Wednesday 27 May 2020

Vyuo Vikuu Zanzibar Kufunguliwa Juni Mosi, Michezo kuanzia tarehe 5 juni, 2020

...
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaungana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kuwa kuanzia tarehe 01 juni, 2020 vyuo vyote vya elimu ya juu vitafunguliwa na kuendelea na programau zao kama kawaida kwa upande wa Zanzibar.

Hayo yameelezwe na Makamo wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari amesema wanafunzi wa kidato cha sita nao wataanza masomo yao tarehe 01 juni, 2020 ili kuwawezesha kufanya mitihani yao ya taifa.

“Kufuatia maamuzi haya Serikali imeiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kushirikiana kikamilifu na wizara ya afya katika kuandaa miongozo ya kiafya itakayopaswa kuzingatiwa ili kuepuka maambukizo ya maradhi Corona”-Amesema

Aidha Balozi Seif amesema kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tano pamoja na wanafunzi wa skuli za msingi, maandalizi na madrasa, zitaendelea kufungwa hadi yatakapotolewa maelekezo mengine ya Serikali.

Kwa upande wa michezo, ligi kuu ya mpira wa miguu Zanzibar itaendelea kuanzia tarehe 5 juni, 2020 na kuiagiza Wizara ya Vijana, Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na ZFF pamoja na Wizara ya Afya kuandaa muongozo na namna bora ya kuendesha ligi hiyo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger