Wednesday 24 February 2021

RAIS MAGUFULI : NINATEGEMEA KUVUNJA JIJI LA DAR ES SALAAM

...

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kuvunja Jiji la Dar es Salaam na kuchagua manispaa moja katika jiji hilo itakayopandishwa hadi na kuwa Jiji lengo likiwa kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatano Februari 24, 2021 wakati akizindua Daraja la Juu katika Makutano ya Barabara za Ubungo (Kijazi Interchange) Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Ninategemea kuvunja Jiji la Dar es Salaam ili tutengeneze jiji la eneo fulani tunaweza kuifanya Ilala ndio iwe jiji itategemea na namna mambo yatakavyokwenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu wanachangiwa fedha na hawana miradi ya maendeleo hili nitalikataa”,amesema.

"Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa. Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani na ninafikiri Ilala inafaa kuwa jiji maana ndio ipo katikati, Ubungo itasubiri maana barabara bado hazijatengenezwa,” amesema Rais Magufuli.

Amewataka viongozi ambao walijiandaa kuwa mameya wa jiji wajue hilo limekwisha.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger