Saturday 30 September 2023

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA GGML MAONESHO YA MADINI GEITA




Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia akimpatia zawadi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Sita ya Tekonolojia ya Madini Geita. Suleima alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho hayo.
Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman kuhusu shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo katika sekta ya madini. Makamu huyo alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga maonesho hayo
Mkurugenzi mtendaji wa GGML, Terry Strong akimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Sita ya Tekonolojia ya Madini Geita. Suleima alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho hayo.


NA MWANDISHI WETU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman leo Jumamosi ametembelea banda la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita na kupata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mgodi huo.



Pia amepata maelezo kuhusu huduma za uchunguzi na elimu ya saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume zinazotolewa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita kwa ushirikiano wa GGML ambapo hadi jana zaidi watu 1000 wamefanyiwa vipimo.

Akitoa maelezo kwa Makamu Rais huyo wa Zanzibar ambaye ndiye mgeni rasmi anayefunga maonesho hayo yaliyofanyika kwa siku 10, Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia alisema kampuni hiyo ndio inayoongoza kwa kuwa muajiri bora nchini.


Pia inaongoza kuwa kuzingatia sheria ya local content Pamoja na kuzingatia masuala ya usalama kazini.


Pamoja na mambo mengine amesema GGML ambaye ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo yaliyoanza tarehe 20 Septemba mwaka huu.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong amemshukuru Makamu huyo wa Rais kwa kutembelea banda hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Share:

TPA YAPONGEZWA KUSHIRIKI NA KUDHAMINI MAONESHO YA SITA YA KIMATAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI MKOANI GEITA.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara ameipongeza TPA kwa kushiriki na kudhamini maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofikia tamati leo tarehe 30 Septemba,2023 Katika Viwanja vya EPZ Bombambili Mjini Geita.

Amesisitiza umuhimu wa TPA kufanya Kampeni za Kimasoko ili kupanua Wigo wa biashara na Kampeni za Elimu kwa Umma ili kulinda Taswira ya TPA dhidi upotoshaji unaofifisha umuhimu wa Mamlaka yenye Mchango adhimu kwa Maendeleo ya Uchumi wa Taifa.

Maonesho haya yamefungwa na Makamu wa pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdullah


Share:

WAZIRI WA MADINI ATEMBELEA BANDA LA GGML,ASHUHUDIA MRADI WA UWANJA WA KISASA




Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Stephen Mhando akimpatia maelezo Waziri wa Madini, Anthony Mavunde kuhusu baadhi ya miradi inayotekelezwa na GGML ikiwamo ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Magogo ambao unatakelezwa na kampuni hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya GGML alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho hayo ya teknolojia ya madini yanayoendela mjini Geita
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Stephen Mhando akimpatia maelezo Waziri wa Madini, Anthony Mavunde kuhusu baadhi ya miradi inayotekelezwa na GGML ikiwamo ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Magogo ambao unatakelezwa na kampuni hiyo.


NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde ametembelea banda la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita na kupata maelezo kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa.


Waziri huyo pia alishuhudia mfano wa mradi wa uwanja wa kisasa wa michezo (Magogo Stadium) unaojengwa na GGML kwa lengo la kuendeleza michezo mkoani Geita.


Akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa GGML, Stephen Mhando alielezwa kwamba kampuni hiyo ambayo imeshiriki mara zote sita tangu maonesho hayo yaasisiwe mwaka 2018, imekuwa mdhamini mkuu na mwaka huu pia imetoa Sh milioni 150.


Mhando alimueleza pia Waziri kuwa mbali na udhamini huo mwaka huu, GGML imetoa jenereta maalumu ili kukabiliana na dharura yoyote ya umeme itakapojitokeza.


Mbali na Mavunde kutembelea idara tisa za GGML zilizopo katika maonesho hayo, pia Mhando alimueleza kuwa zaidi ya Sh bilioni 2.4 hadi sasa zimetumika katika mradi huo wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo.


“Kazi hii inaendelea na sisi GGML kama wadhamini wakuu wa Timu ya Geita Footbal Club, tunaamini kuwa uwanja utakapokamilika utakuwa moja ya chanzo cha mapato hata kwa halmashauri ya Geita,” amesema.
Share:

WAZIRI MAVUNDE AIPONGEZA TANTRADE KURATIBU NA KUSIMAMIA KLINIKI YA BIASHARA GEITA


Waziri wa Madini Anthony Mavunde (Kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), na Msimamizi Mkuu wa Kliniki ya Biashara katika Maonesho ya sita ya Teknolojia ya Madini, Bi. Samirah Mohamed (kulia), kuhusu Kliniki ya Biashara inayoratibiwa na Taasisi hiyo, kwenye Maonesho ya sita ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili Mkoani Geita, leo Septemba 29,2023.

TANTRADE imeshiriki Maonesho hayo ikisimamia Kliniki ya Biashara yenye jukumu la kutoa huduma kwa pamoja kusikiliza na kutatua changamoto za wadau na wananchi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Afisa Biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), na Msimamizi Mkuu wa Kliniki ya Biashara katika Maonesho ya sita ya Teknolojia ya Madini, Bi. Samirah Mohamed (kulia), na Bi. Clara Mwamba (Kushoto), Afisa Biashara kutoka katika Taasisi hiyo, , wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Banda lao inapofanyika Kliniki ya Biashara kwenye Maonesho ya sita ya Teknolojia ya Madini Mkoani Geita.

Afisa Biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), na Msimamizi Mkuu wa Kliniki ya Biashara katika Maonesho ya sita ya Teknolojia Katika Dekta ya Madini Bi. Samirah Mohamed (wa kwanza kulia), akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi wezeshi za Serikali zilizoshiriki kwenye Kliniki hiyo katika Maonesho hayo, Geita.

Muonekano wa Banda ya Kliniki ya Biashara katika Maonesho ya Madini Geita.
Share:

Friday 29 September 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 30,2023





Share:

JKT TANZANIA , KAGERA SUGAR HAKUNA MBABE CCM KAMBARAGE

 



Na Mwandishi wetu _ Malunde 1 blog

Timu ya JKT Tanzania wametoka thuruhu ya goli 1 - 1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye nmchezo wa ligi kuu NBC Tanzania Bara.

Mchezo huo uliochezwa leo Septemba 29, 2023 katika uwanjan wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga uliomalizika kwa droo ya goli 1 - 1 huku magoli yote yakifungwa dakika za nyongeza  goli la JKT Tanzania likifungwa na Daniel Lyanga kwa mkwaju wa penati Dk 97 huki goli la Kagera Sugar likifungwa na Gasper Mwaipasi Dk 98.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo kocha msaidizi wa timu ya JKT Tanzania George Mketo amesema makosa waliyofanya baada ya kupata goli ndio limewaadhibu na kupelekea wapinzani wao kupata goli na kufanikiwa kusawazisha.

Kwa upande wake kocha msaidizi wa timu ya Kagera Sugar Marwa Chambeli amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kufanikiwa kusawazisha goli na kugawana pointi kwenye mchezo huo.


Share:

WATAALAM UGANDA WATINGA MAONESHO YA MADINI GEITA, WAPEWA DARASA TEKNOLOJIA MPYA UCHIMBAJI MADINI


Mhandisi Uchimbaji Mwandamizi wa mipango kazi mirefu na wa chini ya ardhi kutoka GGML, Emanuel Njabugeni (kushoto) akiwaelezea wageni kutoka nchini Uganda namna GGML inavyotumia teknolojia mbalimbali katika uchimbaji wa wazi na wa chini kwa chini ya ardhi.

Na Mwandishi wetu - Geita

MAONESHO ya Teknolojia ya Madini yamezidi kuwa darasa kwa wadau mbalimbali baada ya wageni kutoka Wizara ya Madini ya Serikali ya Uganda kushiriki na kujifunza namna Kampuni ya GGML inavyotumia teknolojia za kisasa katika shughuli za uchimbaji wa chini kwa chini ya ardhi pamoja na wa wazi.


Wageni hao walioongozwa na Mkaguzi wa Migodi katika Kurugenzi ya Utafiti wa Jiolojia na Migodi anayesimamia shughuli za uchimbaji Mashariki mwa Uganda, Morris Muheirwe Tabaaro, walitembelea banda la GGML lililopo katika maonesho hayo ya sita yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili-EPZ mjini Geita.


Akizungumzia dhumuni la kutembelea maonesho hayo, Tabaaro alisema mbali na kubadilishana uzoefu, pia wamekuja kujifunza namna kampuni hiyo inafanya utafiti wa madini, uchimbaji wa madini hiyo kwa njia za wazi na chini ya ardhi.


Aidha, akizungumzia darasa alililowapatia wageni hao kutoka Uganda, Mhandisi Uchimbaji Mwandamizi wa mipango kazi mirefu na wa chini ya ardhi kutoka GGML, Emanuel Njabugeni alisema hatua hiyo imedhihirisha kuwa Tanzania imezidi kuwa mfano wa kuigwa katika shughuli za uchimbaji kupitia miongozo mbalimbali iliyowekwa na hata kufikia dira ya Taifa.


Njabugeni mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika shughuli hizo za uchimbaji, alisema katika maonesho hayo, wameelekeza wageni, wachimbaji wadogo na washiriki kuhusu matumizi sahihi ya teknoliojia ambazo zinapunguza gharama za uchimbaji lakini pia kulinda mazingira.

“Tuna teknolojia ambazo zimepiga hatua ikiwamo software ya Studio UG for under ground Pamoja na teknolojia nyingine ambazo tumewaelekeza wenzetu wa Uganda namna zinavyoweza kuwapatia faida.

“Wenzetu wa Uganda wanayo haja kubwa kujifunza kutoka kwetu sisi watanzania hasa GGML ambayo ndio mgodi mkubwa Afrika Mashariki kwani unaongoza kiteknolojia na hata uhifadhi wa mazingira.

“Kwa hiyo nimewaelekeza ni kwa namna gani GGML inatumia teknolojia hizi katika kuchimba madini na kuhifadhi mazingira jambo ambalo limekuwa faida kwetu na hata jamii inayotuzunguka kwa ujumla,” alisema na kuongeza;


“Niliwaelezea kuwa kuna kampuni ambazo tunazitumia kwa ajili ya utafiti hapa Geita, mfano GGML tunatumia kampuni ya Capital Mining Services ambao wakishatupatia hizo data tunajua kwamba hapa tutachimbaji kwa faida au hasara. Kwa kuzingatia bei ya dhahabu, vifaa ambavyo tutavitumia na gharama za rasilimali watu na gharama mbalimbali kama kujaza mashimo na kuacha mwamba katika mazingira salama.”


Hatua hiyo inakuja wakati Serikali ikiendelea na jitihada za kutekeleza dira ya 2030 ambayo imeanzishwa na Waziri wa Madini, Athony Mavunde ambaye amelenga kuhakikisha madini yawe ni utajiri na maisha ya watanzania

Share:

USAILI “INTERVIEW” SEKRETARIETI YA AJIRA DODOMA KIZUNGUMKUTI ‘JINSI MARIUM ABDUL” ALIVYONYIMWA HAKI YAKE YA MSINGI YA KUFANYA USAILI,BAADHI YA MAOFISA KUJIITA MIUNGU WATU MFANO:ALLY MTUMISHI SEKRETARIETI YA AJIRA

 


Na mwandishi Maswayetu blog;



Baada ya Serikali ya Jamhuri ya MUUNGANO kuhakikisha kwamba nafasi za kazi zote Tanzania zinatolewa kwa usawa na uwazi kwa vijana wote wanaopambana kutafuta kazi Serikalini,kumekuwa na changamoto nyingi katika usaili huo ambao wafanyakazi wake wamegeuka Miungu Mtu.

Hadithi ya Marium,inaanza Tangu alivyomaliza Chuo mwaka 2016,Chuo kikuu cha kilimo Sua shahada ya sayansi ya Kilimo. Alikuwa na mategemeo makubwa sana ya kuajiriwa kutokana na mifumo ya aliekuwa Rais wa awamu yan ne Dkt.Kikwete,lakini ndoto zake zilizimika ghafla baada ya mabadiliko ya uongozi yaliyotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambao ulimpa Nafasi ya kuongoza nchi aliekuwa Rais wa Awamu ya 5 Dkt.Magufuli.

Ajira zilisimamishwa ghafla na kumfanya Marium ambae tangu anasoma wakati huo akili yake ilikuwa kuajiriwa serikalini kupoteza uelekeo wa Maisha.Alikaa mtaani kuanzia mwaka 2016 mpaka 2022 ambapo ajira zilianza kutangazwa upya tena kupitia sekretarieti ya ajira iliyopewa mamlaka hayo.

Marium aliomba kazi zilipotangazwa na alifanikiwa kuitwa kwenye usaili Mjini Dodoma ,ambapo katika nafasi 5 zilizotangazwa waliitwa vijana Zaidi ya 3879 kugombania nafasi hizo(hii ilitokana na wingi wa wahitimu waliokosa kuajiriwa kuanzia mwaka 2016 mpaka 2022).

Tangazo hilo la usaili lilimkuta Marium akiwa mjini Moshi,hivyo kumfanya ajikusanye nauli na kufunga safari kutoka Mosho hadi Dodoma kwa ajili ya kuhakikisha anapambana kuweza kuajiriwa. Alifika Dodoma akiwa kamili na vyeti vyake,siku ilipofika aliwasili mapema yalipo majengo ya chou kikuu cha Dodoma (udom) kwa ajili ya kufanya usaili huo.

Afisa wa Ajira aitwae Ally aliwasili akiwa yeye ndio incharge wa zoezi hilo siku hiyo,alitangaza waliofika kwa ajili ya usaili shahada ya kilimo waendeo chumba namba 3,alianza kukagua vyeti kama ni original, Marium alikuwa nav yeti origina vyote ilipofika katika zoezi la vitambulisho,kitambulisho cha Marium kilikuwa kwenye simu yake (soft copy) alikataliwa na kuwekwa pembeni.Marium alishtuka sana ,akauliza anaweza kwenda kufatilia barua kwa mtendaji? Akaambiwa subiri,kumbuka ilikuwa saa 1 asubuhi,lakini walikalikshwa mpaka saa 3 asubuhi,ndipo taarifa ilitoka kwamba wanatakiwa kurudi nyumbani kwani hawana sifa ya kufanya mtihani,huku wenzao wakianza mtihani wa dk 40 muda huo.

Marium alilia sana,kumbuka kapoteza mud ana pesa ,pia alichokifata kakikosa, Alimfata Ally na kumsihi amruhusu akafanye mtihani,lakini Ally alijinasibu kwamba ana “MIAKA 10 KAZINI YA UZOEFU” hivyo hizo janja janja anazijua, na KUSEMA KWAMBA “Yeye akitamka ndio mwanzo na mwisho” hivyo waondoke tu.

Marium alirudi nyumbani na kukosa haki yake ya msingi,Lakini Mungu si Amina wala Juma,zilizotoka nafasi nyingine Marium aliomba na kufanikiwa kufika Dodoma kwa ajili ya usaili,alifanya mtihani ,akafaulu kwenda oral akiwa na maksi za juu kabisa, na sasa ameajiriwa Baraza la mitihani kama Afisa wa baraza(NECTA).

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 29,2023



 



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger