Saturday 23 September 2023

TBS WAFANYA UKAGUZI SOKONI WA BIDHAA ZILIZOISHA MUDA WA MATUMIZI MSOMERA .

...
Maafisa wa Shirika la Viwango Tanzania wakitoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara wa kijiji cha Msomera wilaya ya Handeni Tanga kuhusu umuhimu wa kusoma taarifa kwenye vifungashio ikiwemo muda wa mwisho wa matumizi wa bidhaa.

**************

Shirika la Viwango Tanzania ( TBS) , jana Septemba 22,2023 katika Kijiji Cha Msomera Wilaya ya Handeni - Tanga limefanya Ukaguzi wa Bidhaa zilizopitwa na Wakati pamoja na kutoa Elimu kwa Wafanyabiashara na Wananchi juu ya Umuhimu wa kuzingatia muda wa matumizi ya bidhaa husika hasa za Chakula.

Aidha Maafisa wa TBS wamebaini na kuziondoa sokoni baadhi ya bidhaa hasa Za Vinywaji ambazo zimepitwa na wakati na kuwasisitiza wafanyabiashara kuzingatia muda wa matumizi ya bidhaa ikiwemo na kuhakikisha wanauza bidhaa bora.

Akizungumza katika eneo la Mnada wa Msomera baada ya kumaliza zoezi la kukagua na kutoa Elimu kwa Wananchi na Wafanyabiashara, Afisa Usalama Wa Chakula kutoka kanda ya Kaskazini TBS Bi. Mariam Maarufu amesema Shirika hilo limejipanga kuhakikisha linaondoa Bidhaa hafifu sokoni ikiwemo zilizopitwa na wakati ili kulinda afya za walaji.

" Leo tupo katika kijiji cha Msomera na tumeyafikia na kufanya ukaguzi katika maduka kadhaa ambapo tumebaini na kuziondoa Sokoni bidhaa ambazo zimepitwa na wakati lakini pia tumetoa elimu kwa wananchi kuhakikisha wanaangalia muda wa mwisho wa matumizi ya bidhaa ( expire date) kabla ya kuzinunua ili kuepukana na matatizo ya kiafya ambayo yanaweza kuwakumba kutokana na matumizi ya bidhaa zilizopitwa na wakati " amesema Bi Mariam

Nao kwa nyakati Tofauti Tofauti Simon Kipondo Mfanyabiashara Msomera na Martine Oleikayo Paraketi Mwenyekiti Wa serikali ya Kijiji Cha Msomera wamelipongeza shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) kwa kuwakumbuka na kuja kufanya Ukaguzi pamoja na kutoa elimu maana imewafumbua mambo mengi hasa kuhusu matumizi ya bidhaa, Aidha wameliomba Shirika hilo kuongeza Elimu zaidi ili Kujenga uelewa zaidi kwa wananchi.Maafisa wa Shirika la Viwango Tanzania wakitoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara wa kijiji cha Msomera wilaya ya Handeni Tanga kuhusu umuhimu wa kusoma taarifa kwenye vifungashio ikiwemo muda wa mwisho wa matumizi wa bidhaa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger