Saturday 30 May 2020

UTAFITI MPYA CHANJO YA CORONA WAONESHA MATUMAINI

...

Utafiti wa jarida la kitabibu la The Lancet umeonesha chanjo ya COVID-19 ya China imeleta matumaini baada ya kujaribiwa kwa watu wazima 108 wenye umri wa miaka 18 hadi 60 katika jimbo la Wuhan. 

Matokeo ya awali kutokana na jaribio la watafiti wa nchini China yameonesha chanjo hiyo ni salama, himilivu na yenye uwezo wa kuzalisha kinga dhidi ya SARS-COV-2 ambavyo ni visababishi vya COVID-19 kwa binadamu.

Utafiti huo umeonesha matumaini katika siku 28 za kwanza ambapo matokeo ya mwisho yanatarajia kutolewa ndani ya miezi sita, huku Profesa wa kitengo cha magonjwa ya kuambukiza na afya ya jamii katika Chuo Kikuu cha California, Robert Schooley akisema chanjo hiyo ni himilivu.

"Chanjo imeonesha kuwa ni himilivu kutokana na dozi tatu zilizojaribiwa na watu waliojaribiwa wameonekana kutengeneza kinga dhidi ya virusi vya Corona", amesema Prof. Schooley.

Prof. Schooley amesema kuwa utafiti zaidi unatakiwa kufanyika ili kubaini endapo nguvu ya kinga ya mwili itakuwepo na kinga ya T-cells inayopatikana mwilini itaendelea kupungua baada ya siku 28 huku akitaja umuhimu wa dunia kuungana katika utafiti wa maendeleo ya chanjo ya COVID-19 kwa pamoja.

Chanzo- EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger