Sunday 28 February 2021

Market Sales Manager at TalentintheCloud International

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Market Sales Manager   TalentintheCloud International Zanzibar West, Tanzania The continent’s most successful and fastest growing payments company is looking to add a talented and experienced Market Sales Manager to their team. Since identifying a gap in the African online payments landscape, they have rapidly led the online payments industry into centre stage – turning […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Medical Specialist II (Dermatologist) at Muhimbili National Hospital

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

  POST: MEDICAL SPECIALIST II (DERMATOLOGIST) – 1 POST POST CATEGORY(S) HEALTHCARE AND PHARMACEUTICAL EMPLOYER Muhimbili National Hospital APPLICATION TIMELINE: 2021-02-26 2021-03-11  DUTIES AND RESPONSIBILITIES   To provide routine specialized medical services for in-patients and out patients; To supervise ward rounds and advice on appropriate medication; To participate in the training of student doctors in their areas […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Tanzia : MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AFARIKI DUNIA


Andrew Mollel enzi za uhai wake

Na Mussa Juma - Arusha
 Mfanyabiashara maarufu mkoani Arusha, Andrew Mollel ambaye alikuwa mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampuni mbalimbali mkoani Arusha amefariki dunia na kuibua simanzi kwa wakazi wengi wa jiji hilo.

Akizungumza na Mwananchi leo, Februari 28, Mbunge wa jimbo la Monduli , Fredrick Lowassa amesema kifo cha Mollel ni pigo kubwa katika jiji la Arusha kutokana na mchango wake.

Lowassa amesema taratibu za mazishi wa Mollel zinaendelea kufanywa na wanafamilia lakini, kubwa ambalo Arusha watamkumbuka ni kuandaa michoro ya mradi mkubwa wa nyumba za PPF zilizopo eneo la Kijenge jijini hapa ambalo lilikuwa ni eneo lake.

Mollel alikuwa pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Happy Sausages ,Kijenge Animal Products Limited, Georges Center Ltd na AGM Holding na pia mjumbe wa bodi mbalimbali hapa nchini.

Via Mwananchi
Share:

JOGOO ASHIKILIWA POLISI KWA KUUA MMILIKI WAKE


Mtu mmoja ameuawa na Jogoo wake aliyekuwa amefungwa kisu mguuni kwa ajili ya mchezo uliopigwa marufuku wa kupambanisha jogoo Kusini mwa India.

Mmiliki wa jogoo alichomwa kisu usawa wa kati ya tumbo na nyonga wakati kuku huyo akijaribu kutoroka. Mwanaume huyo alipoteza maisha akiwa njiani kuelekea hospitali kwasababu ya kupoteza damu nyingi.

Polisi hivi sasa wanawatafuta watu wengine 15 waliohusika kwenye tukio hilo, ambalo lilifanyika kwenye kijiji cha Lothunur jimbo la Telangana wiki hii.

Kuku huyo alishikiliwa katika kituo cha polisi kabla ya kupelekwa shambani.

Polisi wamesema mnyama huyo alikuwa akitayarishwa kwa ajili ya kushiriki mpambano alipojaribu kutoroka.

 Mmiliki alijaribu kumkamata lakini alichomwa na kisu hicho chenye urefu wa sentimita 7 kilichokuwa kimefungwa kwenye mguu wa kuku huyo wakati wa purukushani hizo.

Wale waliohusika katika tukio hilo wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kutokusudia, kujihusisha na mchezo haramu wa kamari na kuhodhi mchezo wa kupiganisha kuku, shirika la habari la Ufaransa limeripoti.

Afisa polisi katika eneo hilo B Jeevan amesema kuku huyo atapelekwa mahakamani kwa ajili ya ushahidi, kwa mujibu wa gazeti la The New Indian Express.

Mchezo wa kuwapambanisha jogoo ulipigwa marufuku India mwaka 1960, lakini mchezo huo bado ni maarufu vijijini kama Telangana wengi hasa katika matamasha ya jamii ya Hindu wa Sankranti.

Si mara ya kwanza kwa mmiliki wa kuku kuuawa na jogoo wake.

Mwaka jana mwanaume mmoja huko Andhra Pradesh aliaga dunia baada ya kukatwa shingoni na kiwembe kilichokuwa kimefungwa kwenye mguu wa jogoo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la CNN, mmiliki alikuwa akimchukua jogoo wake tayari kwa mpambano wa jogoo wakati tukio hilo lilipotokea.

CHANZO- BBC SWAHILI

Share:

AWESO ATOA SIKU SABA MKANDARASI KULIPWA DENI LAKE


Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akipanda kwenye tanki la Mradi wa maji Lusilile, Manyoni kujiridhisha na viwango vya ujenzi wake.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikabidhi Mkataba kwa Jumuiya ya Watumiaji maji kwa mmoja wa wakazi wa kijiji cha Kashangu Itigi wilayani Manyoni. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Mbunge wa Manyoni Magharibi, Yahya Massare ( mwenye miwani) na Mkuu wa wilaya hiyo, Rahabu Mwagisa( kulia).


Na Abby Nkungu,  Manyoni

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amemwagiza Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Singida kumlipa ndani ya siku saba Mkandarasi wa Kampuni ya CMG Construction takriban Sh milioni 700 anazodai kutokana na kujenga tanki la kuhifadhia na kusambaza maji Lusilile wilayani Manyoni lenye ujazo wa lita milioni mbili.

Waziri Aweso alilazimika kutoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Manyoni Mashariki, Dk Pius Chaya kudai kuwa wananchi wake zaidi ya 50,000 katika vijiji 11 vilivyopo eneo hilo hawajaanza kunufaika na huduma ya maji ya mradi huo kutokana na Mkandarasi huyo kutolipwa deni lake.

"Lengo la mradi huu lilikuwa kupeleka maji kwenye Kituo cha Afya Kintinku na vijiji vilivyopo eneo hili lakini usambazaji wa maji unasuasua sana japo tanki lipo tayari." alisema Mbunge huyo na kuongeza;

Kituo hiki cha afya kinahudumia wananchi wa tarafa mbili; hivyo ni matamanio yangu huduma hii ya maji ifikishwe hapo mapema ili huduma nyingine za kiafya pia ziweze kufanyika ipasavyo".

Kutokana na hoja hiyo, Waziri Aweso alimuuliza Meneja RUWASA mkoa, Mhandisi Lucas Saidi iwapo ni kweli Mkandarasi huyo anaidai Serikali naye akathibitisha kuwa anadai takriban Sh milioni 700.

"Ndio maana mradi huu unasuasua. Hakikisha ndani ya siku saba Mkandarasi huyu awe amelipwa. Katoe Sh milioni 700 kwenye akaunti yenu umpe ili amalizie kazi wananchi waanze kupata huduma ya maji" aliagiza Waziri Aweso.

Akiwa kijiji cha Kashangu, Itigi Jimbo la Manyoni Magharibi, kwenye ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani Singida kukagua miradi mbalimbali ya maji, Waziri Aweso alielezwa kuwa jumla ya Sh milioni 150 ziliweza kuokolewa katika ujenzi wa mradi huo wa maji.

Meneja wa RUWASA wilaya ya Manyoni, Gabriel Ngongi alimweleza Waziri kuwa mradi huo ingawa ulitengewa jumla ya Sh milioni 350, lakini kwa kutumia wataalam wa ndani na mbinu nyingine mbadala, wameweza kutumia Sh milioni 200 tu; hivyo kuokoa Sh milioni 150.

Waziri Aweso aliipongeza hatua hiyo huku akiahidi kuwa Serikali haitakuwa kikwazo bali itatoa ushirikiano  wake wote kwa watumishi wanaojituma kama RUWASA Manyoni.

Aidha, alitoa mwito kwa wananchi wa eneo hilo na popote ilipo miradi ya aina hiyo Nchini kuitunza na kuilinda kwa nguvu zao zote kwa kuwa Serikali inatumia gharama kubwa katika kutekeleza miradi hiyo.  


Share:

Picha : ASKOFU MACHIMU AZINDUA WIMBO MAALUMU WA TANZANIA YA AMANI WA KWAYA YA DYNAMIC EAGT...AONGOZA MAOMBI DHIDI YA CORONA

Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akionesha DVD ya Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani kutoka Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Tazama Video : Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga - Tanzania ya Amani

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu amezindua Wimbo Maalumu wa Tanzania ya Amani kutoka Kwaya ya Dynamic ya kanisa la EAGT Ushirika Shinyanga.

Uzinduzi wa wimbo wa Tanzania ya Amani umefanyika leo Jumapili Februari 28,2021 katika kanisa hilo lililopo Ushirika Mjini Shinyanga ambapo pia Askofu Raphael Machimu ameongoza Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona.

Akizindua na kuweka Wakfu CD/DVD ya Wimbo huo, Askofu Machimu amesema wimbo wa Tanzania ya Amani kutoka Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga umegusa viongozi wan chi kwa kazi wanayofanya katika kulinda amani ya nchi hivyo kuwaomba Wakisto na watu mbalimbali kununua CD ya wimbo huo ambao pia umewekwa katika Mtandao wa Youtube katika Chaneli ya Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga.

“Tunazindua CD hivyo tunapozindua CD hii ni muhimu tuombe kwa ajili ya Rais wetu Mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa sababu amekuwa kiongozi wa mfano katika kuimarisha amani ya nchi yetu”,amesema Askofu Machimu.

Askofu Machimu ameeleza kuwa Rais Magufuli ameonesha mfano mkubwa katika kusimamia imani na hasa katika kukabiliana na Ugonjwa hatari wa Corona na amekuwa mhamasishaji mkubwa kwa Watanzania kumtegemea Mungu ili aondoe na kutokomeza ugonjwa wa Corona.

Katika kumuombea Rais Magufuli na viongozi wengine wa kitaifa, Askofu Machimu pia amemuombea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack, Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwa jinsi ambavyo amesimamia vyema mkoa wa Shinyanga ambao hapo awali ulikuwa unasifika kwa matukio mabaya ikiwemo mauaji ya vikongwe, watu wenye ualbino n.k

Aidha amesema wimbo wa Tanzania ya Amani ni wimbo mzuri akisema "Hii CD ya wimbo huu ukiwa nayo nyumbani utafurahi,waimbaji wamefanya kazi nzuri. Hii ni kazi takatifu kwa ajili ya kumpa heshima Mungu".

Mwenyekiti wa Kwaya ya Dynamic Daniel Chunga amesema lengo la wimbo huo maalumu wa picha walioupa jina la Tanzania ya Amani ni Kumshukuru Mungu kwa ajili ya kuilinda nchi ya Tanzania na kuliepusha taifa na majanga mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Corona.

“Kupitia wimbo huu tumezalisha nakala 150 zitakazouzwa leo na tutaweka wimbo huu katika Chaneli ya kwaya yetu Youtube”,amesema.

Kwa upande wake, Mgeni wakati wa uzinduzi huo, Mhandisi Edward Mollel amewapongeza wanakwaya kwa kutunga na kuimba wimbo wenye ujumbe mzuri huku akiwasisitiza waimbaji kuendelea kuwa wamoja, kushikamana na kushirikiana.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waimbaji wa Kwaya ya Dynamic ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga wakiimba wakati wa uzinduzi wa Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo leo Jumapili Februari 28,2021 . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Waimbaji wa Kwaya ya Dynamic ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga wakiimba wakati wa uzinduzi wa Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo.
Waimbaji wa Kwaya ya Dynamic ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga wakiimba wakati wa uzinduzi wa Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo.
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akiweka Wakfu CD ya  Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo leo Jumapili Februari 28,2021 
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akikata utepe kuzindua rasmi wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo leo Jumapili Februari 28,2021. Wa kwanza kushoto ni Mweka Hazina wa Kwaya ya Dynamic Veronica Shinyanga akifuatiwa na Mgeni rasmi Mhandisi Edward Mollel. Kulia ni Mwenyekiti wa kwaya ya Dynamic, Daniel Chunga.
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akifurahia baada kuzindua Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo leo Jumapili Februari 28,2021 
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akizungumza baada kuzindua Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo leo Jumapili Februari 28,2021 
Mweka hazina akifungua boksi maalumu lililobeba CD/DVD za wimbo wa Tanzania ya Amani baada ya Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu kuzindua Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo leo Jumapili Februari 28,2021 
Mweka Hazina wa Kwaya ya Dynamic Veronica na Mwenyekiti wa kwaya ya Dynamic, Daniel Chunga wakitoa CD/DVD kwenye boksi.
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akiangalia CD/DVD ya Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani kutoka Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga.
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akiangalia CD/DVD ya Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani kutoka Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga.
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akionesha CD/DVD ya Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani kutoka Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga.
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akionesha CD/DVD ya Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani kutoka Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga.


Muonekano wa DVD ya wimbo wa Tanzania ya Amani
Mgeni rasmi Mhandisi Edward Mollel akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani  
Mgeni rasmi Mhandisi Edward Mollel akionesha CD ya wimbo wa Tanzania ya Amani.
Waimbaji wa Kwaya ya Dynamic ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga wakiimba wakati wa uzinduzi wa Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo.
Awali MC Johnson Daniel akizungumza wakati Waimbaji wa Kwaya ya Dynamic ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga wakiimba kwenye uzinduzi wa Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo.
MC Johnson Daniel akizungumza wakati Waimbaji wa Kwaya ya Dynamic ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga wakiimba kwenye uzinduzi wa Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo.
Mwenyekiti wa Kwaya ya Dynamic Daniel Chunga akisoma risala kuhus Wimbo wa Tanzania ya Amani ambapo alisema lengo la wimbo huo maalumu wa picha ni Kumshukuru Mungu kwa ajili ya kuilinda nchi ya Tanzania na kuliepusha taifa na majanga mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Corona.
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akiongoza Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona.
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akiongoza Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona.
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akiongoza Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona.
Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona yakiendelea.
 Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona yakiendelea.
Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona yakiendelea.
Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona yakiendelea.

Waumini wakiwa ndani ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga
Waumini wakiwa ndani ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga
Wageni waalikwa wakiwa ndani ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga
Wanakwaya wa Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga wakiwa ndani ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga
Waumini wakiwa ndani ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

MKURUGENZI WA SHIRIKA LA AGRI THAMANI FOUNDATION MH NEEMA LUGANGIRA AONGOZA ZOEZI LA KUGAWA TAULO ZA KIKE WANAFUNZI 1,800 MANISPAA YA BUKOBA

 

MKURUGENZI wa Agri Thamani ambaye Pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia NGOs Mh Neema Lugangira akigawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za Sekondari
WANAFUNZI wa kike wa shule za Sekondari wakifurahia kupokea mfuko wao uliojaa taulo za kike za kutosha mwaka mzima kwa kila mmoja
FUSO lililokuwa limejaa Taulo za kike za wanafunzi wa kike 1800 wa Bukoba Manispaa likiingia kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba mjini likitokea Dar es Salaam
Mabox ya Taulo za kike ambazo zote zilikuwa zimeandikwa Jina la Shule ya Sekondari kwa Idadi Kamili ya Wanafunzi wa Kike
Hivi ndivyo kila mwanafunzi wa kike alivyoondoka uwanja wa Kaitaba na Furaha



Mkurugenzi wa Agri Thamani; Mhe Neema Lugangiea (Mb.) ambae pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh.Neema Lugangira ametoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi 1800 kutoka kwenye shule 16 za Manispaa ya Bukoba .

 

Ambapo kila mwanafunzi mmoja ataweza kutumia taulo alizopewa kwa kipindi cha mwaka mmoja katika zoezi ambalo iliyofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kwa Manispaa ya Bukoba jumla ya packet 25,200 za Taulo za Kike ziligawiwa kwa Wanafunzi wa Kike 1,800 kutoka Sekondari 16 za Kata zote 14 za Manispaa ya Bukoba.


Akizungumza wakati wa ugawaji wa taulo hizo katika zoezi ambalo liliratibiwa na Idara ya Elimu Sekondari Bukoba Manispaa na Afisa Elimu Taaluma Sekondari alishiriki zoezi zima.

 

Mhe Neema Lugangira amesema ameamua kufanya hivyo ili kuwasaidia wanafunzi hao kuweza kujihifadhi na kuweza kuendelea na masomo yao wakati wa  kipindi cha hedhi.

 

Alisema wanafunzi ambao watanufaika na msaada huo ni kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne ambao kwa sasa wataondoka na adha ambayo walikuwa wakikumbana nao wakati wakiwe kwenye kipundi cha hedhi.

 

“Naamini msaada huo utakuwa na manufaa makubwa kwao kutokana na kwamba watatumia muda mwingi kusoma hata wakiwa kwenye kipindi chao cha hedhi kutokana na kuwa na taulo ambazo zitawasaidia” Alisema Mbunge huyo.

 

Akizungumzia kuhusu msaada huo wa Taulo za Kike, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Bukoba Mjini Emanuele Ebeneza alimshukuru Mbunge Neema kwa msaada wake wa taulo za wasichana ambao utakuwa chachu ya kupunguza utoro shuleni.

 

Alisema kupitia msaada huo wanafunzi wengi watajua namna ya kujihifadhi na kupunguza utoro shuleni kwa sababu ya kutokujisikia vizuri kwenye kipindi cha hedhi.

 

“Niseme tu kwamba licha ya kutoa msaada huo lakini pia Mbunge Neema anafundisha wanafunzi juu ya hedhi salama,  anawaandaa kisaikolojia kupita kwenye kipindi cha hedhi na hivyo kuwaondolea hofu na anawapa elimu ya lishe bora inayowasaidia waepukane na changamoto ya upungufu wa damu (anemia) ”Alisema Afisa Elimu Sekondari Bukoba Manispaa. 

 

Afisa Elimu Sekondari huyo alisema kwamba pia Mbunge Neema Lugangira anawafundisha usafi hatua ambayo inasaidia kupunguza utoro ambao ungetokana na wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo wakati wa mzunguko wa hedhi.

 

“Kama unavyojua mzunguko wa wasichana unatokea kila mwezi mara moja na wakati mwengine wakishindwa kuhudhuria masomo hivyo alilolifanya ni kitu cha muhimu sana sana kwa maana ya wanasichana “Alisema Ndg Ebeneza

 

Mmoja wa wanafunzi hao Alisema kwamba changamoto kubwa ni kubwa pale pedi zinapokuwa zimekwisha wanashindwa kuishi kwa amani kabisa wakati wakiwa wanaendelea na masomo

 

Naye mwanafunzi mwengine amesema wanashukuru kwa msaada huo kutokana na kwamba wakati mwengine wamekuwa wakikosa shule kutokana na kutokuwa na taulo za kujihifadhi wakati wakiwa kwenye kipindi cha hedhi.

 

Hata hivyo Avitha Faustini ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari  Hamugumbe alimshukuru Mbunge Neema kwa msaada huo ambao amewapatia ambao umekuwa ni faraja kubwa kwao na kuwaondolea changamoto walizokuwa wakikumbana nazo.

 

Alisema wamepata ujasiri wa kuendele na masomo kwani kabla ya kupata Taulo  hizo walikuwa wakitokewa na hali hiyo wanakuwa wanyonge na wakati mwengine hulazimika kurudi nyumbani na  kukosa masomo. Aliongezea kwamba sasa hivi hawana haja ya kuwaomba wazazi pesa ya kununua pedi.

Mwanafunzi mwingine alikiri kwamba wengi hawajawahi kuziona taulo za kike na alielezea njia ambazo wengi wao wanatumia ambazo kwakweli hata sisi tunashindwa kuziandika maana sio salama kabisa. Mwanafunzi huyu alionyesha furaha ya aina yake kuona kwamba wamekumbukwa na kuthaminiwa hata kama wao ni watoto wa kimaskini.

Mradi huo wa Taulo za Kike umeshawanufaisha  Watoto wa Kike katika mikoa ya Dodoma, Tabora, Pwani, Tanga, Kigoma, Mtwara na Kagera na mikoa inayofuata kwa awamu hii ya kwanza ni Ruvuma na Lindi

Mbunge Neema Lugangira alimalizia kwa kusema kwamba Jumla ya Wanafunzi wa Kike 5,500 nchini watakuwa wamenufika ifikapo mwezi Mei 2021 ambapo Taulo za Kike zote zimetengenezwa na Kiwanda cha Tanzania ambacho kinauzoefu wa zaidi ya miaka 40 kwenye eneo hili. 

 


Share:

NAIBU WAZIRI WA MAJI AAHIDI NEEMA YA MAJI KIJIJI CHA KAZENGA

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi. Maryprisca Mahundi (Mb) amewataka wananchi wa kijiji cha Kazenga wilaya ya Chato mkoani Geita kutunza miundombinu ya maji ili iwe endelevu kwa vizazi vijavyo. 

Ameongea hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kazenga  waliosimamisha msafara wake ili waweze kuishukuru serikali kwa kuwajali kwa kuwakarabatia miundombinu ya mradi wao wa maji ambao uliacha kutoa maji tangu mwaka 1988.

“Tunafahamu mlikuwa na mradi wa siku nyingi ambao muda mrefu ulikuwa hautoi maji lakini sasa mradi umefufuliwa na umeanza kutoa maji, tunafahamu vituo vitatu vimeanza kutoa maji na baadhi ya maeneo bado hawajaanza kupata huduma hiyo, Nataka kuwahakikishia hivi vituo ambavyo havijapatiwa huduma ya maji baada ya mwezi mmoja vitapata maji”, amesema Mhandisi Mahundi.
Share:

MBUNGE KEMBAKI :HATA TUKIVAA BARAKOA KAMA MUNGU HAYUPO PAMOJA NA SISI NI BURE


Aliyenyoosha mkono ni Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato mtaa wa Majengo wilayani Tarime akifanya maombi maalumu kumwombea Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki (aliyevaa tai nyekundu). Picha na Dinna Maningo
Aliyenyoosha mkono ni Mchungaji wa kanisa la Waadventista Wasabato mtaa wa Majengo wilayani Tarime akifanya maombi maalumu kumwombea Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki (aliyevaa tai nyekundu).
Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Michael Kembakiakizungumza na waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato mtaa wa Majengo wilayani Tarime 
Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki akizungumza na waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato mtaa wa Majengo wilayani Tarime 
Walioketi mbele katikati ni Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki, wa kwanza kulia ni katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tarime Marema Sollo na wa kwanza kushoto ni Diwani wa Kata ya Kenyamanyori Farida Joel wakiwa kwenye ibada katika kanisa la Waadventista Wasabato Nkende ambapo walishiriki pia katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa
Wa Kwanza kulia ni Mbunge wa jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki,anayemfuatia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Tarime Thobias Ghati na wa tatu kulia ni Diwani wa Kata ya Turwa Chacha Marwa wakiwa kwenye ibada Kanisa la Waadventista Wasabato Majengo.

***
Na Dinna Maningo, Tarime
Mbunge wa Jimbo la Tarime mjini Michael kembaki amesema kuwa Mungu ndiye tumaini la Watanzania hata watu wakivaa barakoa kama Mungu hayupo pamoja nao ni kazi bure na kwamba ni vyema kuzidi kuombeana na kuliombea Taifa ili mwenyezi Mungu aepushe janga la Corona.

Kembaki aliyasema hayo wakati akichangia sh. milioni mbili ya ujenzi wa nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato mtaa wa Majengo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake huku akiwa ameambatana na Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Marema Sollo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyamisangura Thobias Ghati na Diwani wa kata ya Turwa Chacha Marwa.

Mbunge huyo aliwaomba waumini hao kuzidi kuliombea taifa dhidi ya janga la Corona ambalo limesababisha hofu kwa wananchi huku akiwapongeza waumini hao kwa kutovaa barakoa na kuweka tumaini lao kwa Mungu.

"Nawashukuru sana kwa jinsi mnavyoliombea taifa Mungu ndiye tumaini letu bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure, hata tukivaa barakoa kama Mungu hayupo pamoja na sisi ni bure, nimefurahi sijaona muumini hata mmoja aliyevaa barakoa.

"Kuna kanisa nilienda nikakuta asilimia 80 wamevaa barakoa na mimi nilikuwa sina barakoa ilinipa hofu sana, Mungu ndiye tumaini letu tuzidi kuliombea taifa letu ili lipite kwa ushindi katika janga hili ,mungu aliyetuepusha na janga hili wakati ule ndiye huyo huyo atatuokoa na janga hili",alisema Kembaki.

Mzee wa Kanisa la Majengo Simon Andrea alimshukuru mbunge kwa kutekeleza ahadi na kusema kuwa mtaa wa Majengo hauna nyumba ya mchungaji hivyo fedha hizo zitasaidia kuanza kujenga msingi kwa kuwa tayari wameshanunua uwanja.

"Mbunge katimiza ahadi yake mungu ambariki kuna watu wanatoa ahadi lakini hawatimizi, Mchungaji wetu anaishi nyumba ya kupanga kwa fedha hizi zitatusaidia kwenye hatua ya ujenzi nikuombe tutakapokuomba tena msaada tusikie na tusaidie", alisema Andrea.

Baada ya Mbunge huyo kuzungumza na waumini mchungaji wa mtaa wa Majengo Kumba Kihiri alifanya maombi maalumu kwa mbunge huyo ili mwenyezi mungu amuongoze katika kazi zake za kuwatumikia wananchi na familia yake pamoja na kumpatia afya njema.

Wakati huo huo, Mbunge Kembaki amechangia milioni 2.5 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Nkende ambapo mgeni rasmi katika harambee hiyo alikuwa mbunge wa viti maalumu Ghati Chomete aliyechangia sh.milioni mbili na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Samwel Keboye (Namba tatu) akichangia mifuko 50 ya saruji.

Baadhi ya viongozi wengine waliochangia fedha na saruji ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Tarime ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nkende Daniel Komote alichangia sh.500.000,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Thobias Ghati alichangia 100,000 na Marema Sollo akichangia mifuko mitano ya Saruji.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Samwel Keboye aliwapongeza wabunge hao Madiwani na wana CCM kwa kujitolea kusaidia shughuli za kanisa, aliwaomba kuendelea kusaidia makanisa na misikiti mbalimbali pale kunapohitajika msaada Kwani kwakufanya hivyo Mungu atabariki na akawakumbusha waumini kuliombea Taifa lililokumbwa na Janga la Corona.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger