Imebainishwa kuwa shughuli za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika Machimbo mbalimbalI ya dhahabu Wilayani Mbogwe mkoani Geita unachangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa Misitu iliyohifadhiwa kutokana na ukatiji holela wa magogo yanayotumika katika ujenzi wa Maduara pindi yanapoibuka maeneo mapya ya Uchimbaji.
Kauli hiyo imetolewa Mei 30 Mwaka huu na Mhifadhi Misitu wa wilaya ya Mbogwe, Ezekiel Mbilinyi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na hatua zilizochukuliwa kuhusiana na watu wanaojihusisha na vitendo vya ukataji misitu bila ya kuzingatia sheria za nchi.
Alisema sheria kali zimeanza kuchukuliwa kwa baadhi ya wachimbaji wanaobainika kujihusisha na vitendo vya uvunaji holela wa miti iliyopo katika maeneo ya misitu inayosimamiwa na wakala huo ili kuhakikisha ukataji miti hauhusiwi katika maeneo yaliyohifadhiwa kisheria.
“Kuibuka kwa migodi mipya ya madini katika wilaya hiyo imekuwa ikisababisha uharibifu wa Mazingira kwani maeneo mengi yameanza kuwa wazi kutokana na uvunaji halolela wa Magogo (matimba) jambo ambalo lisipochukuliwa hatua za dharura linaweza kusababisha maeneo mengi kugeuka kuwa jangwa,”alisema Mbilinyi.
Alifafanua kuwa Wilaya hiyo bado inahazina kubwa ya Misitu ya asili ambayo imetunzwa kwa muda mrefu hivyo ni budi wananchi wakaitunza kwa manufaa yao na kuacha na ukataji miti usiokuwa na tija kwaajili ya mkaa na shughuli za madini na badala yake wajikite katika matumizi ya Mkaa mbadala na uchimbaji wa kisasa usiotumia magogo ya miti.
Sambamba na hilo Mbilinyi aliwaomba wakazi wa vijiji ambavyo vinazungukwa na mapori hayo kuhakikisha wanafanya shughuli mbadala ikiwemo ufugaji wa nyuki ili kujiongezea kipato kwa kutengeneza mizinga ya kisasa kutokana na maeneo wanayoishi kuwa rafiki na ni salamaa kwao kwa ufagaji huo.
“Asali iuzwa kwa bei nzuri fugeni nyuki ili muweze kupata fedha kwaajili kununulia gesi ambayo itakuwa ni mbadala wa mkaa na kuni ambayo ni rafiki wa mazingira,eneo lenu linamisitu na nyuki wapo mnachotakiwa ni kutengeneza mizinga ya kisasa ili muweze kunufaika na biasahara hii ambayo inasoko kubwa,”alisema Mbilinyi.
Mateo Shija ni mchimbaji katika machimbo ya Nyakafulu wilayani humo ameiomba serikali kupitia wizara ya Madini kuwapatia elimu na vifaa vya kisasa ambavyo vitawasaidia kufanyashughuli za uchimbaji kwa teknolojia ya kisasa ambayo itaweza kunusuru ukataji wa miti kwaajili ya shughuli za uchimbaji kutokana na wengi wao kutumia mfumo wa kizamani wa magogo.
Guchonza Makoye mfanyabiashara wa Madini wilayani humo ameiomba serikali kuwapatia vifaa vya kisasa vya uchimbaji kama vile Mitambo ,matrekta,magari na mashine za Gesi ilikuachana uchimbaji wa kizamani ambao unasababisha wachimabaji wengi kupoteza Maisha kutonana na kufukiwa na vifusi vya udongo pindi mvua zinapoanza kunyesha.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment