Saturday 30 May 2020

Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Kabudi Ataka Nchi Za Sadc Kuimarisha Ushirikiano

...
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof Palamagamba Kabudi amezitaka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuimarisha ushirikiano na umoja wakati huu wa kuenea kwa janga la  Virusi vya Corona huku bidhaa na huduma muhimu zinazovuka mipaka baina ya nchi na zikiendelea kutolewa.

Prof. Kabudi amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa njia ya Video katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Nawaomba Nchi zote Wanachama wa SADC tuimarishe umoja na mshikamano wetu wakati huu wa kuenea kwa janga la Virusi vya Corona, huku bidhaa na huduma muhimu zinazovuka mipaka baina ya nchi nan chi zikiendelea kutolewa, huu ni wakati wa kuepuka vitendo vya kujitenga na kuongeza mashauriano baina ya nchi,” amesema.

Aidh Mhe Waziri ameziomba Nchi za SADC kuwapa heshima na kuthamini utu wa madereva wanaosafirisha bidhaa na huduma muhimu kuvuka mipaka ya nchi kwa wakati huu ambao ugonjwa wa corona umeenea katika nchi wanachama.

Amesema Nchi wanachama zinapaswa kuchukua hatua za kukabiliana na ueneaji wa virusi vya Corona bila ya kuwanyanyapaa madereva na kuwachukulia kama watu wanaosambaza virusi hivyo na kuongeza kuwa madereva hao wanapaswa kupewa heshima stahiki kama binadamu wengine na kuwashukuru kutokana na hatari wanayochukua ya kusafirisha mizigo na huduma wakati huu wa kuenea kwa janga hilo.

“Madereva wetu wamevunjika moyo kwa sababu wanaonekana kama wao ndio wanaosambaza virusi vya Corona na sio askari wazuri ambao wanatoa huduma ya kusafirisha huduma na biidhaa muhimu wakati huu wa mlipuko, katika nchi za jumuiya,”

Ameziomba nchi za SADC kuwapa heshima na kuthamini utu wa madereva hao huku zikiendelea kuchukua tahadhari za kupambana na janga la virusi vya corona na kuongeza kuwa umoja wetu ni muhimu sana kwa wakati huu.

“Naziomba nchi zetu tuwape heshima na kuthamini utu wa madereva hao na kuwapa heshima wanayostahili huku tukiendelea kuchukua tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa afya katika kukabiliana na janga hilo,” alisema.

Prof. Kabudi amesema janga la COVID 19 linaonekana kama halitoisha ndani ya muda mfupi na nchi za ukanda wa SADC lazima ziishi  kwa kufuata mifumo salama katika biashara na usafirishaji wa huduma na bidhaa ili kupata ukuaji wa uchumi na kuondoa umasikini huku tukiwa bado tunakabiliana na janga hili la ueneaji wa virusi vya corona.

Amesema wakati hatua za kukabiliana na janga la Corona zikiendelea kuchukuliwa nchi za SADC lazima zikumbuke dhumuni la utangamano miongoni mwa nchi wanachama ambalo ni kuboresha ufanyaji biashara baina ya nchi na nchi na hivyo kutowaangusha waanzilishi wa Jumuiya ya SADC.

Amesema ufanyaji wa biashara baina ya nchi na nchi ndani ya SADC uko chini ya asilimia 20 hali ambayo inazuia nchi wanachama kuona ukuaji wa uchumi wake na kuongeza kuwa janga la corona lichukuliwe kama chachu ya kuongeza juhudi za kuinua kiwango cha ufanyaji biashara baina ya nchi na nchi kupitia utekelezajia wa Protokali ya SADC katika biashara ya 2005 na uanzishwaji wa eneo huru la biashara la SADC.

Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la SADC Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwele na Waziri wa Maliasilia na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger