini amefika Jijini Arusha na kukagua eneo la ajali lilotokea Februali 24, 2024 katika barabara ya Arusha - Namanga, Eneo la Ngaramtoni kibaoni Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
 
Mhe Jumanne Sajini Pamoja nakutoa pole kwa wahanga wa ajali hiyo, amelitaka Jeshi la Polisi kuweka mikakati madhubuti ya ukaguzi wa magari yanayotoka nje ya nchi  pamoja na yale yaliyopo ndani ya nchi pasipo kusubiria wiki ya nenda kwa usalama ili kuepuka ajali zinazoweza kujitokeza kutokana na uzembe wa madereva ama ubovu wa magari.
 
Aidha Mheshimiwa Sagini ametoa Pongezi kwa Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Wa Arusha Mount
Meru, Madaktari, wauguzi pamoja na Jeshi la Polisi na kwa namna walivyotoa huduma bora kwa majeruhi waliopata ajali siku ya jana.
 
Amefafanua kuwa ajali hiyo imehusisha raia wa kigeni kutoka nchi za Marekani, Afrika kusini, Nigeria, Togo, Bukinafaso, Madagasca na Kenya.
 
Pia ametoa salamu za Pole toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa watanzania hususani wananchi wa Mkoa wa Arusha kufuatia ajali hiyo.
 
Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP. Awadh Juma Haji amesema amepokea maelekezo yalitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi na kuahidi kuwa watayafanyia kazi ili kuhakikisha watumiaji wa barabara wanafuata sheria za usalama Barabarani ikiwemo watembea wa Miguu ili kuhakikisha wanafuata sheria zilizowekwa.
 
CP Awadhi amesema kuwa katika kuhakikisha wanatokomeza ajali tayari Jeshi hilo limeingia makubali ya shirika viwango Tanzania (TBS) ili kutumia vifaa vya kisasa katika ukaguzi wa vyombo vya moto.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger