Sunday 31 May 2020

Video kali : BAHATI BUGALAMA - UTAFUTAJI


Hii hapa ngoma mpya ya Msanii Bahati Bugalama inaitwa Utafutaji..Itazame hapa chini


Share:

Tazama Video : GUDE GUDE - SIRI YA MAISHA


Hii hapa ngoma ya Msanii wa Nyimbo za asili Gude Gude inaitwa Siri ya Maish..
Tazama hapa chini
Share:

AWAMU YA PILI YA WATANZANIA WALIOKWAMA INDIA KUTOKANA NA UGONJWA WA CORONA WAREJEA NCHINI


Serikali yarejesha kwa awamu ya pili Watanzania 192 waliokuwa wamekwama nchini India kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.

Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Tanzania [ATCL] pamoja na Diaspora wa Tanzania nchini India kwa mara nyingine wamefanikisha safari ya pili ya kuwarejesha nchini Watanzania 192 waliokuwa wamekwama katika miji mbalimbali nchini India. 

Watanzania hao walikwama kutokana na zuio la kuingia na kutoka kwa ndege za Kimataifa lililowekwa na Serikali ya India kama hatua mojawapo ya kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.

Ndege maalum ya aina ya Boeng 787-8 ya Dreamliner ya Shirika la Ndege la Tanzania ilitumwa tena na Serikali Jijini Mumbai kuja kuwachukua Watanzania hao waliokwama nchini India tangu tarehe 22 Machi 2020 lilipowekwa zuio hilo na Serikali ya India. 

Ndege hiyo iliondoka tarehe 30 Mei 2020 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji,  Mumbai ikiwa imebeba jumla ya raia wa Tanzania 192, miongoni mwao ni waliokuwa wamekwenda India kwa ajili ya matibabu; wahitimu kutoka vyuo mbali mbali na wanafunzi ambao wanalazimika kurudi nyumbani kwa kuwa vyuo vimefungwa hadi mwezi Agosti/Septemba 2020.

Tofauti na awamu ya kwanza, safari hii pia ilihusisha kuwarejesha nchini India raia wa nchi hiyo wapatao 202 ambao walikuwa wamekwama nchini Tanzania. Hatua hii ya Serikali ya Tanzania itasaidia sana katika kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya India na Tanzania.

Mpaka sasa jumla ya Watanzania 438 wamerejeshwa Tanzania kutoka India kwa utaratibu huu maalum.


Share:

Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya Nane (08)

Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA
Akaning’inizwa hewani huku mikono yake ikiwa imechanuliwa mithili ya Yesu alivyo sulubiwa msalabani. Wapelelezi hao wakamwagia maji mwilini mwake, kisha mmoja wao ahachukua nyaya mbili za umeme, zenye hasi na chanya. Akazigusanisha na zikaanza kutoa cheche cheche, zilizo mfanya Tomas kujawa na mshangao hata kabla ya kupachikwa na nyaya hizo mwilini.
“Ukijibu kwa usahihi basi adhabu hii huto ipata. Ila ukijiu kwa jeuri basi adhabu hii utakumbana nayo.”
Kauli ya mpelelezi ikamfanya Tomas macho kumtoka huku akiwa haelewi ni kosa gani lililo mfanya kukumbana na shurba zote hizo.
“YUPO WAPI NABII SANGA”   
Mapigo ya moyo ya Tomas yakaanza kumdunda kwa kasi sana kwani hakutarajia kwamba, mpango wa siri alio upanga yeye na mrs Sanga utajulikana kirahisi namna hiyo.


ENDELEA
“Mi……mi sijui”
Tomas alizungumza kwa kubabaika. Kutokana na utaalamu walio nao wapelelezi hawa. Wakatambua kabisa jibu la Tomas si la kweli. Mpelelezi aliye shika nyaya hizo za umeme, akazipatichika kwenye mbavu za Tomas na kumfanya aanze kutetemeshwa huku akipiga mayowe makubwa yatokanayo na maumivu hayo makali sana.
“Ni wapi mulipo muhifadhi nabii Sanga?”
“Nitasema nitasema”
Tomas alizungumza huku machozi yaliyo ambatana na mkojo vikianza kumchurukika kwa pamoja.
                                ***
“Hapa panatosha. Chukua hii kofia uvae ili watu wasiweze kukugundua.”
Rama D alizungumza huku wakilisimamisha gari lao karibu kidogo na stendi ya Mkinga. Nabii Sanga akachukua kofia nyeusi aliyo pewa na akaivaa.
“Hakikisheni kwamba muna fanya kile nilicho waeleza muweze kufanya”
“Sawa tutafanya hivyo”
Magreth akafunguliwa kitambaa machoni mwake na wakashuka na nabii Sanga kwenye gari hilo. Rama D na wadogo zake wakawasha gari na kurudi porini huku wakiwa wamejawa na furaha ya kupata kiasi kikubwa sana cha pesa.
“Upo salama baba?”
Magreth aliuliza huku akimtazama nabii Sanga mwilini mwake.
“Ndio. Ulicho kiona na ulicho kisikia hakikisha umuambii mtu”
“Sawa baba sinto fanya hivyo”
“Inabidi tutafute usafiri wa kurudi Dar”
“Nimekuja na dereva taksi, acha niwasiliana naye”
Magreth akampigia Sheby, baada ya sekunde kadhaa Sheby akapokea simu.
“Sheby, mimi Mage”
“Niambie upo wapi?”
“Nipo karibu na sheli hapa stendi”
“Poa ngoja nina kuja hapo kwa maana nilikuwa nimepitiwa na ka usingizi”
“Poa poa”
Sheby akawasha gari lake na kuelekea eneo ilipo sheli na kuwakuta Magreth na mwanaume ambaye hakuweza kumfahamu, hii ni kutokana na uvaaji wake wa kofia ulio ificha sura yake. Wakaingia kwenye taksi hiyo, na wote wawili wakakaa siti ya nyuma.
“Tunarudi Dar ehee?”
Sheby alizungumza huku akitazama nyuma kwa kupitia kioo kilichopo pembeni yake.
“Ndio”
Magreth alijibu kwa ufupi.
“Poa”
Safari ikaanza huku ndani ya gari ukimya ukitawala. Nabii Sanga hakutamani hata kufungua kinywa chake, hii ni kuhofia sauti yake kujulikana na dereva taksi huyo. Majira ya saa saba usiku wakaingia jijini Dar es Salaam. Moja kwa moja wakaelekea nyumbani kwa Magreth.
“Hivi Sheby ni wapi sasa hivi watakuwa hawajafunga vibanda vya chipsi?”
“Zipo sehemu nyingi mbona”
“Basi ngoja nimpeleke mgeni wangu ndani. Nisubiri hapa tukachukue wote”
“Sawa bossi”
Magreth na nabii Sanga wakashuka kwenye gari hilo na kuingia ndani ya nyumba hiyo iliyopo uswahilini. Magreth akafungua mlango wa chumbani kwake na wakaingia ndani, pasipo mpangaji mwezake yoyote kugundua juu ya ugeni wa nabii Sanga.
“Hapa ndio kwangu jisikie huru”
“Nashukuru Magreth”
“Basi ngoja nikachukue chakula. Si unatumia chipsi za huku kwetu”
“Una maanisha nini ukisema huku kwenu?”
“Uswahilini, si unajua kuna utaofauti na zile chipsi za kwenye migahawa mikubwa mikubwa?”
“Wewe lete chakula chochote nitakula”
“Sawa”
Magreth akaliweka begi lake sehemu alipo litoa, kisha akatoka ndani humo na kurudi kwenye taksi.
“Mage wewe muongo”
“Kwa nini?”
“Uliniambia kwamba huna mtu”
“Hembu kumbuka vizuri”
“Ndio, nilikuuliza tunakwenda Mkinga kwa jamaa yako. Ukasema hapana, ona sasa umerudi na mtu wako. Yaani umenifanya njia nzima nikae kimya nishindwe hata kupiga stori”
“Hahaa woga wako tu.Twende bwana tukachukue chakula”
Magreth na Sheby wakaondoka eneo hili na kuelekea kwenye kibanda cha Masawe anaye sifika kwa kupika chipsi nzuri sana na ana wateja wengi wanao mfanya kila siku afunge kibanda chake saa kumi usiku au saa kumi na moja alfajiri.
“Na wewe uta kula chipsi na nini?”
Magreth alimuuliza Sheby anaye onekana kuchoka kiasi fulani.
“Chipsi kuku”
“Nakununulia wewe na mke wako. Hakikisha mtoto wa watu unampeleka hichi chakula. Nina imani atakuwa amekupigia simu urudi nyumbani ukale, ila ndio hivyo ulikuwa mbali”
“Sawa mama”
Magreth akashuka kwenye gari hilo, kutokana ana fahamiana na Massawe. Ikamuwia urahisi kuhudumiwa kwa haraka na kuondoka. Wakarudi nyumbani, Magreth akamuongezea Sheby kiasi cha shilingi elfu ishirini, wakaagana na yeye akaingia ndani.
Magreth akastuka kidogo mara ya kumkuta nabii Sanga akiwa na boksa tu huku amelala chali kitandani. Nabii Sanga aliye jawa na mawazo kichwani mwake, kumemfanya asitambue uwepo wa Magreth ndani humo. Magreth aliye anza kupepesa macho akijikaza asimtazame nabii Sanga. Akamsogelea na kushika mkono na nabii Sanga akastuka kidogo.
“Nimerudi.”
“Ohoo sawa sawa”
Magreth akachukua taulo na kumkabidi nabii Sanga huku akiwa ametazama pembeni. Kwani haitaji kabisa kuona maungo ya chini ya mtu anaye muheshimu kama baba yake. Nabii Sanga akajifunga taulo hilo na kumpa amani Magreth.
“Toka jana sikuweza kutia kitu chochote mdomoni mwangu”
“Pole sana baba”
“Mage”
“Bee”
“Ukiwa nami naomba usiniite baba wala nabii”
“Aha…a…ha…Kwa nini?”
“Niite tu Sanga peke yake, sinto pendelea ukitese kinywa chako kwa kuita jina refu”
“Ila baba hivi ndivyo nilivyo zoea na ninakupa cheo chako kutokana na mambo makubwa ambayo Mungu ana endelea kutufunulia juu yako”
“Sawa nina litambua hilo, ila tafadhali fanya hivyo nilivo kueleza”
“Nitajitahidi”
Magreth akaandaa chakula na wote wakaanza kula huku nabii Sanga kwa mara kadhaa ana endelea kutazama uumbaji wa Mungu alio ufanya juu ya Magreth. Ila Magreth kichwani mwake ana waza ni jinsi gani ambavyo anaweza kumkabidhi nabii Sanga ushahidi wa video unao onyesha uchafu wa mke wake pamoja na Tomas.
                                ***
Tomas hakutamani nyaya hizo ziweze kurudishwa tena mwilini mwake. Ila kitu cha pekee ambacho ana jitahidi kukificha ni ushirikiano wake na mrs Sanga.
“Ni wapi?”
Mpelelezi huyo alimuuliza Tomas kwa upole huku akimtazama usoni mwake. Kabla ya Tomas kujibu RPC akaingia katika chumba hicho, huku akiwa ameongozana na body gard wake.
“Mume fikiwa wapi vijana?”
“Ana hitaji kutaja ni wapi walipo wezake.”
“Tunakusikiliza wewe kenge. Sema wapi alipo nabii Sanga?”
RPC alizungumza kwa ukali na kumfanya Tomas kuanza kuzungumza ni eneo gani walipo wezake.
“Wasiliana na RCO wa Handeni. Aniandalie vijana wanne, wakakamavu na wenye uwezo mkubwa. Nyinyi mutaongoza timu ya askari nane kuelekea msituni huko.”
“Sawa mkuu”
“Kamera mliyo piga picha ipo wapi?”
“Hii hapa mkuu”
“Nenda kazisafishe picha hizo sasa hivi”
RPC alimueleza body gard wake huku akiipokea kamera hiyo na kumkabidhi kijana wake.
“Sawa mkuu”
“Kikosi hicho hakikisheni kwamba nina onana nacho sasa hivi na wawe vijana mashupavu”
“Sawa mkuu acha nikiandae kikosi”
“Haya. Nahitaji kusikia mazungumzo ya mwisho ya huyu kijana aliyo yafanya kwenye simu yake. Niunganishe na kurugenzi wa mtando wa simu anao utumia ili tuweze kutumiwa mazungumzo yake ya mwisho”
“Sawa mkuu”
Tomas akashushwa kwenye minyororo hiyo huku mwili mzima ukiendelea kumtetemeka kwa woga na maumivu makali aliyo yapata.
    Akavalishwa nguo zake na kutolewa katika chumba hicho cha mateso na kuwekwa chumba cha mapumziko kabla ya kuchukuliwa na kuongozana na askai hao kuelekea Handeni.
RPC akazungumza na mkurugenzi wa mtandao wa simu anao utumia Tomas na akatumiwa mazungumzo ya mwisho na watekaji na ushahidi huo ukazidi kumuweka Tomas sehemu mbaya kisheria. Simu inayo pigwa kila mara kwenye simu ya Tomas kukamfanya RPC kuendelea kuzikata simu hizo kwani namba hiyo imeandikwa kwa jila na Mke wangu.
“Kijana mshenzi huyu ana mke alafu ana fanya mambo ya ajabu”
RPC alizungumza huku akiizima simu hiyo. Akaingia katika chumba cha silaha na kuwakuta vijana wake wakiwa wana jiandaa.
“Tusikilizane”
Kila askari akaacha kazi aliyo kuwa ana ifanya na kusimama wima mithili ya mlingoti ili kumsikiliza mkuu wao.
“Mna kwenda kwenye oparesheni hatari sana. Msitu huo ni mithili ya misitu iliyopo Kibiti. Hakikisheni kwamba mna kuwa makini sana kwa kila jambo ambalo mna lifanya.”
“Akikisheni mna muokoa nabii Sanga akiwa hai. Ila ombi langu ni moja tu. Musiache pumzi ya ya jambazi yoyote, hata ikitokea wame jisalimisha. Hakikisheni kwamba mna waua sawa”
“Sawa afande”
“Mtaongozana na huyo kijana Tomas. Hakikisheni mna rudi naye akiwa hai na gereza lita muhusu, ili iwe fundisho kwa vijana wengine wote. Udalali wake kumbe si kwenye nyumba tu, hadi kwa watu”
“Niwatakie kazi njema na mapambano mema”
“Shukrani mkuu”
Askari hao wakapiga saluti na RPC akatoka ndani humo na kuwaacha vijana wake wakiendelea kujiandaa. Kikosi hicho cha askari nane walio valia mavazi meusi, huku wote wakiwa wamejikamilisha kwa mapambano, wakaingia kwenye gari nne aina ya Toyota land cruzer zenye rangi nyeusi na kuianza safari ya kuelekea Mkinga, Handeni, huku Tomas akiwa miongoni mwa walio ndani ya magari hayo, tena chini ya ulinzi mkali sana.

                                ***
    Kitendo cha Tomas kuto kupoekea simu yake na kuizima kabisa, kikazidi kumchanganya Mrs Sanga. Namba yake ya siri aliyo iweka hewani, ndio anayo itumia kuwasiliana na Tomas.
“Amekumbwa na nini baby wangu?”
Mrs Sanga ali haha huku akiendelea kuzunguka zunguka ndani ya chumba hicho. Mlango wa chumbani kwake ukagongwa, akastuka sana huku akiutazama. Saa yake ya mkononi ina onyesha muda huu ni saa saba usiku.
“Nani?”
Mrs Sanga alizungumza huku akiutazama mlango huo.
“Ni mimi”
Sauti ya mkuu wa polisi wa kikosi kinacho mlinda yeye na familia yake, ikamstua sana. Mrs Sanga akajifunga tenge na kutoka ndani humo.
“Samahani mama kwa kukuamsha wakati huu”
“Bila samahani”
“Tunaweza kushuka sebleni mara moja”
“Kuna nini?”
“RPC yupo hapa”
“RPC!!?”
“Ndio”
“Sawa nina kuja”
Mrs Sanga akarudi ndani kwake huku mawazo ya kwa nini ameitwa muda huu yakiwa yamemtawala sana kichwani mwake. Akaitoa laini hiyo ya siri na kuiweka katika pochi yake. Akaweka laini yake ya kawaida. Akavaa suruli na tisheti kisha akatoka ndani humo. Akafika sebeleni na kumkuta RPC akiwa na vijana wake sita wenye bunduki. Uwepo wa mzee huyo kidogo uka mstua.
“Ahaa kwema jamani?”
Mrs Sanga aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka.
“Kwema, karibu unaweza kukaa tukazungumza mama”
RCP alizungumza huku akimkazia macho Mrs Sanga.
“Vijana wangu kwa sasa wapo njiani wana kwenda kwenye oparesheni ya kumkomboa mume wako. Tunashukuru sana kwa kuweza kutusaidia kumkamata mmoja wa watu walio mteka mume wako.”
Kauli ya RPC ikaufanya moyo wa mrs Sanga kumdunda mfululizo, huku moyo huo ukipoteza muelekeo wake wa kudunda.
“U…u…m….e…sema U…me….me..mkamata nani?”
Mrs Sanga alizungumza kwa kubabaika.
“Mtekaji wa mume wako.”
RCP akampa ishara kijana wake mmojaa kuweka bahasha ya rangi ya kaki, aliyo ishika mezani hapo.
“Fungua”
Mrs Sanga taratibu huku akitetemeka akaichukua bahasha hiyo. Akachungulia ndani ya bahasha hiyo na kukuta lundo la picha. Taratibu akazitoa picha hizo, Mrs Sanga alipo inaona sura ya Tomas akishuka kwenye gari lake, akahisi mwili mzima ukiishiwa nguvu, ubaridi mkali ukamtawala na kujikuta akiziangusha picha hizo na kuwafanya askari wote kumshangaa.
                            ITAENDELEA
Haya sasa, kitendo cha kuangusha picha hizo kitaleta picha gani kwa askari? Je Magreth ata weza kumpa nabii SANGA ushahidi wa video hiyo iliyomo kwenye simu yake? Nini kitatokea? Endelea kufaatilia kisa hiki cha kusisimua, usikose sehemu ya 09


Share:

Uchimbaji Holela Wa Madini Unachangia Kuharibu Uoto Wa Asilina Misitu Iliyohifadhiwa Kisheria

SALVATORY NTANDU
Imebainishwa kuwa shughuli za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika Machimbo mbalimbalI ya dhahabu  Wilayani Mbogwe mkoani Geita unachangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa Misitu iliyohifadhiwa  kutokana na ukatiji holela wa magogo yanayotumika katika ujenzi wa Maduara pindi yanapoibuka  maeneo mapya ya Uchimbaji.

Kauli hiyo imetolewa  Mei 30 Mwaka huu na  Mhifadhi Misitu wa wilaya ya Mbogwe, Ezekiel Mbilinyi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na hatua zilizochukuliwa kuhusiana na watu wanaojihusisha na vitendo vya ukataji misitu bila ya kuzingatia sheria za nchi.

Alisema sheria kali zimeanza kuchukuliwa kwa baadhi ya wachimbaji wanaobainika kujihusisha na vitendo vya uvunaji holela wa miti iliyopo katika maeneo ya misitu inayosimamiwa na wakala huo ili kuhakikisha  ukataji miti   hauhusiwi katika maeneo yaliyohifadhiwa kisheria.

“Kuibuka kwa migodi mipya ya madini katika wilaya hiyo  imekuwa ikisababisha uharibifu wa Mazingira kwani maeneo mengi yameanza kuwa wazi kutokana na uvunaji halolela wa Magogo (matimba) jambo ambalo lisipochukuliwa hatua za dharura linaweza kusababisha maeneo mengi kugeuka kuwa jangwa,”alisema Mbilinyi.

Alifafanua kuwa Wilaya hiyo bado inahazina kubwa ya Misitu ya asili ambayo imetunzwa kwa muda mrefu hivyo ni budi wananchi wakaitunza kwa manufaa yao na kuacha na ukataji miti usiokuwa na tija kwaajili ya mkaa na shughuli za madini na badala yake wajikite katika matumizi ya Mkaa mbadala na uchimbaji wa kisasa usiotumia magogo ya miti.

Sambamba na hilo Mbilinyi aliwaomba wakazi wa vijiji ambavyo vinazungukwa na mapori hayo kuhakikisha wanafanya shughuli mbadala ikiwemo ufugaji wa nyuki  ili kujiongezea kipato kwa kutengeneza mizinga ya kisasa kutokana na maeneo wanayoishi kuwa rafiki  na ni salamaa kwao kwa ufagaji huo.

“Asali iuzwa kwa bei nzuri fugeni nyuki ili muweze kupata  fedha kwaajili kununulia gesi ambayo itakuwa ni mbadala wa mkaa na kuni ambayo ni rafiki wa mazingira,eneo lenu linamisitu na nyuki wapo mnachotakiwa ni kutengeneza mizinga ya kisasa ili muweze kunufaika na biasahara hii ambayo inasoko kubwa,”alisema Mbilinyi.

Mateo Shija ni mchimbaji katika machimbo ya Nyakafulu wilayani humo ameiomba  serikali kupitia wizara ya Madini kuwapatia elimu na vifaa  vya kisasa ambavyo vitawasaidia kufanyashughuli za uchimbaji kwa teknolojia ya kisasa ambayo itaweza kunusuru ukataji wa  miti kwaajili ya shughuli za uchimbaji kutokana na wengi wao kutumia mfumo wa kizamani wa magogo.

Guchonza Makoye mfanyabiashara wa Madini wilayani humo ameiomba serikali kuwapatia vifaa vya kisasa vya uchimbaji kama vile Mitambo ,matrekta,magari na mashine za Gesi ilikuachana  uchimbaji wa kizamani ambao unasababisha wachimabaji wengi kupoteza Maisha kutonana na kufukiwa na vifusi vya udongo pindi mvua zinapoanza kunyesha.

Mwisho.


Share:

‘‘Tuwekeze Kwenye Viwanda Vinavyotumia Malighafi Za Ndani’’- Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amewataka Watanzania kuwekeza katika sekta ya viwanda vinavyotumia malighafi za ndani.

Prof. Shemdoe aliyasema hayo Mkoani Simiyu alipokuwa katika ziara ya siku moja kutembelea Viwanda katika Mkoa huo. Katika ziara hiyo Katibu Mkuu na ujumbe wake walipata fursa ya kutembelea kiwanda kipya cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha cha Bugari Investment Ltd kinachomilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100.

Prof Shemdoe alisema Bw. Bugari ameonyesha umuhimu wa kuwa na malengo katika kutekeleza jambo lolote.

 “ukiwa na malengo unaweza kufanya kitu chochote, hivyo natoa rai kwa watanzania wengine ambao wanaweza kuiga mfano huu  kufika mahali hapa na kujifunza, maana yote yanawezekana ukiweka nia”.

Kiwanda cha Bugari Investment Ltd  kimejengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 2  kinatarajiwa kutoa ajira kwa Watanzania 65 ikiwa ni  ajira za kudumu na za muda pamoja na kuchangia mapato kwa Serikali kupitia kodi mbalimbali.

Prof Shemdoe aliishukuru Serikali ya Mkoa kwa kumpa ushirikiano mwekezaji huyo na kumuwezesha kufanikisha kutimiza azma yake ya kujenga kiwanda. Pia alizishukuru Taasisi za fedha kwa kumuamini na kumpatia mkopo uliofanikisha kujenga kiwanda hicho.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Bw. Festo Kiswaga alisema wananchi wa Simiyu na mikoa ya jirani wamepata uhakika wa soko la alizeti kwa kuwepo kiwanda hicho.

“Tumekuwa tukiwasisitiza wananchi kulima, lakini changamoto iilikuwa upatikanaji wa masoko, hivyo uwepo wa kiwanda hiki utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Mkoa huu na mikoa jirani’’.

Aidha alitoa wito kwa wananchi wa bariadi kuendelea kuzalisha alizeti kwa wingi ili kiwanda kiendelee kupata malighafi ya kutosha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Nkuba Bugari alisema ujenzi wa kiwanda hicho umeanza mwaka 2015 na upo katika hatua za mwisho na ujenzi na kinatarajiwa kukamilika na kuanza uzalishaji mapema hivi karibuni.

Bugari alisema wazo la kujenga kiwanda hicho alipata  baada ya kupata hamasa kutoka kwa Mhe. Rais   Dkt. John Joseph Magufuli alipotoa rai kwa Watanzania kujenga viwanda.

“Ndugu Watanzania wezangu tusiache bahati hii ya kuwa na Mhe. Magufuli, ni kwa namna gani Mhe. Rais anajitoa kwa ajili watanzania katika kufanikisha Tanzania ya Viwanda”.

Anasema mashine zilizofungwa katika kiwanda hicho zina uwezo wa kuchakata mbegu za alizeti, pamba na karanga.

 Aliongeza kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata tani elfu arobaini na nane  za mbegu za alizeti. Hivyo lengo lao ni kushika soko la ndani pamoja kuuza mafuta hayo nje ya nchi ya Tanzania.Aidha aliwasisitiza watanzania kuwa na uthubutu katika kutimiza malengo mbalimbali.


Share:

Rwanda yaripoti kifo cha kwanza cha ugonjwa wa Corona

Wizara ya Afya ya Rwanda imetangaza kifo cha kwanza kilichosababishwa na ugonjwa wa COVID-19 (corona) katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Katika taarifa ya leo Jumapili, wizara hiyo imesema aliyeaga dunia ni dereva wa lori mwenye umri wa miaka 65 na ambaye alikuwa amerejea nchini humo hivi karibuni kutoka nchi jirani ambako alikuwa anaishi.

Taarifa hiyo imesema mtu huyo ameaga dunia akipokea matibabu katika moja ya vituo maalumu vya kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini Rwanda.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Rwanda, watu 359 wameambukizwa virusi vya corona nchini Rwanda kufikia jana Jumamosi ya Mei 30. Aidha idadi ya wagonjwa wa corona waliopata ahueni nchini humo imeongezeka na kufikia watu 250.


Share:

Spika mpya wa Bunge la Iran atoa wito wa kulipa kisasi kwa Marekani

Spika mpya wa Bunge la Iran Mohammad Ghalibaf amesema leo majadaliano yoyote na Marekani hayatokuwa na manufaa na badala yake mkakati wa Iran unapaswa kuwa wa kulipa kisasi na siyo mazungumzo. 

Ghalibaf, kamanda wa zamani wa kikosi cha anga katika jeshi la walinzi wa mapinduzi ametoa matamshi hayo alipokuwa akitoa hotuba ya kwanza mbele ya bunge la Iran . 

Spika huyo aliyechaguliwa hivi karibuni amesema ni lazima Iran ilenge kuondoa uwepo wa majeshi ya Marekani kwenye kanda hiyo na kulipa kisasi kwa kifo cha kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran Qassim Soleimani aliyeuliwa na Marekani mnamo mwezi Januari. 

Kadhalika Ghalibaf ametoa wito kwa serikali kuimarisha mahusiano na mataifa mengine yenye nguvu yaliyo rafiki na Iran ambayo mara zote yamewaunga mkono katika kipindi kigumu.


Share:

Je Wewe Ni Mwanasiasa, Mfanyabiashara, Msanii au Mwanamziki.... Tunazo Dawa Na Pete Za Bahati

Je Wewe ni MWANASIASA, MFANYABIASHARA,
MSANII  wa Maigizo, MWANAMZIKI, ama MWANAFUNZI tunazo dawa na PETE za BAHATI zenye uwezo mkubwa wa Kuyabadilisha MAISHA yako nakukupatia MAFANIKIO MAKUBWA ndani ya mda mfupi tu.
 
Hapa Leo tutazungumzia Pete zenye Bahati na power yani nguvu za ziada na pia ukipata pesa zikae sio kukutoka, na pia zipo Pete zenye nuksi lakini wewe ukiivaa utaiona nzuri kumbe inakufanya Nyota yako kufifia kila kukicha bila wewe mwenyewe kujua maana jini mwenye Pete aina ya Aina kwenye picha itazame kwa makini ina Vito vingapi
 
Pili inatakiwa kuvaliwa mkono gani na kidole kipi piga picha Pete yako nitakwambia jinsi ilivyo na jina lako
 
Kwa wale watu wanao chimba madini pia wana aina za Pete za kuvaa sio Pete ni Pete tu unakuta mtu yupo miaka kumi haja pata kitu nakushauri ipo Pete itakayo kuonyesha njia Rahisi ya mafanikio yako haina masharti hiyo uliyo ivaa ivue iweke kwenye kisahani ipake marashi rose km una biashara iweke kwenye biashara yako

Je kuna mabadiliko ya mauzo au wateja kuja ukiona hakuna mabadiliko uliza nitakusaidia Ila piga picha unitumie aina ya pete uliyo nayo unaweza vaa Pete ya ndoa ukachanganya na pete yenye kito ukaona umependeza kumbe umeongeaza matatizo ktk ndoa yako au mwanaume kulala na wewe na kukuacha bila sababu alikuwa anakusaidia na akaondoka hafla hata kwa wanaume kumchoka mwanamke au mkewe ndani ya nyumba bila sababu yoyote ile Ila akiivuwa nyumba huwa na amani sana.

Pia hata kwa wasanii namaanisha waimbaji pia utakuta mtu anavuma hafla anafifia bila kujuwa nini kimemsibu na nakutafuta kupanda inakuwa tabu anabakia kuongea kuwa amerogwa au amefungwa laa wasanii wengi waimbaji wanakuwa na jini ambae hawamuoni ambae huyo humpa pawa kubwa bila yeye kujitambua.

Pili ni lazima awe na kiti chake ambayo ni pete yenye Power yaani nguvu za ziada kupendwa ila si Rahisi kwa jambo kama hili au  kwa Pete hii kuipata ina siri kubwa sana  utajikuta unaimba mpaka unakata tamaa..

Whatsapp 0744 900180
Sheikh Omary pia ANATOA HUDUMA HIZI
Mrudishe Mpenzi, MUME/MKE Ndani ya Saa 24 tu
Safisha Nyota yako/Mvuto wa Biashara na Mvuto Kazini
Pia Narudisha Mali zilio Dhulumiwa au Kupotea
Pete za Bahati
Zindiko Nyumbani na Biashara
Magonjwa Sugu/Kisukari/Miguu Kuwaka Moto
Nguvu za Kiume
Hutoa Utajili usio Na Masharti


Share:

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUANZA ZIARA MKOANI TANGA KESHO

 MKUU wa Mkua wa Tanga Martine Shigella akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo leo  ambao hawapo pichani kuhusu ziara maalumu ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa itakayoanza kesho Jumatatu

MKUU wa Mkua wa Tanga Martine Shigella akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo kuhusu ziara maalumu ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa itakayoanza kesho Jumatatu mkoani hapa

WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwasili jijini Tanga kesho June Mosi Mwaka huu kwa ziara maalum ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa agizo lake kwa bodi ya Mkonge alilolitoa mapema mwezi machi mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela alisema waziri mkuu anatarajiwa kuzindua Jengo la Bodi ya Mkonge lililopo Jijini Tanga na baadae atatembelea Taasisi ya utafiti ya Mlingano na kukagua vitalu vya zao hilo.


Shigela alisema kuwa ziara hiyo ni mahususi kwa ajili ya kufuatilia maagizo aliyoyatoa machi 1, mwaka huu baada ya kupokea taarifa ya kamati maalum aliyounda kwa ajili ya ufuatiliaji wa mali za bodi ya mkonge.


"Baada ya taarifa hiyo yapo maelekezo aliyoyatoa, hivyo ziara yake hii ni mahususi kwa ajili ya kuja kuona maagizo aliyoyatoa ya ufuatiliaji wa kufufua zao la mkonge na namna ya utekelezaji wa urejeshwaji wa mali ambazo zilitajwa kuwa zilizoporwa kinyume cha utaratibu na sheria" alifafanua.


Aidha Shigela aliwashukuru na kuwapongeza waandishi wa habari mkoani humo kwa namna walivyowajibika na kushirikiana katika nyanja mbalimbali kufanikisha utoaji wa taarifa kwa wananchi kwa urahisi na wakati.


"Niwashukuru sana ninyi waandishi wa habari kwa namna mlivyowajibika katika ile ziara ya waziri mkuu pamoja na kupigania kwa pamoja mapambano dhidi ya corona na kuwatetea wananchi wetu hasa katika eneo la mpakani kule horohoro" alieleza.


Hata hivyo Shigela aliwataka waandishi wa habari kushiriki kikamilifu katika ziara hiyo ya siku moja kwani ziara hiyo inalenga kuleta manufaa kwa mkoa wa Tanga kupitia zao la mkonge kutokana na kwamba ndio zao kubwa linalotegemewa kibiashara.


Alibainisha kwamba ujio wa Waziri Mkuu Majaliwa ni ukombozi kwa mkoa wa Tanga kwani endapo zao la mkonge litafufuliwa na kuimarika mkoani humo wananchi wataweza kujikwamua kiuchumi kutokana na kilimo cha zao.


"Ziara hii kwetu sisi ni ukombozi mkubwa kwasababu zao la mkonge kwa mkoa wa Tanga ndio zao mahususi na ndio zao kuu tunalolitegemea katika mazao ya biashara, na tuna uhakika tukifufua zao letu la mkonge tutakuwa na uhakika wa wananchi wa wananchi wetu kujikwamua katika umasikini" alisema.

Ziara hiyo ya Waziri Mkuu Majaliwa itakuwa na lengo la kufuatilia utekelezaji wa majengo pamoja na mashamba ya bodi ya mkonge yaliyokuwa yamechukuliwa na wananchi kinyemela kwa maslahi yao ambapo baadhi yao kuweka taasisi zao binafsi huku bodi hiyo ikiwa haina ofisi mkoani humo.
Share:

Utaratibu wa Uendeshaji ligi za soka na michezo mingine hapa nchini




Share:

IGP Sirro Awataka Wanaoachiwa Kwa Msamaha Wa Rais Kufuata Sheria Za Nchi

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewataka baadhi ya wananchi ambao ni washtakiwa au wafungwa wanaopata msamaha wa Rais kutoka gerezani, kuacha kujiingiza katika matukio ya uhalifu jambo ambalo nikinyume na sheria za nchi.

IGP Sirro amesema hayo akiwa kwenye ziara ya ukaguzi mkoani Singida ambapo alizungumza na Polisi Kata waliopo kwenye mkoa huo na kuwataka kuendelea kushirikiana na wananchi katika mapambano dhidi ya uhalifu ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuacha kujiingiza kwenye matukio ya uhalifu hususan wa kutumia silaha za moto.

Aidha, IGP Sirro amesema kuwa, wenyeviti wa kamati za Ulinzi na usalama za wilaya na mikoa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kwamba hadi kufikia sasa hali ya usalama nchini imeendelea kuwa shwari.

Naye kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Sweetbert Njewike amesema kuwa, hali ya usalama katika mkoa huo inaendelea kuwa shwari na kwamba matukio ya uhalifu yamepungua kutokana na ushirikiano mkubwa unaotolewa na wananchi pamoja na wadau wengine.


Share:

Mawasiliano ya kidijitali yanavyosaidia kutuleta pamoja

Mawasiliano ya kidijitali yanavyosaidia kutuleta pamoja

Ugonjwa wa korona (COVID-19) umebadili maisha ya watu wengi kwa namna ambazo hatukutegemea.  Moja ya badiliko makubwa ni lile la kupunguza mikusanyiko, kukabaribiana na wengine kuathiri mipango ya safari.

Bahati nzuri teknolojia ya mawasiliano kama mitandao ya kijamii, video calls na nyingine sawa na hizo zimetusaidia kuendelea kuwasiliana huku tukipunguza mikutano na mikusanyiko.

Katika wakati huu, kampuni za mawasilino ya simu nchini Tanzania zimefanya kila jitihada kusaidia wateja wake kuendelea kupata huduma bora za mtandao wa intaneti na mawasiliano kwa ujumla.

Moja ya kampuni hizo ni Tigo Tanzania, moja ya kampuni kubwa za mawasiliano nchini. Huduma ya Tigo Home Internet huwapa wateja wake mtandao wenye kasi na wa kuaminika kuendana na mahitaji yao. Wakati huo huo simu ya Tigo Kitochi 4G yenyewe inawapa wateja waishio kwenye maeneo yenye mtandao wa 4G huduma ya uhakika ya intaneti na kufurahia mitandao kama Facebook, WhatsApp na Barua pepe.

Tigo imesema kuwa inaendelea kufanya kila iwezalo kutoa huduma bora kwa wateja wake. Sasa wateja wa Tigo wanaweza kuwasiliana na huduma kwa wateja kupitia njia mbalimbali zaidi ya kupiga simu kama WhatsApp, Facebook au Twitter.

Katika nyakati hizi za changamoto ya kirusi cha korona kuwa na mawasiliano ya kidijitali yenye uhakika ni muhimu pengine kuliko wakati mwingine wowote ule. Ni jambo jema kwamba kampuni za mawasiliano ya simu kama Tigo zinaendelea kuhakikisha hilo linawezekana.


Share:

Naibu Katibu Mkuu Wizara Ya Elimu Akagua Maandalizi Ya Mapokezi Ya Wanafunzi Mzumbe

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dr. Evamarie Semakafu, ametembelea Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro, kukagua maandalizi ya kuwapokea wanafunzi tarehe 01 Juni 2020, kufuatia tamko la hivi karibuni la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli la kufungua Vyuo Vikuu nchini, baada ya kuvifunga kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 unaotokana na virusi vya Corona.

Aidha, amekagua maandalizi ya ratiba ya masomo, usajili wa wanafunzi unaoendelea, utekelezaji wa agizo la Wizara la kufanya malipo kwa wakati kwa wanafunzi wa mikopo ya Elimu ya Juu inayotolewa na Bodi ya Mikopo Tanzania, pamoja na hatua za tahadhari ambazo Chuo imezichukua hadi sasa kuwakinga wanafunzi na maambuziki ya Corona.

Ameridhishwa na hali katika Kituo cha Afya kinachotoa huduma, ufungaji wa vifaa vya kunawa mikono kabla ya wanafunzi kuingia madarasani, pamoja na elimu ya jumla inayohusu tahadhari binafsi kwa wanafunzi.

Prof. Lughano Kusiluka, Makamu Mkuu wa Chuo; amemhakikishia Naibu huyo utekelezaji wa maagizo yote yaliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kadhalika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto na kwamba kwa zaidi ya asilimia 98% maandalizi yote msingi yamekamilika na tayari wanafunzi wameshaanza kuingia chuoni kwa kuanza masomo Jumatatu 01 Juni 2020.

Dr. Avemarie Semakafu ameonyesha kuridhishwa na hatua za maandalizi na kupongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Chuo hicho, huku akiwataka elimu zaidi kuendelea kutolewa kujikinga na ugonjwa na hasa kwa wafanyakazi na wahadhiri wa chuo hicho.


Share:

Korea Kusini yafunga shule tena baada ya maambukizi kuongezeka zaidi

Zaidi ya shule 200 nichini Korea Kusini zimelazimika kufunga tena shule siku chache baada ya kufunguliwa, kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Mapema Jumatano, melfu ya wanafunzi walirejea shuleni baada ya kufunguliwa tena nchini humo na kulegeza masharti yaliyowekwa awali kukabiliana na virusi vya corona 
 
Lakini baada ya siku moja tu, maambukizi mapya 79 yalirekodiwa, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kwa siku nchini humo kwa kipindi cha miezi 12.

Maambukizi haya mapya yalihusisha watu wa kituo kimoja ambacho kipo nje ya mji wa Seoul.


Share:

Mashauri 4,711 Yasikilizwa Kwa Mahakama Mtandao Kuepuka Corona

Na Magreth Kinabo –Mahakama     
Mahakama ya Tanzania imefanikiwa kuendesha mashauri 4,711 kwa njia ya Mahakama Mtandao maarufu kama ‘Video Conference’ ikiwa ni hatua mojawapo  za kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 1 9 katika kipindi cha miezi miwili.

Mashauri  hayo yamesikilizwa kwa njia  hiyo, kufuatia  utekelezaji wa agizo la Jaji Mkuu wa  Tanzania, Prof. Ibrahim  Hamis Juma alilolitoa Machi 23, mwaka huu la kutumia  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuwaepusha Watumishi wa Mahakama, Magereza, wafungwa na mahabusu na wateja wengine wa Mahakama dhidi ya maambukizo hayo, wakati shughuli za utoaji haki zikiendelea kufanyika.

Agizo hilo lilitolewa na Prof. Juma kupitia mkutano wake na waandishi wa  habari uliofanyika Jijini Mwanza, la kuongeza matumizi ya TEHAMA kwenye kipindi hichi ambacho Tanzania na dunia kwa ujumla  kukumbwa  na janga la ugonjwa huo.

Akizungumzia kuhusu usikilizaji wa mashauri kwa kutumia teknolojia hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Bw. Machumu Essaba alisema imelipunguzia pia Jeshi  la Magereza gharama za usafiri wa kila siku za kuwaleta wafungwa au mahabusu mahakamani na msongamano.

‘‘Njia hii imetumika katika kipindi cha ugonjwa huu, kuanzia Machi 23, mwaka huu  hadi Mei 26, mwaka huu, ambapo Mahakama ya Rufani Tanzania, imesikiliza mashauri 48 kupitia vikao vitano, kati ya hivyo vitatu vilifanyika katika Jiji la Dar es Salaam, vilivyohusisha mashauri 30 na kimoja Tabora kilichohusisha mashauri tisa na kingine Iringa kilichokuwa na mashauri tisa,’’ alisema Essaba.

Alisema  kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania  Kanda ya Dar es Salaam imesikiliza mashauri 3,188 kati ya hayo, mashauri 804 ymesikilizwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mahakama za Wilaya, Kinondoni 714, Ilala 992, Temeke 523, na  Kigamboni 155.

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, Mahakama ya Mkoa na Wilaya mashauri yaliyosikilizwa kwa teknolojia hiyo ni 367,  kanda  zingine ni Tanga 310, Musoma 158, Tabora 130, Dodoma 78, Mtwara 66, Moshi 46, Arusha 41, Kigoma, 37,  Sumbawanga 23,  Iringa 15, Songea 14, Shinyanga 12, Mwanza 28 na Bukoba 5.

Essaba  alifafanua kwamba Mahakama Kuu Divisheni za Biashara imesikiliza mashauri 55 na Kazi mashauri 90, ambazo zilitumia vifaa vilivyopo kwenye maeneo yao.

Aidha  aliongeza kwamba  zaidi mashauri 300 yamesikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza kwa kutumia simu ya mezani ‘Teleconference’ kwa sababu kuna tatizo la ukosefu wa huduma ya  mtandao ‘internet’ kwenye ofisi  za Mwanasheria  wa Serikali, hali inayosababisha kutumia njia hiyo.

Uongozi wa Mahakama katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na Virusi vya Corona ulikabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Maafisa TEHAMA wa kanda 16 za Mahakama Kuu yaTanzania Aprili 16 mwaka huu ili kuziwezesha Mahakama nyingine kusikiliza mashauri kwa  teknolojia hiyo,

Awali teknolijia hiyo  ilikuwa inatumika katika vituo sita, ambavyo ni mfumo huo, umefungwa ambavyo ni  Mahakama Kuu ya Tanzania katika Kanda za Dar es salaam, Mbeya, na Bukoba pamoja na Kituo cha Mafunzo cha Kisutu, Gereza la Keko na Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), Lushoto.


Share:

Serikali Yatahadharisha ‘Tegesha’ Nyamongo

Na Munir Shemweta, WANMM TARIME
Serikali imewatahadharisha wananchi wa kijiji cha Komarera kata ya Nayamongo Tarime Vijijini mkoani Mara kuacha tabia ya kufanya maendelezo maarufu kama Tegesha katika eneo linalotaka kuchukuliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara kwa shughuli za uchimbaji madini.

Tahadhari hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki Nyamongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara na Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha wakati wa kutangazwa notisi ya kusitisha kufanyika maendelezo kwenye vijiji vinavyozunguka Mgodi wa North Mara vya Kemorera na Kewanja vilivyopo wilayani Tarime na Mkuu wa wilaya Mtemi Msafiri.

Evelyne alisema, wakati mchakato wa kutwaa eneo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini ukifanyika tayari baadhi ya wananchi wasio waaminifu katika maeneo ya Nyamongo wameanza kufanya maendelezo kwa kasi (Tegesha) kwa kupanda migomba na Mialovela lengo likiwa kujipatia fedha wakati wa zoezi la uthamini.

‘’Wananchi mmekosa subira kabisa mmeanza kupanda mialovera, migomba, miembe  na katani ili mjipatie fedha huko ni kutegesha na serikali haiko tayari kuwalipa watu wa aina hiyo, mimi kama mshauri wa uthamini nasema ni kosa kufanya hivyo’’ alisema Evelyne

Amewataka wananchi wa wameneo hayo hasa wanawake kutodanganywa kwa kushiriki kupanda vitu kwa kutegesha kwa kuwa havitahesabiwa na badala yake wote waliofanya hivyo waondoe walivyoapanda ili kuepuka hasara ya kutolipwa.

Akitangaza uamuzi wa kusitisha maendeleo kwenye eneo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Injinia Mtemi Msafiri alisema kuanzia siku ya kutangazwa notisi ya usitishaji hairuhusiwi mtu yoyote kufanya maendelezo na wananchi ambao vijiji vyao vinapitiwa na zoezi hilo wanatakiwa kusubiri zoezi la uthamini na atakayeenda kinyume atahesabika kama ametegesha

Alisema, Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara sasa unamilikiwa kwa ubia wa Kampuni ya Barick na Serikali kupitia Twiga Corporation Ltd na kusisitiza udanganyifu utakaofanyika utasababisha wananchi kutolipwa kwa wakati kama ilivyotokea kwenye zoezi la awali lililolazimu kufanyika uhakiki katika maeneo yaliyothaminiwa.

Kwa mujibu wa Mrakibu wa Maendeleo ya Jamii wa Mgodi wa Barrick North Mara Sadala Hamis eneo linalotakiwa kuchukuliwa kwa shughuli za uchimbaji madini kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi huo lina ukubwa wa takriban hekta 404 na wakazi wasioopungua mia tatu.

Hivi karibuni wakati wa kutoa fidia ya shilingi bilioni 33 kwa wakazi 1,639 wa vijiji vya Matongo na Nyabichune katika eneo la Nyamongo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazo Dkt Angeline Mabula alieleza kuwa zoezi la utoaji fidia lilichukua muda mrefu kwa sababu wananchi hawakuwa wakitoa taarifa sahihi na baadhi kutegesha na kuwaasa kutoa ushirikiano na kuwa wakweli katika masuala yanahusu ulipaji fidia sambamba na  kuwataka kutowekeza maeneo ambayo mgodi unataka kuyachukua.


Share:

Serikali Yataka Mikopo Ya Tadb Kuwa Chachu Kwa Wavuvi Kuanzisha Viwanda Vidogo.

Na. Edward Kondela
Serikali imesema inataka kuona uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vya wafugaji na wavuvi kupitia mikopo inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuyaongezea thamani mazao yanayotokana na sekta za mifugo na uvuvi.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amezungumza hayo (30.05.2020) katika Kijiji cha Kanyala kilichopo Halmashauri ya Buchosa iliyopo Wilaya Sengerema Mkoani Mwanza, wakati wa kukabidhi mkopo wa Shilingi Milioni 100.7 uliotolewa na TADB kwa Chama cha Ushirika cha Zilagula ambacho pia kimepata mkopo wa Shilingi Milioni Tano kutoka katika mfuko wa mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.

Mhe. Ulega amesema licha ya vyama vingine vya Kasalazi na Soswa ambavyo kila kimoja kimepata pia mkopo wa halmashauri wa Shilingi Milioni Tano, ili wafugaji na wavuvi waweze kunufaika na mikopo kupitia ushirika wao, wizara itakuwa msimamizi kwa vyama vitakavyokidhi sifa za kupata mikopo kutoka TADB.

“Wizara ya Mifugo na Uvuvi itaenda kuwa msimamizi namba moja wa vyama vya ushirika tena kwa barua hivyo niwatakeni uongozi wa mkoa, halmashauri na ushirika wekeni taarifa zenu vizuri. Tunataka viwanda vidogo vidogo vya wafugaji na wavuvi vikiwemo vya kukausha dagaa, minofu ya samaki na kutengeneza kayabo nzuri ili mpeleke bidhaa hizo kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.”  Amesema Mhe. Ulega

Aidha Mhe. Ulega amevitaka vyama hivyo vitatu vilivyopata mikopo waitunze mikopo hiyo kwa kuifanyia kazi na hatimaye kuirejesha, kikiwemo Chama cha Zilagula kilichopata mkopo kutoka TADB, kwa kuwa fedha zilizotolewa na benki hiyo zinamilikiwa na watanzania kwa asilimia mia moja  ili watanzania wengine pia waweze kunuifaika na mikopo hiyo na kutoa rai kwa wavuvi kuendelea kujiunga katika vyama vya ushirika wakati akikabidhi hati ya kuandikishwa kwa vyama vya Sangara-Nyakaliro na Gembare vilivyopo Halmashauri ya Buchosa.

Amewataka pia watendaji wa serikali kutoa elimu kwa vyama vya ushirika namna ya kuitumia vyema mikopo wanayopata ili waweze kuirejesha kwa wakati pamoja na kuwaongoza ili waweze kupata mikopo mikubwa zaidi kwa kuwa utoaji mikopo kwa vyama vya ushirika vya wafugaji na wavuvi ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa kutaka kuona wananchi wananufaika na rasilimali zilizopo hapa nchini.

“Watendaji wakati mwingine vyama vya ushirika havikosei kufikia hatua mbaya ya kukosa mikopo ni muhimu elimu itolewe na watendaji kwa wafugaji na wavuvi msiwaache hawa watu wa ushirika waliopatiwa mikopo kwa kuwapatia elimu na kuwaongoza hatua kwa hatua ili waweze kulipa marejesho ya mikopo waliyopatiwa.” Amefafanua Mhe. Ulega

Vilevile, Naibu Waziri Ulega amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kujiepusha na ubadhilifu wa fedha za mikopo hiyo kutoka TADB, huku akitoa rai kwa wavuvi kuwa na uchumi endelevu na hatimaye kuwa walinzi wa rasilimali za uvuvi kupitia vyama vyao vya ushirika kwa kuwa azma ya serikali ni kuona Tanzania inaongoza kwa kusafirisha minofu ya samaki kwenda nje ya nchi na mchango wa samaki katika pato la taifa unaongezeka kutoka Asilimia 1.7 hadi Mbili ya sasa na kufikia Asilimia Tano na kuendelea.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Japhet Justine ameishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuweka mikakati mizuri na benki hiyo iliyowezesha kuweka mazingira mazuri ya kuhakikisha wafugaji na wavuvi wanakuwa na sifa za kupatiwa mikopo ili kujiendeleza katika sekta hizo.

“Tuliomba kwanza vyama hivi vikae katika ushirika kwa sababu tuliamini ule umoja wao utatupatia njia kuhakiksha mikopo inalipwa kwa kuwaweka katika mfumo ulio rahisi, wizara pia iliweka mazingira ya kubadilisha mitumbwi kuwa na namba na kufahamika ili benki iweze kuwa na taarifa sahihi ya mitumbwi ya wahusika wanaopatiwa mikopo pamoja na kuweka mazingira ya wavuvi kuwa na mifumo rasmi ya kuweka na kutoa pesa ili benki iweze kujua historia na kutoa mikopo kulingana na historia ya waombaji.” Amebainisha Bw. Justine

Bw. Justine ameongeza kuwa TADB inatoa mikopo hiyo na nia yao ni kuona wafugaji na wavuvi wengine wengi wananufaika na mikopo hiyo na kuwataka kufanya biashara zao kwa kuweka kumbukumbu zao vizuri ili wanufaika waweze kufikia hatua ya kuwa na viwanda vidogo vidogo.

Aidha, amesisitiza kwa vyama vya ushirika vilivyopata mkopo kutoka TADB kuhakikisha vinalipa mikopo hiyo kwa wakati ili watanzania wengine wenye uhitaji wa kupata mikopo hiyo waweze kupata na kukuza biashara zao.

Kuhusu Dawati La Sekta Binafsi lililo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambalo limekuwa likifanya kazi kubwa katika kuhakikisha wafugaji na wavuvi wanaunganishwa na taasisi mbalimbali za kifedha, Mratibu wa dawati hilo Bw. Steven Michael amesema kazi yao kubwa ni kuhakikisha matokeo chanya yanaonekana likiwemo tukio la Chama cha Ushirika cha Zilagula kupatiwa mkopo wa Shilingi Milioni 100.7 kutoka TADB.

Bw. Michael amesema wamefanya kazi kubwa kuhakikisha vyama vya ushirika wanaviunganisha na taasisi za kifedha pamoja na halmashauri mbalimbali nchini na kufuatilia mara kwa mara kwa kuwa wao wanafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha wadau wa mifugo na uvuvi na taasisi hizo kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Zilagula Bw. Joram Yuda amesema wanaishukuru serikali kwa kuwa wavuvi wameanza kuaminika na taasisi za kifedha kwa kuwapatiwa mikopo ili kujiendeleza katika sekta hiyo, huku Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Gembare Bw. Hassan Muhenga ameishukuru pia Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na TADB kwa kuhakikisha wanasimamia maono ya Rais Dkt. John Magufuli ya wavuvi kupatiwa mikopo.

Mwisho.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili May 31















Share:

Saturday 30 May 2020

Picha : RAIS MAGUFULI NA MARAIS WASTAAFU WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI ZA IKULU YA CHAMWINO DODOMA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika Chepe ili kuweka zege na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benja min Mkapa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika Chepe ili kuweka zege na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benja min Mkapa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere kuashiria uzinduzi wa Mitambo na magari yatakayotumika katika ujenzi wa Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na vijana wa JKT wanaojenga Ikulu ya Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere wakisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere wakielekea kwenye uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Ofisi za Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia bendi ya ya JKT mara baada ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020.
Waandishi mbalimbali wa Habari wakiwa wameshika chepe ili kuweka zege kama ishara ya kuweka kumbukumbu kwenye jiwe la msingi Ujenzi Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 30 Mei 2020.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo la Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino.PICHA NA IKULU



Share:

Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya Saba (07)

Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188


ILIPOISHIA   
“Yaani sijui kwa nini uliaolewa na yule mzee”
“Ahaa ni maisha tu. Tumefika baba yangu”
Mrs Sanga alizungumza huku akisimamisha gari lake nyuma ya gari la Tomas alilo liacha kwenye maegesho ya ofisi za rafiki yake.
“Haya shuka, acha mimi niwahi nyumbani”
“Sawa mke wangu”
Tomas taratibu akafungua mlango wa gari la mrs Sanga na kushuka huku akiwa na mfuko wenye pesa. Mpelelezi mmoja akaanza kazi ya kumpiga picha Tomas bila ya yeye kufahamu. Huku mpelelezi mwengine akitoa ripoti kwa mkuu wao kwamba wamempata jambazi aliye mteka nabii Sanga.


ENDELEA
“Hakikisheni kwamba hamumpotezi mtuhumiwa”
“Sawa mkuu”
“Pia kuweni makini kumfatilia na ikiwezekana muweze kumkamata hata kabla hajafanya jambo lolote”
“Sawa sasa mkuu”
Tomas pasipo kujua chochote akaingia kwenye gari lake aina ya Toyota Prado Tx. Tomas akaanza kuondoka eneo hilo huku akiwa na furaha ya kujivunia milioni ishirini za bure, kwani makubaliano yake na watekaji ni kuwalipa milioni arobaini.
                                ***
“Mage Mkinga una ndugu?”
Sheby aliuliza huku akipunguza mwendo, kwani mbele yao kuna tuta refu kidogo.
“Hapana”
“Au unakwenda kwa shemeji?”
“Hakuna kitu kama hicho Sheby”
“Ila nini tena jamani?”
“Kuna mambo yangu nakwenda kuyafanya”
“Mmmmm….ila unaweza kunipa nafasi ya kuzungumza”
“Kuzungumza nini?”
“Ahaa….katika siku zote za maisha yangu, nimetokea kukupenda Mage, ila nilikuwa nina tafuta muda muafaka wa kuweza kukueleza hilo”
“Ila Sheby wewe si unaishi na mwanamke?”
“Ndio nina ishi naye tu, ila ukweli ni kwamba sina mapenzi naye”
“Acha uongo Sheby na yule dada alivyo mzuri, inakuwaje huna mapenzi naye?”
“Unaweza kuishi na mtu ila usimpende. Hivyo ni sawa na mimi, nina ishi naye tu ila ukweli ni kwamba simpendi”
“Inakuwaje una ishi na mwamke usiye mpenda?”
“Ana mimba yangu na hicho ndio kinacho mfanya kuwepo kwangu. Ila ingekuwa sio mimba wala nisinge kuwa naye”
“Sheby muogope Mungu.  Mpende mtoto wa watu usije ukamuumiza kwa chochote”
“Ila simpendi?”
“Sawa humpendi na mbaya ana kwenda kuwa mama wa mwanao. Hivyo mpende na kumuheshimu bwana”
“Haya bwana. Ila hata siku moja sijawahi kumuona shemeji yetu. Vipi?”
“Usijali utamuona”
“Ni nani?”
“Ahhaa….wewe si unataka kumuona. Utamuona siku itakapo fika”
“Haya bwana”
Safari ikazidi kusonga huku wakizungumza mambo mengi sana kuhusiana na maisha. Majira ya saa moja kasoro wakafika Mkinga. Magreth akatoa simu  yake na kupiga namba ya watekaji.
“Nimefika Mkinga”
“Upo na nani?”
“Dereva taksi”
“Muache hapo stendi na panda pikipiki na umpatie simu dereva wa pikipiki nitampatia maelekezo ya wapi anapaswa kukuleta”
“Sawa”
Simu ikakatwa.
“Nani huyo”
“Ni jamaa yangu. Ameniambia nikuache hapa kwa maana huko ninapo kwenda gari haiwezi kuingia. Nitapanda pikipiki, kisha nitapelekewa huko ninapo pahitaji”
“Sawa, kwa hiyo nikusubirie hapa kwa muda gani?”
“Hadi nitakapo rudi. Nipatie namba yako ya simu”
Sheby akamtajia Magreth namba yake ya simu. Magreth akashuka kwenye taksi hiyo. Waendesha pikipiki kama kawaida yao ya kumkimbilia mteja, ndivyo jinsi walivyo fanya kwa Magreth. Magreth akamchagua dereva mmoja kati ya watano walio mfata. Akapiga simu kwa watekeji.
“Mpatie dereva pikipiki simu”
Magreth akampatia dereva pikipiki simu. Baada ya kuelekezwa wapi ampeleke Magreth simu hiyo ikakatwa.
“Una pafahamu?”
“Ndio”
“Itakuwa kiasi gani?”
“Elfu kumi”
“Ni mbali sana?”
“Sio sana”
“Haya”
Magreth akapanda pikipiki na kuondoka eneo hilo la stendi. Ndani ya dakika arobaini na tano, wakafanikiwa kufika karibu kabisa na msitu huo. Magreth akashuka na kumlipa na dereva pikipiki akaondoka. Simu ya Magreth ikaita na kuipokea. Tembea hatua kumi mbele kisha kunja kushoto utaona gari nyeusi”
Magreth akaanza kutembea huku simu yake ikiwa sikioni mwake. Baada ya hatua hizo kumi akakunja kushoto na kuona gari nyeusi ikiwa imefichwa vichakani. Japo kigiza kimeanza kuingia ila hakuweza kuogopo kwa lolote kwani tayari amesha dhamiria kumuokoa nabii Sanga. Wanaume wawili walio zifunika sura zao wakatoka ndani ya gari hilo huku wakiwa na bastola mikononi mwao.
“Vua begi”   
Magreth akavua beigi hilo mgongoni na kulishika mkono wa kulia. Watekeji hao wakaanza kumpapasa mwili wake wote. Walipo hakikisha hana silaha wala kinasa sauti wakaichukua simu yake kisha wakamfunga kitambaa cheusi usoni mwake. Wakamuingiza ndani ya gari, ili kumchanganya Magreth asitambue ni wapi anapo elekea, wakaanza safari ya kurudi mjini. Walipo karibia na mjini, wakageuza gari na kuianza safari ya kurudi msituni huku gari hilo likiendeshwa kwa kasi sana. Wakafika msituni, wakamshusha Magreth kwenye gari, wakaongozana naye hadi kwenye chumba walipo muweka nabii Sanga.
                                ***

Wapelelezi hawa wakazidi kulifaafilia gari la Tomas kwa umakini sana. Tomas akatoa simu yake mfukoni, akatafuta namba ya Rama D, ambaye ndio kiongozi mkuu wa kikosi cha watekaji hao.
“Mzee baba”
“Niambie mwana”
“Vipi huyo boya ana endeleaje?”
“Yupo fresh, ana mbwela mbewle tu hapa”
“Chok** huyo. Sasa ni hivi mzee baba. Ninawaletea mpunga wenu muda huu”
“Muda huu?”
“Ndio”
“Fresh mwana, ni wewe ila kuwa makini”
“Usijali mwana nipo makini sana. Ila hakikisheni kwamba hamumpigi kwa maana bibie ana mbwela kishenzi”
“Ahahaa”
“Yaa nyinyi hakikisheni kwamba ana kuwa salama huyo mzee”
“Poa poa mwana, hilo halina tabu, kikubwa mpunga uwe mezani”
”Fresh mida”
“Poa”
Kitendo cha Tomas kukata simu, akastukia gari ndogo ikimpita kwa kasi na kupunguza mwendo hadi ikamlazimu na yeye kupunguza mwendo.
“Huyu msen** nini, anapunguzaje mwendo?”
Tomas alizungumza kwa hasira huku akipiga honi. Dereva wa gari hilo akaligeuza gari lake na kulifanya liifunge barabara nzima. Tomas akasimamisha gari lake na kushuka kwa hasira sana huku akimfaata dereva wa gari hilo.
“Wewe msen** umelewa nini?”
Tomas aliporomosha matusi. Wapelelezi hao wakashuka kwenye gari lao huku wakichomoa bastola zao. Kitendo hicho kikaanza kumtetemesha Tomas.
“Ka…kaaakkk…..ma…..”
Mpelelezi mmoja hakumpa nafasi Tomas ya kumalizia sentensi yake. Akampiga mtama mmoja matata na kumfanya arushwe juu kimo cha mbuzi na kuanguka mzima zima. Mpelelezi huyo akamgeuza Tomas na kumlaza kifudifudi. Akamuwekea kigoti cha shingoni huku akiichomeka bastola yake kiunoni mwake na kutoa pingu mfukoni mwake. Akaifunga mikono yake hiyo na kumnyanyua. Kitendo hicho kikamfanya Tomas atambue kwamba watu hao ni polisi na si majambazi kama alivyo hisi kwa mara ya kwanza.
“Munanikamata nini? Kosa langu ni nini?”
“Ushibitisho wa pesa upo hapa”
Mpelelezi ambaye alikuwa akikagua gari la Tomas alizungumza huku akitoa mfuko huo wenye milioni arobaini.
“Poa piga picha ushahidi kisha endesha gari lake na mimi nina muingiza huku. Una haki ya kukaa kimya, kila kitu utakwenda kukijua kituoni”
Mpelelezi huyo alizungumza huku akimuingiza Tomas, ndani ya buti ya Alteza na kuifunga. Akaingia ndani ya gari hilo, kisha wakageuza na kuanza safari ya kuelekea central Polisi.
                                ***
    Magreth akafunguliwa kitambaa alicho fungwa usoni mwake. Macho yake yakakutana na nabii Sanga, aliye kaa kwenye kiti huku pembeni yake wakiwa wamesimama watu wa wiwili wenye mitutu ya bunduki aina ya AK47. Akataka kumkimbilia na kumkumbatia, ila mtekaji mmoja akamzuia.
“Tunahitaji kuziona pesa”
Magreth akaliweka chini begi hilo na kulifungua. Vitita vya dola za Kimarekani, vikawafanya watekaji hao wawili walio kuwa karibu na begi hilo kutazamana. Kwa isharaha mkuu wao akamuagiza mmoja wao kuzimwaga pesa hizo juu ya meza. Vibunda hivyo vikamwagwa juu ya meza  na kuifanya mioyo ya watekaji hao kujawa na furaha.
“Kalete mashine”
“Sawa”
Mtekaji mmoja akatoka, baada ya dakika mbili akarudi akiwa na mashine ya kuheshabia pesa. Wakaanza kazi ya kuhesabu vibunda hivyo vya pesa. Ilipo timia dola elfu sitini, mkuu wao akampa mkono wa kumshukuru nabii Sanga.
“Unaweza kuzungumza chochote mzee”
“Ni nani ambaye amewapa oda ya kuniteka?”
“Ni kutoka kwa kijana wako Tomas ambaye ni dalali wako”
“Tomas?”
“Ndio na hapa ninavyo zungumza yupo njiani ana ileta milioni ishirini kwa ajili ya kazi tuliyo mfanyia.”
Nabii Sanga akakaa kimya huku akiisikilizia hasira jinsi inavyo utafuna moyo wake. Akanyanyuka kwenye kiti hicho huku macho yakitawaliwa na uwekundu. Muda wote Magreth yupo kimya akishuhudia jinsi nabii Sanga alivyo kasirishwa kwa kitendo hicho kibaya alicho fanyiwa.
“Ana kuja hapa eheee?”
“Ndio mzee”
“Sasa hiyo ni milioni mia na ishirini. Hizi ishirini anazo zileta chukueni na hiyo ishirini ya ziada aliyo zidi, hakikisheni muna mchinja mume nielewa?”
Kauli ya nabii Sanga ika mstua sana Magreth, ila hakuweza kufungua kinywa chake kwa maana hajajua ni makubaliano gani nabii Sanga ameingia na watekaji hao.
“Sawa mkuu”
“Tena nina hitaji mumkate kate kiungo kimoja baada ya kingingine na mumuambie kwamba mimi ndio nimetoa kazi hiyo”
“Sawa mzee”
“Na kuanzia hivi sasa, nitakuwa nina wapa kazi zangu. Nahitaji muzifanye kwa uhakika na sitaki kabisa mulegelege, kama muna taka pesa zaidi ya hii basi mushikamane na mimi sawa”
“Sawa, ila tunahitaji kukudhibitisha kwamba huto tusaliti. Wote hapa tumeingia kiapo cha damu hivyo na wewe tuna hitaji uingie kiapo cha damu”
“Hilo halina shida. Niambieni nifanye nini?”
Mmoja wao akatoa kisu. Wakamtazama Magreth, wakampa ishara ya kutoka ndani humo na Magreth akatii. Wakaufunga mlango wa chumba hicho. Wakavua vinyago vilivyo ficha sura zao.
“Mimi ninaitwa Rama D. Sisi sote ni watoto wa familia moja na mimi ndio kaka yao. Huyu anaitwa Selemani D. Huyu anaitwa Rashid D na huyu ni mdogo wetu wa mwisho ana itwa Abdalah D. Baba yetu alikuwa ni komandoo wa jeshi la nchi hii. Alitupa mafunzo toka tukiwa wadogo na tumekuwa ni professional wa mbinu za kijeshi. Tuna uwezo wa kufanya kila aina ya tukio hivyo karibu katika familia”
Rama D, alizungumza huku akimtazama nabii Sanga. Nabii Sanga alipo hakikisha kwamba amewakremisha sura zao vijana hao. Akajikata sehemu ndogo ya kiganja chake na akapewa kikopo cha kuiweka damu hiyo inayo mchuruzika kiganjani. Rama D na wadogo zake wakajikata na wao na damu zao wakaziweka katika kikopo hicho, ikiwa ni ishara ya muungano wa damu.
“Nimekaribia. Nina juana na watu wengi sana duniani. Nitahakikisha nina wawezesha kisilaha, kifedha na kila aina ya mbinu mpya nitawapatia kwa maana, hadi leo hii nimekuwa tajiri si kwamba ni Mungu amenibariki, ila nilitumia kila aina ya njia kuwa tajiri. Hivyo natambua shida kama hizi”
“Karibu sana.”
Baada ya nabii Sanga kukaribishwa katika familia hiyo. Rama D na wadogo zake, wakavaa vinyango vyao. Wakafungua mlango na kumuita Magreth ndani.
“Simu yako”
Selemani D, alizungumza huku akimkabidhi Magreth simu yake.
“Huyu mwanamke nina imani wote mume muona”
“Ndio”
“Hakikisheni kwamba hakuna anaye msogelea na kila anaye jaribu kumsogelea basi mnajua nini mna paswa kufanya”
“Tumekuelewa.”
Kutokana na Magreth sio mwana familia wao. Wakamfunga kitambaa machoni mwake, kisha wakainza safari ya kuelekea Mkinga mjini huku wakiwa pamoja na nabii Sanga ndani ya gari lao.
                                ***
    Tomas akatolewa ndani ya buti ya gari hilo. Kwa mwendo wa haraka, akaingizwa kwenye kituo hicho kikubwa cha polisi. Umaarufu wake wa udalali katika jiji hilo la Dar es Saalam, likawafanya baadhi ya askari kushangaa juu ya uwepo wake hapo kituoni. Ila kutokana  ameletwa na pingu mikononi mwao hapakuwa na hata mmoja aliye wazuia wapelelezi hao kumpeleka katika chumba cha mateso. Thomas akavuliwa nguo zake zote, akafunguliwa pingu za mikononi mwake na kufungwa minyororo mizito. Akaning’inizwa hewani huku mikono yake ikiwa imechanuliwa mithili ya Yesu alivyo sulubiwa msalabani. Wapelelezi hao wakamwagia maji mwilini mwake, kisha mmoja wao ahachukua nyaya mbili za umeme, zenye hasi na chanya. Akazigusanisha na zikaanza kutoa cheche cheche, zilizo mfanya Thomas kujawa na mshangao hata kabla ya kupachikwa na nyaya hizo mwilini.
“Ukijibu kwa usahihi basi adhabu hii huto ipata. Ila ukijibu kwa jeuri basi adhabu hii utakumbana nayo.”
Kauli ya mpelelezi ikamfanya Tomas macho kumtoka huku akiwa haelewi ni kosa gani lililo mfanya kukumbana na shurba zote hizo.
“YUPO WAPI NABII SANGA”
Mapigo ya moyo ya Tomas yakaanza kumdunda kwa kasi sana kwani hakutarajia kwamba, mpango wa siri alio upanga yeye na mrs Sanga utajulikana kirahisi namna hiyo.


 ITAENDELEA
Haya sasa nabii SANGA yupo huru na ametambua kwamba Tomas ndio muhusika wa kutekwa kake. Tomas yupo mikononi mwa polisi. Je akibanwa atafichua siri nzito ambayo hata polisi wakielezwa hawato iamini?. Nini kitatokea? Endelea kufaatilia kisa hiki cha kusisimua, usikose sehemu ya 08

 


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger